Hosea 7
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 When I heal Israel, the iniquity of Ephraim will be exposed, as well as the crimes of Samaria. For they practice deceit and thieves break in; bandits raid in the streets. | SWKCV 1 kila mara nilipotaka kumponya Israeli, dhambi za Efraimu zinafichuliwa na maovu ya Samaria yanafunuliwa. Wanafanya udanganyifu, wevi huvunja nyumba, maharamia hunyangʼanya barabarani, |
| BSB 2 But they fail to consider in their hearts that I remember all their evil. Now their deeds are all around them; they are before My face. | SWKCV 2 lakini hawafahamu kwamba ninakumbuka matendo yao yote mabaya. Dhambi zao zimewameza, ziko mbele zangu siku zote. |
| BSB 3 They delight the king with their evil, and the princes with their lies. | SWKCV 3 “Wanamfurahisha sana mfalme kwa maovu yao, wakuu wao kwa uongo wao. |
| BSB 4 They are all adulterers, like an oven heated by a baker who needs not stoke the fire from the kneading to the rising of the dough. | SWKCV 4 Wote ni wazinzi, wanawaka kama tanuru ambayo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchochea kuanzia kukanda unga hadi umekwisha kuumuka. |
| BSB 5 The princes are inflamed with wine on the day of our king; so he joins hands with those who mock him. | SWKCV 5 Katika sikukuu ya mfalme wetu wakuu wanawaka kwa mvinyo, naye anawaunga mkono wenye mizaha. |
| BSB 6 For they prepare their heart like an oven while they lie in wait; all night their anger smolders; in the morning it blazes like a flaming fire. | SWKCV 6 Mioyo yao ni kama tanuru, wanamwendea kwa hila. Hasira yao inafoka moshi usiku kucha, wakati wa asubuhi inalipuka kama miali ya moto. |
| BSB 7 All of them are hot as an oven, and they devour their rulers. All their kings fall; not one of them calls upon Me. | SWKCV 7 Wote ni moto kama tanuru; wanawaangamiza watawala wao. Wafalme wake wote wanaanguka, wala hakuna yeyote kati yao aniitaye mimi. |
| BSB 8 Ephraim mixes with the nations; Ephraim is an unturned cake. | SWKCV 8 “Efraimu anajichanganya na mataifa; Efraimu ni mkate ambao haukuiva. |
| BSB 9 Foreigners consume his strength, but he does not notice. Even his hair is streaked with gray, but he does not know. | SWKCV 9 Wageni wananyonya nguvu zake, lakini hafahamu hilo. Nywele zake zina mvi hapa na pale, lakini hana habari. |
| BSB 10 Israel’s arrogance testifies against them, yet they do not return to the LORD their God; despite all this, they do not seek Him. | SWKCV 10 Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yake, lakini pamoja na haya yote harudi kwa Bwana Mungu wake wala kumtafuta. |
| BSB 11 So Ephraim has become like a silly, senseless dove—calling out to Egypt, then turning to Assyria. | SWKCV 11 “Efraimu ni kama hua, hudanganywa kwa urahisi na hana akili: mara anaita Misri, mara anageukia Ashuru. |
| BSB 12 As they go, I will spread My net over them; I will bring them down like birds of the air. I will chastise them when I hear them flocking together. | SWKCV 12 Wakati watakapokwenda, nitatupa wavu wangu juu yao; nitawavuta chini waanguke kama ndege wa angani. Nitakaposikia wakikusanyika pamoja, nitawanasa. |
| BSB 13 Woe to them, for they have strayed from Me! Destruction to them, for they have rebelled against Me! Though I would redeem them, they speak lies against Me. | SWKCV 13 Ole wao, kwa sababu wamepotoka kutoka kwangu! Maangamizi ni yao kwa sababu wameniasi! Ninatamani kuwakomboa, lakini wanasema uongo dhidi yangu. |
| BSB 14 They do not cry out to Me from their hearts when they wail upon their beds. They slash themselves for grain and new wine, but turn away from Me. | SWKCV 14 Hawanililii mimi kutoka mioyoni mwao, bali wanaomboleza vitandani mwao. Hukusanyika pamoja kwa ajili ya nafaka na divai mpya, lakini hugeukia mbali nami. |
| BSB 15 Although I trained and strengthened their arms, they plot evil against Me. | SWKCV 15 Niliwafundisha na kuwatia nguvu, lakini wanapanga mabaya dhidi yangu. |
| BSB 16 They turn, but not to the Most High; they are like a faulty bow. Their leaders will fall by the sword for the cursing of their tongue; for this they will be ridiculed in the land of Egypt. | SWKCV 16 Hawamgeukii Yeye Aliye Juu Sana, wako kama upinde wenye kasoro. Viongozi wao wataanguka kwa upanga kwa sababu ya maneno yao ya jeuri. Kwa ajili ya hili watadhihakiwa katika nchi ya Misri. |
Questions about Hosea 7? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.