Matthew 15
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then some Pharisees and scribes came to Jesus from Jerusalem and asked, | SWKCV 1 Ndipo baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria wakamjia Yesu kutoka Yerusalemu na kumuuliza, |
| BSB 2 “Why do Your disciples break the tradition of the elders? They do not wash their hands before they eat.” | SWKCV 2 “Mbona wanafunzi wako wanakiuka mapokeo ya wazee? Kwa maana wao hawanawi mikono yao kabla ya kula!” |
| BSB 3 Jesus replied, “And why do you break the command of God for the sake of your tradition? | SWKCV 3 Yesu akawajibu, “Mbona ninyi mnavunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? |
| BSB 4 For God said, ‘Honor your father and mother’ and ‘Anyone who curses his father or mother must be put to death.’ | SWKCV 4 Kwa maana Mungu alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ |
| BSB 5 But you say that if anyone says to his father or mother, ‘Whatever you would have received from me is a gift devoted to God,’ | SWKCV 5 Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia kimewekwa wakfu kwa Mungu,’ |
| BSB 6 he need not honor his father or mother with it. Thus you nullify the word of God for the sake of your tradition. | SWKCV 6 basi hana tena sababu ya kumheshimu baba yake nacho. Basi kwa ajili ya mafundisho yenu mnavunja amri ya Mungu. |
| BSB 7 You hypocrites! Isaiah prophesied correctly about you: | SWKCV 7 Ninyi wanafiki! Isaya alikuwa sawa alipotabiri juu yenu kwamba: |
| BSB 8 ‘These people honor Me with their lips, but their hearts are far from Me. | SWKCV 8 “ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. |
| BSB 9 They worship Me in vain; they teach as doctrine the precepts of men.’” | SWKCV 9 Huniabudu bure; nayo mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu tu.’” |
| BSB 10 Jesus called the crowd to Him and said, “Listen and understand. | SWKCV 10 Yesu akaita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni na mwelewe: |
| BSB 11 A man is not defiled by what enters his mouth, but by what comes out of it.” | SWKCV 11 kinachomfanya mtu kuwa najisi mbele za Mungu si kile kiingiacho kinywani mwake, bali ni kile kitokacho kinywani mwake.” |
| BSB 12 Then the disciples came to Him and said, “Are You aware that the Pharisees were offended when they heard this?” | SWKCV 12 Kisha wanafunzi wake wakamjia na kumuuliza, “Je, unajua kwamba Mafarisayo walichukizwa sana waliposikia yale uliyosema?” |
| BSB 13 But Jesus replied, “Every plant that My heavenly Father has not planted will be pulled up by its roots. | SWKCV 13 Akawajibu, “Kila pando ambalo Baba yangu wa mbinguni hakulipanda, litangʼolewa. |
| BSB 14 Disregard them! They are blind guides. If a blind man leads a blind man, both will fall into a pit.” | SWKCV 14 Waacheni; wao ni viongozi vipofu, wanaoongoza vipofu. Kama kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, wote wawili watatumbukia shimoni.” |
| BSB 15 Peter said to Him, “Explain this parable to us.” | SWKCV 15 Petro akasema, “Tueleze maana ya huu mfano.” |
| BSB 16 “Do you still not understand?” Jesus asked. | SWKCV 16 Yesu akawauliza, “Je, bado ninyi hamfahamu? |
| BSB 17 “Do you not yet realize that whatever enters the mouth goes into the stomach and then is eliminated? | SWKCV 17 Je, hamwelewi kwamba chochote kiingiacho kinywani huenda tumboni, na hatimaye hutolewa nje kikiwa uchafu? |
| BSB 18 But the things that come out of the mouth come from the heart, and these things defile a man. | SWKCV 18 Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi. |
| BSB 19 For out of the heart come evil thoughts, murder, adultery, sexual immorality, theft, false testimony, and slander. | SWKCV 19 Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio. |
| BSB 20 These are what defile a man, but eating with unwashed hands does not defile him.” | SWKCV 20 Haya ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula bila kunawa mikono hakumtii mtu unajisi.” |
| BSB 21 Leaving that place, Jesus withdrew to the district of Tyre and Sidon. | SWKCV 21 Yesu aliondoka mahali pale, akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. |
| BSB 22 And a Canaanite woman from that region came to Him, crying out, “Lord, Son of David, have mercy on me! My daughter is miserably possessed by a demon.” | SWKCV 22 Mwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu jirani na hizo akaja kwake akilia, akasema, “Nihurumie, Ee Bwana, Mwana wa Daudi! Binti yangu amepagawa na pepo mchafu, na anateseka sana.” |
