Numbers 10
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then the LORD said to Moses, | SWKCV 1 Bwana akamwambia Mose: |
| BSB 2 “Make two trumpets of hammered silver to be used for calling the congregation and for having the camps set out. | SWKCV 2 “Tengeneza tarumbeta mbili za fedha ya kufua, uzitumie kwa kuita jumuiya pamoja na wakati wa kuvunja makambi ili kuondoka. |
| BSB 3 When both are sounded, the whole congregation is to assemble before you at the entrance to the Tent of Meeting. | SWKCV 3 Tarumbeta zote mbili zikipigwa, jumuiya yote itakusanyika mbele yako katika ingilio la Hema la Kukutania. |
| BSB 4 But if only one is sounded, then the leaders, the heads of the clans of Israel, are to gather before you. | SWKCV 4 Kama tarumbeta moja tu ikipigwa, viongozi, yaani wakuu wa koo za Israeli, ndio watakaokusanyika mbele yako. |
| BSB 5 When you sound short blasts, the camps that lie on the east side are to set out. | SWKCV 5 Wakati mlio wa kujulisha hatari ukipigwa, makabila yaliyo na makambi upande wa mashariki yataondoka. |
| BSB 6 When you sound the short blasts a second time, the camps that lie on the south side are to set out. The blasts are to signal them to set out. | SWKCV 6 Ukisikika mlio wa pili wa jinsi hiyo, walioko kwenye makambi ya kusini wataondoka. Mlio huo wa kujulisha hatari utakuwa ishara ya kuondoka. |
| BSB 7 To convene the assembly, you are to sound long blasts, not short ones. | SWKCV 7 Ili kukusanya kusanyiko, piga tarumbeta zote, lakini siyo kwa mlio wa kujulisha hatari. |
| BSB 8 The sons of Aaron, the priests, are to sound the trumpets. This shall be a permanent statute for you and the generations to come. | SWKCV 8 “Wana wa Aroni, makuhani, ndio watakaopiga hizo tarumbeta. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu na kwa vizazi vijavyo. |
| BSB 9 When you enter into battle in your land against an adversary who attacks you, sound short blasts on the trumpets, and you will be remembered before the LORD your God and saved from your enemies. | SWKCV 9 Wakati mtakapopigana vita katika nchi yenu wenyewe dhidi ya adui anayewaonea, piga tarumbeta kwa mlio wa kujulisha hatari. Ndipo utakumbukwa na Bwana Mungu wenu na kuokolewa kutoka kwa adui zenu. |
| BSB 10 And on your joyous occasions, your appointed feasts, and the beginning of each month, you are to blow the trumpets over your burnt offerings and peace offerings to serve as a reminder for you before your God. I am the LORD your God.” | SWKCV 10 Pia nyakati za furaha yenu, yaani sikukuu zenu zilizoamriwa na sikukuu za Mwezi Mwandamo, mtapiga tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za amani, nazo zitakuwa ukumbusho kwa ajili yenu mbele za Mungu wenu. Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.” |
| BSB 11 On the twentieth day of the second month of the second year, the cloud was lifted from above the tabernacle of the Testimony, | SWKCV 11 Katika siku ya ishirini ya mwezi wa pili wa mwaka wa pili, wingu liliinuka kutoka juu ya maskani ya Ushuhuda. |
| BSB 12 and the Israelites set out from the Wilderness of Sinai, traveling from place to place until the cloud settled in the Wilderness of Paran. | SWKCV 12 Ndipo Waisraeli wakaondoka kutoka Jangwa la Sinai wakasafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine mpaka wingu lilipotua katika Jangwa la Parani. |
| BSB 13 They set out this first time according to the LORD’s command through Moses. | SWKCV 13 Waliondoka kwa mara ya kwanza kwa agizo la Bwana kupitia kwa Mose. |
| BSB 14 First, the divisions of the camp of Judah set out under their standard, with Nahshon son of Amminadab in command. | SWKCV 14 Vikosi vya kambi ya Yuda vilitangulia kwanza chini ya alama yao. Nashoni mwana wa Aminadabu alikuwa kiongozi wao. |
| BSB 15 Nethanel son of Zuar was over the division of the tribe of Issachar, | SWKCV 15 Nethaneli mwana wa Suari alikuwa kiongozi wa kabila la Isakari, |
| BSB 16 and Eliab son of Helon was over the division of the tribe of Zebulun. | SWKCV 16 naye Eliabu mwana wa Heloni alikuwa kiongozi wa kabila la Zabuloni. |
| BSB 17 Then the tabernacle was taken down, and the Gershonites and the Merarites set out, transporting it. | SWKCV 17 Ndipo Maskani iliposhushwa, nao wana wa Gershoni na wana wa Merari ambao waliibeba wakaondoka. |
| BSB 18 Then the divisions of the camp of Reuben set out under their standard, with Elizur son of Shedeur in command. | SWKCV 18 Vikosi vya kambi ya Reubeni vilifuata, chini ya alama yao. Elisuri mwana wa Shedeuri alikuwa kiongozi wao. |
