Joshua 12
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now these are the kings of the land whom the Israelites struck down and whose lands they took beyond the Jordan to the east, from the Arnon Valley to Mount Hermon, including all the Arabah eastward: | SWKCV 1 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba: |
| BSB 2 Sihon king of the Amorites, who lived in Heshbon. He ruled from Aroer on the rim of the Arnon Valley, along the middle of the valley, up to the Jabbok River (the border of the Ammonites), that is, half of Gilead, | SWKCV 2 Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi. |
| BSB 3 as well as the Arabah east of the Sea of Chinnereth to the Sea of the Arabah (the Salt Sea), eastward through Beth-jeshimoth, and southward below the slopes of Pisgah. | SWKCV 3 Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi ), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga. |
| BSB 4 And Og king of Bashan, one of the remnant of the Rephaim, who lived in Ashtaroth and Edrei. | SWKCV 4 Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei. |
| BSB 5 He ruled over Mount Hermon, Salecah, all of Bashan up to the border of the Geshurites and Maacathites, and half of Gilead to the border of Sihon king of Heshbon. | SWKCV 5 Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni. |
| BSB 6 Moses, the servant of the LORD, and the Israelites had struck them down and given their land as an inheritance to the Reubenites, the Gadites, and the half-tribe of Manasseh. | SWKCV 6 Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao. |
| BSB 7 And these are the kings of the land that Joshua and the Israelites conquered beyond the Jordan to the west, from Baal-gad in the Valley of Lebanon to Mount Halak, which rises toward Seir (according to the allotments to the tribes of Israel, Joshua gave them as an inheritance | SWKCV 7 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao: |
| BSB 8 the hill country, the foothills, the Arabah, the slopes, the wilderness, and the Negev—the lands of the Hittites, Amorites, Canaanites, Perizzites, Hivites, and Jebusites): | SWKCV 8 nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi): |
| BSB 9 the king of Jericho, one; the king of Ai, which is near Bethel, one; | SWKCV 9 mfalme wa Yeriko mmoja mfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja |
| BSB 10 the king of Jerusalem, one; the king of Hebron, one; | SWKCV 10 mfalme wa Yerusalemu mmoja mfalme wa Hebroni mmoja |
| BSB 11 the king of Jarmuth, one; the king of Lachish, one; | SWKCV 11 mfalme wa Yarmuthi mmoja mfalme wa Lakishi mmoja |
| BSB 12 the king of Eglon, one; the king of Gezer, one; | SWKCV 12 mfalme wa Egloni mmoja mfalme wa Gezeri mmoja |
| BSB 13 the king of Debir, one; the king of Geder, one; | SWKCV 13 mfalme wa Debiri mmoja mfalme wa Gederi mmoja |
| BSB 14 the king of Hormah, one; the king of Arad, one; | SWKCV 14 mfalme wa Horma mmoja mfalme wa Aradi mmoja |
| BSB 15 the king of Libnah, one; the king of Adullam, one; | SWKCV 15 mfalme wa Libna mmoja mfalme wa Adulamu mmoja |
| BSB 16 the king of Makkedah, one; the king of Bethel, one; | SWKCV 16 mfalme wa Makeda mmoja mfalme wa Betheli mmoja |
| BSB 17 the king of Tappuah, one; the king of Hepher, one; | SWKCV 17 mfalme wa Tapua mmoja mfalme wa Heferi mmoja |
| BSB 18 the king of Aphek, one; the king of Lasharon, one; | SWKCV 18 mfalme wa Afeki mmoja mfalme wa Lasharoni mmoja |
| BSB 19 the king of Madon, one; the king of Hazor, one; | SWKCV 19 mfalme wa Madoni mmoja mfalme wa Hazori mmoja |
| BSB 20 the king of Shimron-meron, one; the king of Achshaph, one; | SWKCV 20 mfalme wa Shimron-Meroni mmoja mfalme wa Akishafu mmoja |
| BSB 21 the king of Taanach, one; the king of Megiddo, one; | SWKCV 21 mfalme wa Taanaki mmoja mfalme wa Megido mmoja |
| BSB 22 the king of Kedesh, one; the king of Jokneam in Carmel, one; | SWKCV 22 mfalme wa Kedeshi mmoja mfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja |
| BSB 23 the king of Dor in Naphath-dor, one; the king of Goiim in Gilgal, one; | SWKCV 23 mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) mmoja mfalme wa Goimu katika Gilgali mmoja |
| BSB 24 and the king of Tirzah, one. So there were thirty-one kings in all. | SWKCV 24 mfalme wa Tirsa mmoja wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja. |
Questions about Joshua 12? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.