Matthew 16
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then the Pharisees and Sadducees came and tested Jesus by asking Him to show them a sign from heaven. | SWKCV 1 Mafarisayo na Masadukayo wakamjia Yesu na kumjaribu kwa kumwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni. |
| BSB 2 But He replied, “When evening comes, you say, ‘The weather will be fair, for the sky is red,’ | SWKCV 2 Yesu akawajibu, “Ifikapo jioni, mnasema, ‘Hali ya hewa itakuwa nzuri, kwa kuwa anga ni nyekundu.’ |
| BSB 3 and in the morning, ‘Today it will be stormy, for the sky is red and overcast.’ You know how to interpret the appearance of the sky, but not the signs of the times. | SWKCV 3 Nanyi wakati wa asubuhi mnasema, ‘Leo kutakuwa na dhoruba, kwa sababu anga ni nyekundu na mawingu yametanda.’ Mnajua jinsi ya kupambanua kule kuonekana kwa anga, lakini hamwezi kupambanua dalili za nyakati. |
| BSB 4 A wicked and adulterous generation demands a sign, but none will be given it except the sign of Jonah.” Then He left them and went away. | SWKCV 4 Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya Yona.” Yesu akawaacha, akaenda zake. |
| BSB 5 When they crossed to the other side, the disciples forgot to take bread. | SWKCV 5 Wanafunzi wake walipofika ngʼambo ya bahari, walikuwa wamesahau kuchukua mikate. |
| BSB 6 “Watch out!” Jesus told them. “Beware of the leaven of the Pharisees and Sadducees.” | SWKCV 6 Yesu akawaambia, “Jihadharini. Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo.” |
| BSB 7 They discussed this among themselves and concluded, “It is because we did not bring any bread.” | SWKCV 7 Wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, “Ni kwa sababu hatukuleta mikate.” |
| BSB 8 Aware of their conversation, Jesus said, “You of little faith, why are you debating among yourselves about having no bread? | SWKCV 8 Yesu, akifahamu majadiliano yao, akauliza, “Enyi wa imani haba! Mbona mnajadiliana miongoni mwenu kuhusu kutokuwa na mikate? |
| BSB 9 Do you still not understand? Do you not remember the five loaves for the five thousand, and how many basketfuls you gathered? | SWKCV 9 Je, bado hamwelewi? Je, hamkumbuki ile mikate mitano iliyolisha watu 5,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya? |
| BSB 10 Or the seven loaves for the four thousand, and how many basketfuls you gathered? | SWKCV 10 Au ile mikate saba iliyolisha watu 4,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya? |
| BSB 11 How do you not understand that I was not telling you about bread? But beware of the leaven of the Pharisees and Sadducees.” | SWKCV 11 Inakuwaje mnashindwa kuelewa kwamba nilikuwa sisemi nanyi habari za mikate? Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.” |
| BSB 12 Then they understood that He was not telling them to beware of the leaven used in bread, but of the teaching of the Pharisees and Sadducees. | SWKCV 12 Ndipo wakaelewa kwamba alikuwa hasemi juu ya chachu ya kutengeneza mikate, bali juu ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo. |
| BSB 13 When Jesus came to the region of Caesarea Philippi, He questioned His disciples: “Who do people say the Son of Man is?” | SWKCV 13 Basi Yesu alipofika katika eneo la Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake, “Watu husema kwamba mimi Mwana wa Adamu ni nani?” |
| BSB 14 They replied, “Some say John the Baptist; others say Elijah; and still others, Jeremiah or one of the prophets.” | SWKCV 14 Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji; wengine husema ni Eliya; na bado wengine husema ni Yeremia au mmojawapo wa manabii.” |
| BSB 15 “But what about you?” Jesus asked. “Who do you say I am?” | SWKCV 15 Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?” |
| BSB 16 Simon Peter answered, “You are the Christ, the Son of the living God.” | SWKCV 16 Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” |
| BSB 17 Jesus replied, “Blessed are you, Simon son of Jonah! For this was not revealed to you by flesh and blood, but by My Father in heaven. | SWKCV 17 Naye Yesu akamwambia, “Heri wewe, Simoni Bar-Yona, kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni. |
| BSB 18 And I tell you that you are Peter, and on this rock I will build My church, and the gates of Hades will not prevail against it. | SWKCV 18 Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kulishinda. |
| BSB 19 I will give you the keys of the kingdom of heaven. Whatever you bind on earth will be bound in heaven, and whatever you loose on earth will be loosed in heaven.” | SWKCV 19 Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, nalo lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.” |
| BSB 20 Then He admonished the disciples not to tell anyone that He was the Christ. | SWKCV 20 Kisha akawakataza wanafunzi wake wasimwambie mtu yeyote kwamba yeye ndiye Kristo. |
| BSB 21 From that time on Jesus began to show His disciples that He must go to Jerusalem and suffer many things at the hands of the elders, chief priests, and scribes, and that He must be killed and on the third day be raised to life. | SWKCV 21 Tangu wakati huo, Yesu alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi mikononi mwa wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na kwamba itampasa auawe lakini siku ya tatu kufufuliwa. |
| BSB 22 Peter took Him aside and began to rebuke Him. “Far be it from You, Lord!” he said. “This shall never happen to You!” | SWKCV 22 Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea akisema, “Haiwezekani, Bwana! Jambo hili kamwe halitakupata!” |
| BSB 23 But Jesus turned and said to Peter, “Get behind Me, Satan! You are a stumbling block to Me. For you do not have in mind the things of God, but the things of men.” | SWKCV 23 Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.” |
| BSB 24 Then Jesus told His disciples, “If anyone wants to come after Me, he must deny himself and take up his cross and follow Me. | SWKCV 24 Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. |
| BSB 25 For whoever wants to save his life will lose it, but whoever loses his life for My sake will find it. | SWKCV 25 Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata. |
| BSB 26 What will it profit a man if he gains the whole world, yet forfeits his soul? Or what can a man give in exchange for his soul? | SWKCV 26 Kwa maana, je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? |
| BSB 27 For the Son of Man will come in His Father’s glory with His angels, and then He will repay each one according to what he has done. | SWKCV 27 Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. |
| BSB 28 Truly I tell you, some who are standing here will not taste death before they see the Son of Man coming in His kingdom.” | SWKCV 28 Nawaambia kweli, baadhi yenu hapa hawataonja mauti kabla ya kumwona Mwana wa Adamu akija katika Ufalme wake.” |
Questions about Matthew 16? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.