Luke 17
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Jesus said to His disciples, “It is inevitable that stumbling blocks will come, but woe to the one through whom they come! | SWKCV 1 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mambo yanayosababisha watu watende dhambi hayana budi kutukia. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha. |
| BSB 2 It would be better for him to have a millstone hung around his neck and to be thrown into the sea than to cause one of these little ones to stumble. | SWKCV 2 Ingekuwa heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutoswa baharini, kuliko kumsababisha mmojawapo wa hawa wadogo kutenda dhambi. |
| BSB 3 Watch yourselves. If your brother sins, rebuke him; and if he repents, forgive him. | SWKCV 3 Kwa hiyo, jilindeni. “Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu, msamehe. |
| BSB 4 Even if he sins against you seven times in a day, and seven times returns to say, ‘I repent,’ you must forgive him.” | SWKCV 4 Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, ‘Ninatubu,’ msamehe.” |
| BSB 5 The apostles said to the Lord, “Increase our faith!” | SWKCV 5 Mitume wake wakamwambia Bwana, “Tuongezee imani.” |
| BSB 6 And the Lord answered, “If you have faith the size of a mustard seed, you can say to this mulberry tree, ‘Be uprooted and planted in the sea,’ and it will obey you. | SWKCV 6 Bwana akawajibu, “Kama mkiwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘Ngʼoka ukaote baharini,’ nao ungewatii. |
| BSB 7 Which of you whose servant comes in from plowing or shepherding in the field will say to him, ‘Come at once and sit down to eat’? | SWKCV 7 “Ikiwa mmoja wenu ana mtumishi anayelima shambani au anayechunga kondoo, je, mtumishi huyo arudipo atamwambia, ‘Karibu hapa keti ule chakula?’ |
| BSB 8 Instead, won’t he tell him, ‘Prepare my meal and dress yourself to serve me while I eat and drink, and afterward you may eat and drink’? | SWKCV 8 Je, badala yake, hatamwambia, ‘Niandalie chakula, nile, jifunge unitumikie ninapokula na kunywa; baadaye waweza kula na kunywa?’ |
| BSB 9 Does he thank the servant because he did what he was told? | SWKCV 9 Je, huyo mtu atamshukuru mtumishi huyo kwa kutimiza yale aliyoamriwa? |
| BSB 10 So you also, when you have done everything commanded of you, should say, ‘We are unworthy servants; we have only done our duty.’” | SWKCV 10 Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi tu watumishi tusiostahili; tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.’” |
| BSB 11 While Jesus was on His way to Jerusalem, He was passing between Samaria and Galilee. | SWKCV 11 Yesu alipokuwa njiani akienda Yerusalemu, alipitia mpakani mwa Samaria na Galilaya. |
| BSB 12 As He entered one of the villages, He was met by ten lepers. They stood at a distance | SWKCV 12 Alipokuwa akiingia kwenye kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma wakakutana naye. Wakasimama mbali, |
| BSB 13 and raised their voices, shouting, “Jesus, Master, have mercy on us!” | SWKCV 13 wakapaza sauti, wakasema, “Yesu, Bwana, tuhurumie!” |
| BSB 14 When Jesus saw them, He said, “Go, show yourselves to the priests.” And as they were on their way, they were cleansed. | SWKCV 14 Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Nao walipokuwa njiani wakienda, wakatakasika. |
| BSB 15 When one of them saw that he was healed, he came back, praising God in a loud voice. | SWKCV 15 Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Yesu, akimsifu Mungu kwa sauti kuu. |
| BSB 16 He fell facedown at Jesus’ feet in thanksgiving to Him—and he was a Samaritan. | SWKCV 16 Akajitupa miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria. |
| BSB 17 “Were not all ten cleansed?” Jesus asked. “Where then are the other nine? | SWKCV 17 Yesu akauliza, “Je, hawakutakaswa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? |
| BSB 18 Was no one found except this foreigner to return and give glory to God?” | SWKCV 18 Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumshukuru Mungu isipokuwa huyu mgeni?” |
| BSB 19 Then Jesus said to him, “Rise and go; your faith has made you well!” | SWKCV 19 Yesu akamwambia, “Inuka na uende zako, imani yako imekuponya.” |
