Luke 3
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 In the fifteenth year of the reign of Tiberius Caesar, while Pontius Pilate was governor of Judea, Herod tetrarch of Galilee, his brother Philip tetrarch of Ituraea and Trachonitis, and Lysanias tetrarch of Abilene, | SWKCV 1 Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Uyahudi, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania akiwa mfalme wa Abilene, |
| BSB 2 during the high priesthood of Annas and Caiaphas, the word of God came to John son of Zechariah in the wilderness. | SWKCV 2 nao Anasi na Kayafa wakiwa makuhani wakuu, neno la Mungu likamjia Yohana, mwana wa Zekaria huko jangwani. |
| BSB 3 He went into all the region around the Jordan, preaching a baptism of repentance for the forgiveness of sins, | SWKCV 3 Akaenda katika nchi yote kandokando ya Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. |
| BSB 4 as it is written in the book of the words of Isaiah the prophet: “A voice of one calling in the wilderness, ‘Prepare the way for the Lord, make straight paths for Him. | SWKCV 4 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Itengenezeni njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake. |
| BSB 5 Every valley shall be filled in, and every mountain and hill made low. The crooked ways shall be made straight, and the rough ways smooth. | SWKCV 5 Kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima vitashushwa. Njia zilizopinda zitanyooshwa, na zilizoparuza zitasawazishwa. |
| BSB 6 And all humanity will see God’s salvation.’” | SWKCV 6 Nao watu wote watauona wokovu wa Mungu.’” |
| BSB 7 Then John said to the crowds coming out to be baptized by him, “You brood of vipers, who warned you to flee from the coming wrath? | SWKCV 7 Yohana akauambia ule umati wa watu uliokuwa unakuja ili kubatizwa naye, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? |
| BSB 8 Produce fruit, then, in keeping with repentance. And do not begin to say to yourselves, ‘We have Abraham as our father.’ For I tell you that out of these stones God can raise up children for Abraham. | SWKCV 8 Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Abrahamu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka mawe haya. |
| BSB 9 The axe lies ready at the root of the trees, and every tree that does not produce good fruit will be cut down and thrown into the fire.” | SWKCV 9 Hata sasa shoka limeshawekwa tayari kwenye shina la kila mti. Basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.” |
| BSB 10 The crowds asked him, “What then should we do?” | SWKCV 10 Ule umati wa watu ukamuuliza, “Inatupasa tufanyeje basi?” |
| BSB 11 John replied, “Whoever has two tunics should share with him who has none, and whoever has food should do the same.” | SWKCV 11 Yohana akawaambia, “Aliye na kanzu mbili amgawie asiye nayo, naye aliye na chakula na afanye vivyo hivyo.” |
| BSB 12 Even tax collectors came to be baptized. “Teacher,” they asked, “what should we do?” | SWKCV 12 Watoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamuuliza, “Bwana na sisi inatupasa tufanyeje?” |
| BSB 13 “Collect no more than you are authorized,” he answered. | SWKCV 13 Akawaambia, “Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa.” |
| BSB 14 Then some soldiers asked him, “And what should we do?” “Do not take money by force or false accusation,” he said. “Be content with your wages.” | SWKCV 14 Askari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?” Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.” |
| BSB 15 The people were waiting expectantly and were all wondering in their hearts if John could be the Christ. | SWKCV 15 Watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yohana angeweza kuwa ndiye Kristo. |
| BSB 16 John answered all of them: “I baptize you with water, but One more powerful than I will come, the straps of whose sandals I am not worthy to untie. He will baptize you with the Holy Spirit and with fire. | SWKCV 16 Yohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji. Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. |
| BSB 17 His winnowing fork is in His hand to clear His threshing floor and to gather the wheat into His barn; but He will burn up the chaff with unquenchable fire.” | SWKCV 17 Pepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.” |
| BSB 18 With these and many other exhortations, John proclaimed the good news to the people. | SWKCV 18 Basi, kwa maonyo mengine mengi Yohana aliwasihi na kuwahubiria watu Habari Njema. |
| BSB 19 But when he rebuked Herod the tetrarch regarding his brother’s wife Herodias and all the evils he had done, | SWKCV 19 Lakini Yohana alipomkemea Mfalme Herode kuhusu uhusiano wake na Herodia, mke wa ndugu yake, na maovu mengine aliyokuwa amefanya, |
| BSB 20 Herod added this to them all: He locked John up in prison. | SWKCV 20 Herode aliongezea jambo hili kwa hayo mengine yote: alimfunga Yohana gerezani. |