| BSB 19 Shelumiel son of Zurishaddai was over the division of the tribe of Simeon, | SWKCV 19 Shelumieli mwana wa Surishadai aliongoza kikosi cha kabila la Simeoni, |
| BSB 20 and Eliasaph son of Deuel was over the division of the tribe of Gad. | SWKCV 20 naye Eliasafu mwana wa Deueli aliongoza kikosi cha kabila la Gadi. |
| BSB 21 Then the Kohathites set out, transporting the holy objects; the tabernacle was to be set up before their arrival. | SWKCV 21 Kisha Wakohathi wakaondoka, wakichukua vitu vitakatifu. Maskani ilikuwa isimamishwe kabla wao hawajafika. |
| BSB 22 Next, the divisions of the camp of Ephraim set out under their standard, with Elishama son of Ammihud in command. | SWKCV 22 Vikosi vya kambi ya Efraimu vilifuata, chini ya alama yao. Elishama mwana wa Amihudi alikuwa kiongozi wao. |
| BSB 23 Gamaliel son of Pedahzur was over the division of the tribe of Manasseh, | SWKCV 23 Gamalieli mwana wa Pedasuri aliongoza kikosi cha kabila la Manase, |
| BSB 24 and Abidan son of Gideoni was over the division of the tribe of Benjamin. | SWKCV 24 naye Abidani mwana wa Gideoni alikuwa kiongozi wa kikosi cha kabila la Benyamini. |
| BSB 25 Finally, the divisions of the camp of Dan set out under their standard, serving as the rear guard for all units, with Ahiezer son of Ammishaddai in command. | SWKCV 25 Mwishowe, kama kikosi cha nyuma cha ulinzi wa vikosi vyote, vikosi vya kambi ya Dani viliondoka chini ya alama yao. Ahiezeri mwana wa Amishadai alikuwa kiongozi wao. |
| BSB 26 Pagiel son of Ocran was over the division of the tribe of Asher, | SWKCV 26 Pagieli mwana wa Okrani aliongoza kikosi cha kabila la Asheri, |
| BSB 27 and Ahira son of Enan was over the division of the tribe of Naphtali. | SWKCV 27 naye Ahira mwana wa Enani aliongoza kikosi cha kabila la Naftali. |
| BSB 28 This was the order of march for the Israelite divisions as they set out. | SWKCV 28 Huu ndio ulikuwa utaratibu wa kuondoka wa vikosi vya Waisraeli walipokuwa wanaondoka. |
| BSB 29 Then Moses said to Hobab, the son of Moses’ father-in-law Reuel the Midianite, “We are setting out for the place of which the LORD said: ‘I will give it to you.’ Come with us, and we will treat you well, for the LORD has promised good things to Israel.” | SWKCV 29 Basi Mose akamwambia Hobabu mwana wa Reueli, Mmidiani, mkwewe Mose, “Tunaondoka kwenda mahali ambapo Bwana amesema ‘Nitawapa ninyi mahali hapo.’ Twende pamoja nasi tutakutendea mema, kwa maana Bwana ameahidi mambo mema kwa Israeli.” |
| BSB 30 “I will not go,” Hobab replied. “Instead, I am going back to my own land and my own people.” | SWKCV 30 Akajibu, “Hapana, sitakwenda; nitarudi kwenye nchi yangu mwenyewe na watu wangu mwenyewe.” |
| BSB 31 “Please do not leave us,” Moses said, “since you know where we should camp in the wilderness, and you can serve as our eyes. | SWKCV 31 Lakini Mose akasema, “Tafadhali usituache. Wewe unajua mahali ambapo yatupasa kupiga kambi jangwani, nawe unaweza kuwa macho yetu. |
| BSB 32 If you come with us, we will share with you whatever good things the LORD gives us.” | SWKCV 32 Ikiwa utafuatana nasi, tutashirikiana nawe mema yoyote tutakayopewa na Bwana.” |
| BSB 33 So they set out on a three-day journey from the mountain of the LORD, with the ark of the covenant of the LORD traveling ahead of them for those three days to seek a resting place for them. | SWKCV 33 Hivyo waliondoka kutoka mlima wa Bwana, nao wakasafiri kwa siku tatu. Sanduku la Agano la Bwana liliwatangulia kwa zile siku tatu ili kuwatafutia mahali pa kupumzika. |
| BSB 34 And the cloud of the LORD was over them by day when they set out from the camp. | SWKCV 34 Wingu la Bwana lilikuwa juu yao wakati wa mchana walipoondoka kambini. |
| BSB 35 Whenever the ark set out, Moses would say, “Rise up, O LORD! May Your enemies be scattered; may those who hate You flee before You.” | SWKCV 35 Wakati wowote Sanduku lilipoondoka, Mose alisema, “Ee Bwana, inuka! Watesi wako na watawanyike; adui zako na wakimbie mbele zako.” |
| BSB 36 And when it came to rest, he would say: “Return, O LORD, to the countless thousands of Israel.” | SWKCV 36 Wakati wowote Sanduku liliposimama, alisema, “Ee Bwana, rudi, kwa maelfu ya Waisraeli wasiohesabika.” |
Questions about Numbers 10? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.