Job 5
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “Call out if you please, but who will answer? To which of the holy ones will you turn? | SWKCV 1 “Ita kama unataka, lakini ni nani atakayekujibu? Ni yupi kati ya hao watakatifu utakayemgeukia? |
| BSB 2 For resentment kills a fool, and envy slays the simple. | SWKCV 2 Kuweka uchungu moyoni humuua mpumbavu, nao wivu humchinja mjinga. |
| BSB 3 I have seen a fool taking root, but suddenly his house was cursed. | SWKCV 3 Mimi mwenyewe nimemwona mpumbavu akistawi, lakini ghafula nyumba yake ikawa imelaaniwa. |
| BSB 4 His sons are far from safety, crushed in court without a defender. | SWKCV 4 Watoto wake wako mbali na usalama, hushindwa mahakamani bila mtetezi. |
| BSB 5 The hungry consume his harvest, taking it even from the thorns, and the thirsty pant after his wealth. | SWKCV 5 Wenye njaa huyala mavuno yake, wakiyatoa hata katikati ya miiba, nao wenye kiu huitamani sana mali yake. |
| BSB 6 For distress does not spring from the dust, and trouble does not sprout from the ground. | SWKCV 6 Kwa maana taabu haioti kutoka kwenye udongo, wala udhia hauchipui kutoka ardhini. |
| BSB 7 Yet man is born to trouble as surely as sparks fly upward. | SWKCV 7 Lakini mwanadamu huzaliwa ili kutaabika, kwa hakika kama cheche za moto zirukavyo kuelekea juu. |
| BSB 8 However, if I were you, I would appeal to God and lay my cause before Him— | SWKCV 8 “Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu, ningeliweka shauri langu mbele zake. |
| BSB 9 the One who does great and unsearchable things, wonders without number. | SWKCV 9 Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, miujiza isiyoweza kuhesabika. |
| BSB 10 He gives rain to the earth and sends water upon the fields. | SWKCV 10 Yeye huipa nchi mvua, huyapeleka maji kunyesha mashamba. |
| BSB 11 He sets the lowly on high, so that mourners are lifted to safety. | SWKCV 11 Huwainua juu wanyonge, nao wale waombolezao huinuliwa wakawa salama. |
| BSB 12 He thwarts the schemes of the crafty, so that their hands find no success. | SWKCV 12 Huipinga mipango ya wenye hila, ili mikono yao isifikie ufanisi. |
| BSB 13 He catches the wise in their craftiness, and sweeps away the plans of the cunning. | SWKCV 13 Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao, nayo mipango ya wadanganyifu huifagilia mbali. |
| BSB 14 They encounter darkness by day and grope at noon as in the night. | SWKCV 14 Giza huwapata wakati wa mchana; wakati wa adhuhuri hupapasa kama vile usiku. |
| BSB 15 He saves the needy from the sword in their mouth and from the clutches of the powerful. | SWKCV 15 Humwokoa mhitaji kutokana na upanga ulioko kinywani mwao; huwaokoa kutokana na makucha ya wenye nguvu. |
| BSB 16 So the poor have hope, and injustice shuts its mouth. | SWKCV 16 Kwa hiyo maskini analo tarajio, nao udhalimu hufumba kinywa chake. |
| BSB 17 Blessed indeed is the man whom God corrects; so do not despise the discipline of the Almighty. | SWKCV 17 “Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi; kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi. |
| BSB 18 For He wounds, but He also binds; He strikes, but His hands also heal. | SWKCV 18 Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga; huumiza, lakini mikono yake pia huponya. |
| BSB 19 He will rescue you from six calamities; no harm will touch you in seven. | SWKCV 19 Kutoka majanga sita atakuokoa; naam, hata katika saba hakuna dhara litakalokupata wewe. |
| BSB 20 In famine He will redeem you from death, and in battle from the stroke of the sword. | SWKCV 20 Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo, naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga. |
| BSB 21 You will be hidden from the scourge of the tongue, and will not fear havoc when it comes. | SWKCV 21 Utalindwa kutokana na kichapo cha ulimi, wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia. |
| BSB 22 You will laugh at destruction and famine, and need not fear the beasts of the earth. | SWKCV 22 Utayacheka maangamizo na njaa, wala hutakuwa na sababu ya kuwaogopa wanyama wakali wa mwituni. |
| BSB 23 For you will have a covenant with the stones of the field, and the wild animals will be at peace with you. | SWKCV 23 Kwa kuwa utakuwa na agano na mawe ya mashamba, nao wanyama wa mwitu watakuwa na amani nawe. |
| BSB 24 You will know that your tent is secure, and find nothing amiss when inspecting your home. | SWKCV 24 Utajua ya kwamba hema lako li salama; utahesabu mali zako wala hutakuta chochote kilichopungua. |
| BSB 25 You will know that your offspring will be many, your descendants like the grass of the earth. | SWKCV 25 Utajua ya kuwa watoto wako watakuwa wengi, nao wazao wako wengi kama majani ya nchi. |
| BSB 26 You will come to the grave in full vigor, like a sheaf of grain gathered in season. | SWKCV 26 Utaingia kaburini ukiwa na umri wa uzee mtimilifu, kama masuke ya ngano yakusanywapo kwa wakati wake. |
| BSB 27 Indeed, we have investigated, and it is true! So hear it and know for yourself.” | SWKCV 27 “Tumelichunguza hili, nalo ni kweli. Hivyo lisikie na ulitendee kazi.” |
Questions about Job 5? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.