| BSB 21 When all the people were being baptized, Jesus was baptized too. And as He was praying, heaven was opened, | SWKCV 21 Baada ya watu wote kubatizwa, Yesu naye akabatizwa. Naye alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka. |
| BSB 22 and the Holy Spirit descended on Him in a bodily form like a dove. And a voice came from heaven: “You are My beloved Son; in You I am well pleased.” | SWKCV 22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua, nayo sauti kutoka mbinguni ikasema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.” |
| BSB 23 Jesus Himself was about thirty years old when He began His ministry. He was regarded as the son of Joseph, the son of Heli, | SWKCV 23 Yesu alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza huduma yake. Alikuwa akidhaniwa kuwa mwana wa Yosefu, Yosefu alikuwa mwana wa Eli, |
| BSB 24 the son of Matthat, the son of Levi, the son of Melchi, the son of Jannai, the son of Joseph, | SWKCV 24 Eli alikuwa mwana wa Mathati, Mathati alikuwa mwana wa Lawi, Lawi alikuwa mwana wa Melki, Melki alikuwa mwana wa Yanai, Yanai alikuwa mwana wa Yosefu, |
| BSB 25 the son of Mattathias, the son of Amos, the son of Nahum, the son of Esli, the son of Naggai, | SWKCV 25 Yosefu alikuwa mwana wa Matathia, Matathia alikuwa mwana wa Amosi, Amosi alikuwa mwana wa Nahumu, Nahumu alikuwa mwana wa Esli, Esli alikuwa mwana wa Nagai, |
| BSB 26 the son of Maath, the son of Mattathias, the son of Semein, the son of Josech, the son of Joda, | SWKCV 26 Nagai alikuwa mwana wa Maathi, Maathi alikuwa mwana wa Matathia, Matathia alikuwa mwana wa Semeini, Semeini alikuwa mwana wa Yoseki, Yoseki alikuwa mwana wa Yoda, |
| BSB 27 the son of Joanan, the son of Rhesa, the son of Zerubbabel, the son of Shealtiel, the son of Neri, | SWKCV 27 Yoda alikuwa mwana wa Yoanani, Yoanani alikuwa mwana wa Resa, Resa alikuwa mwana wa Zerubabeli, Zerubabeli alikuwa mwana wa Shealtieli, Shealtieli alikuwa mwana wa Neri, |
| BSB 28 the son of Melchi, the son of Addi, the son of Cosam, the son of Elmadam, the son of Er, | SWKCV 28 Neri alikuwa mwana wa Melki, Melki alikuwa mwana wa Adi, Adi alikuwa mwana wa Kosamu, Kosamu alikuwa mwana wa Elmadamu, Elmadamu alikuwa mwana wa Eri, |
| BSB 29 the son of Joshua, the son of Eliezer, the son of Jorim, the son of Matthat, the son of Levi, | SWKCV 29 Eri alikuwa mwana wa Yoshua, Yoshua alikuwa mwana wa Eliezeri, Eliezeri alikuwa mwana wa Yorimu, Yorimu alikuwa mwana wa Mathati, Mathati alikuwa mwana wa Lawi, |
| BSB 30 the son of Simeon, the son of Judah, the son of Joseph, the son of Jonam, the son of Eliakim, | SWKCV 30 Lawi alikuwa mwana wa Simeoni, Simeoni alikuwa mwana wa Yuda, Yuda alikuwa mwana wa Yosefu, Yosefu alikuwa mwana wa Yonamu, Yonamu alikuwa mwana wa Eliakimu, Eliakimu alikuwa mwana wa Melea, |
| BSB 31 the son of Melea, the son of Menna, the son of Mattatha, the son of Nathan, the son of David, | SWKCV 31 Melea alikuwa mwana wa Mena, Mena alikuwa mwana wa Matatha, Matatha alikuwa mwana wa Nathani, Nathani alikuwa mwana wa Daudi, |
| BSB 32 the son of Jesse, the son of Obed, the son of Boaz, the son of Sala, the son of Nahshon, | SWKCV 32 Daudi alikuwa mwana wa Yese, Yese alikuwa mwana wa Obedi, Obedi alikuwa mwana wa Boazi, Boazi alikuwa mwana wa Salmoni, Salmoni alikuwa mwana wa Nashoni, |
| BSB 33 the son of Amminadab, the son of Admin, the son of Arni, the son of Hezron, the son of Perez, the son of Judah, | SWKCV 33 Nashoni alikuwa mwana wa Aminadabu, Aminadabu alikuwa mwana wa Aramu, Aramu alikuwa mwana wa Hesroni, Hesroni alikuwa mwana wa Peresi, Peresi alikuwa mwana wa Yuda, |
| BSB 34 the son of Jacob, the son of Isaac, the son of Abraham, the son of Terah, the son of Nahor, | SWKCV 34 Yuda alikuwa mwana wa Yakobo, Yakobo alikuwa mwana wa Isaki, Isaki alikuwa mwana wa Abrahamu, Abrahamu alikuwa mwana wa Tera, Tera alikuwa mwana wa Nahori, |
| BSB 35 the son of Serug, the son of Reu, the son of Peleg, the son of Eber, the son of Shelah, | SWKCV 35 Nahori alikuwa mwana wa Serugi, Serugi alikuwa mwana wa Reu, Reu alikuwa mwana wa Pelegi, Pelegi alikuwa mwana wa Eberi, Eberi alikuwa mwana wa Sala, |
| BSB 36 the son of Cainan, the son of Arphaxad, the son of Shem, the son of Noah, the son of Lamech, | SWKCV 36 Sala alikuwa mwana wa Kenani, Kenani alikuwa mwana wa Arfaksadi, Arfaksadi alikuwa mwana wa Shemu, Shemu alikuwa mwana wa Noa, Noa alikuwa mwana wa Lameki, |
| BSB 37 the son of Methuselah, the son of Enoch, the son of Jared, the son of Mahalalel, the son of Cainan, | SWKCV 37 Lameki alikuwa mwana wa Methusela, Methusela alikuwa mwana wa Enoki, Enoki alikuwa mwana wa Yaredi, Yaredi alikuwa mwana wa Mahalaleli, Mahalaleli alikuwa mwana wa Kenani, |
| BSB 38 the son of Enosh, the son of Seth, the son of Adam, the son of God. | SWKCV 38 Kenani alikuwa mwana wa Enoshi, Enoshi alikuwa mwana wa Sethi, Sethi alikuwa mwana wa Adamu, Adamu alikuwa mwana wa Mungu. |
Questions about Luke 3? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.