| BSB 20 When asked by the Pharisees when the kingdom of God would come, Jesus replied, “The kingdom of God will not come with observable signs. | SWKCV 20 Yesu alipoulizwa na Mafarisayo Ufalme wa Mungu utakuja lini, yeye akawajibu, “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuchunguza kwa bidii, |
| BSB 21 Nor will people say, ‘Look, here it is,’ or ‘There it is.’ For you see, the kingdom of God is in your midst.” | SWKCV 21 wala watu hawatasema, ‘Huu hapa,’ au ‘Ule kule,’ kwa maana Ufalme wa Mungu umo ndani yenu.” |
| BSB 22 Then He said to the disciples, “The time is coming when you will long to see one of the days of the Son of Man, but you will not see it. | SWKCV 22 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona. |
| BSB 23 People will tell you, ‘Look, there He is!’ or ‘Look, here He is!’ Do not go out or chase after them. | SWKCV 23 Watu watawaambia, ‘Yule kule!’ Au, ‘Huyu hapa!’ Msiwakimbilie. |
| BSB 24 For just as the lightning flashes and lights up the sky from one end to the other, so will be the Son of Man in His day. | SWKCV 24 Kwa maana kama vile umeme wa radi umulikavyo katika anga kuanzia mwisho mmoja hadi mwingine, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake. |
| BSB 25 But first He must suffer many things and be rejected by this generation. | SWKCV 25 Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki. |
| BSB 26 Just as it was in the days of Noah, so also will it be in the days of the Son of Man: | SWKCV 26 “Kama ilivyokuwa siku za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Adamu. |
| BSB 27 People were eating and drinking, marrying and being given in marriage, up to the day Noah entered the ark. Then the flood came and destroyed them all. | SWKCV 27 Watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Noa alipoingia katika safina. Ndipo gharika ikaja na kuwaangamiza wote. |
| BSB 28 It was the same in the days of Lot: People were eating and drinking, buying and selling, planting and building. | SWKCV 28 “Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Loti: Watu walikuwa wakila na kunywa, wakinunua na kuuza, wakilima na kujenga. |
| BSB 29 But on the day Lot left Sodom, fire and sulfur rained down from heaven and destroyed them all. | SWKCV 29 Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka mbinguni ukawaangamiza wote. |
| BSB 30 It will be just like that on the day the Son of Man is revealed. | SWKCV 30 “Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Adamu atakapofunuliwa. |
| BSB 31 On that day, let no one on the housetop come down to retrieve his possessions. Likewise, let no one in the field return for anything he has left behind. | SWKCV 31 Siku hiyo, mtu yeyote aliye juu ya dari ya nyumba yake, hata vitu vyake vikiwa ndani ya hiyo nyumba, asishuke kuvichukua. Vivyo hivyo mtu aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua chochote. |
| BSB 32 Remember Lot’s wife! | SWKCV 32 Mkumbukeni mke wa Loti! |
| BSB 33 Whoever tries to save his life will lose it, but whoever loses his life will preserve it. | SWKCV 33 Mtu yeyote anayejaribu kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote atakayeyapoteza maisha yake atayaokoa. |
| BSB 34 I tell you, on that night two people will be in one bed: one will be taken and the other left. | SWKCV 34 Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa wamelala kitanda kimoja; naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa. |
| BSB 35 Two women will be grinding grain together: one will be taken and the other left.” | SWKCV 35 Wanawake wawili watakuwa wanasaga nafaka pamoja; naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa. [ |
| BSB | SWKCV 36 Wanaume wawili watakuwa wanafanya kazi pamoja shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.]” |
| BSB 37 “Where, Lord?” they asked. Jesus answered, “Wherever there is a carcass, there the vultures will gather.” | SWKCV 37 Kisha wakamuuliza, “Haya yatatukia wapi Bwana?” Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, huko ndiko tai watakapokusanyika.” |
Questions about Luke 17? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.