| BSB 23 But Jesus did not answer a word. So His disciples came and urged Him, “Send her away, for she keeps crying out after us.” | SWKCV 23 Lakini Yesu hakumjibu neno. Hivyo wanafunzi wake wakamwendea na kumsihi sana, wakisema, “Mwambie aende zake, kwa maana anaendelea kutupigia kelele.” |
| BSB 24 He answered, “I was sent only to the lost sheep of the house of Israel.” | SWKCV 24 Yesu akajibu, “Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli waliopotea.” |
| BSB 25 The woman came and knelt before Him. “Lord, help me!” she said. | SWKCV 25 Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Yesu, akasema, “Bwana, nisaidie!” |
| BSB 26 But Jesus replied, “It is not right to take the children’s bread and toss it to the dogs.” | SWKCV 26 Yesu akajibu, “Si haki kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.” |
| BSB 27 “Yes, Lord,” she said, “even the dogs eat the crumbs that fall from their master’s table.” | SWKCV 27 Yule mwanamke akajibu, “Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka kwenye meza za bwana zao.” |
| BSB 28 “O woman,” Jesus answered, “your faith is great! Let it be done for you as you desire.” And her daughter was healed from that very hour. | SWKCV 28 Ndipo Yesu akamwambia, “Mwanamke, imani yako ni kubwa! Iwe kwako kama unavyotaka.” Naye binti yake akapona tangu saa ile. |
| BSB 29 Moving on from there, Jesus went along the Sea of Galilee. Then He went up on a mountain and sat down. | SWKCV 29 Yesu akaondoka na kwenda kando ya Bahari ya Galilaya. Kisha akapanda mlimani, akaketi huko. |
| BSB 30 Large crowds came to Him, bringing the lame, the blind, the crippled, the mute, and many others, and laid them at His feet, and He healed them. | SWKCV 30 Umati mkubwa wa watu ukamjia, wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; naye akawaponya. |
| BSB 31 The crowd was amazed when they saw the mute speaking, the crippled restored, the lame walking, and the blind seeing. And they glorified the God of Israel. | SWKCV 31 Hao watu wakashangaa walipoona bubu wakisema, vilema wakipona, viwete wakitembea na vipofu wakiona, wakamtukuza Mungu wa Israeli. |
| BSB 32 Then Jesus called His disciples to Him and said, “I have compassion for this crowd, because they have already been with Me three days and have nothing to eat. I do not want to send them away hungry, or they may faint along the way.” | SWKCV 32 Kisha Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Ninauhurumia huu umati wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa pamoja nami kwa muda wa siku tatu, na hawana chakula chochote. Nami sipendi kuwaaga wakiwa na njaa, wasije wakazimia njiani.” |
| BSB 33 The disciples replied, “Where in this desolate place could we find enough bread to feed such a large crowd?” | SWKCV 33 Wanafunzi wake wakasema, “Tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha umati huu wa watu mkubwa namna hii, nasi tuko nyikani?” |
| BSB 34 “How many loaves do you have?” Jesus asked. “Seven,” they replied, “and a few small fish.” | SWKCV 34 Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” Wakamjibu, “Tunayo mikate saba na visamaki vichache.” |
| BSB 35 And He instructed the crowd to sit down on the ground. | SWKCV 35 Yesu akawaambia ule umati wa watu waketi chini. |
| BSB 36 Taking the seven loaves and the fish, He gave thanks and broke them. Then He gave them to the disciples, and the disciples gave them to the people. | SWKCV 36 Kisha akachukua ile mikate saba na wale samaki, naye akiisha kumshukuru Mungu, akavimega na kuwapa wanafunzi wake, nao wakawapa ule umati wa watu. |
| BSB 37 They all ate and were satisfied, and the disciples picked up seven basketfuls of broken pieces that were left over. | SWKCV 37 Wote wakala na kushiba. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. |
| BSB 38 A total of four thousand men were fed, besides women and children. | SWKCV 38 Idadi ya watu walikuwa wanaume 4,000, bila kuhesabu wanawake na watoto. |
| BSB 39 After Jesus had dismissed the crowds, He got into the boat and went to the region of Magadan. | SWKCV 39 Baada ya kuaga ule umati wa watu, Yesu aliingia katika mashua, akaenda sehemu za Magadani. |
Questions about Matthew 15? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.