Numbers 29
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “On the first day of the seventh month, you are to hold a sacred assembly, and you must not do any regular work. This will be a day for you to sound the trumpets. | SWKCV 1 “ ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu na msifanye kazi ya kawaida. Ni siku kwa ajili yenu ya kupiga tarumbeta. |
| BSB 2 As a pleasing aroma to the LORD, you are to present a burnt offering of one young bull, one ram, and seven male lambs a year old, all unblemished, | SWKCV 2 Mtatayarisha sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri impendezayo Bwana ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. |
| BSB 3 together with their grain offerings of fine flour mixed with oil—three-tenths of an ephah with the bull, two-tenths of an ephah with the ram, | SWKCV 3 Pamoja na fahali, andaeni sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume, andaa unga sehemu ya kumi mbili za efa; |
| BSB 4 and a tenth of an ephah with each of the seven male lambs. | SWKCV 4 na pamoja na wana-kondoo saba kila mmoja aandaliwe na sehemu ya kumi ya efa ya unga. |
| BSB 5 Include one male goat as a sin offering to make atonement for you. | SWKCV 5 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi kufanya upatanisho kwa ajili yenu. |
| BSB 6 These are in addition to the monthly and daily burnt offerings with their prescribed grain offerings and drink offerings. They are a pleasing aroma, a food offering to the LORD. | SWKCV 6 Hivi ni nyongeza ya sadaka za kuteketezwa kila mwezi na kila siku pamoja na sadaka zake za nafaka na sadaka za vinywaji kama ilivyoainishwa. Ni sadaka zinazotolewa kwa Bwana kwa moto, harufu inayopendeza. |
| BSB 7 On the tenth day of this seventh month, you are to hold a sacred assembly, and you shall humble yourselves; you must not do any work. | SWKCV 7 “ ‘Kwenye siku ya kumi ya mwezi huu wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu. Mtajikana wenyewe na msifanye kazi. |
| BSB 8 Present as a pleasing aroma to the LORD a burnt offering of one young bull, one ram, and seven male lambs a year old, all unblemished, | SWKCV 8 Toeni sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza Bwana. |
| BSB 9 together with their grain offerings of fine flour mixed with oil—three-tenths of an ephah with the bull, two-tenths of an ephah with the ram, | SWKCV 9 Pamoja na fahali, andaeni sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini; |
| BSB 10 and a tenth of an ephah with each of the seven lambs. | SWKCV 10 na kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba andaa sehemu ya kumi ya unga laini kwa kila mmoja. |
| BSB 11 Include one male goat for a sin offering, in addition to the sin offering of atonement and the regular burnt offering with its grain offering and drink offerings. | SWKCV 11 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho, na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, na sadaka zake za vinywaji. |
| BSB 12 On the fifteenth day of the seventh month, you are to hold a sacred assembly; you must not do any regular work, and you shall observe a feast to the LORD for seven days. | SWKCV 12 “ ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu, na hamtafanya kazi za kawaida. Adhimisheni sikukuu kwa Bwana kwa siku saba. |
| BSB 13 As a pleasing aroma to the LORD, you are to present a food offering, a burnt offering of thirteen young bulls, two rams, and fourteen male lambs a year old, all unblemished, | SWKCV 13 Toeni sadaka ya kuteketezwa mafahali wachanga kumi na watatu, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza Bwana. |
| BSB 14 along with the grain offering of three-tenths of an ephah of fine flour mixed with oil with each of the thirteen bulls, two-tenths of an ephah with each of the two rams, | SWKCV 14 Pamoja na hao mafahali kumi na watatu, kila mmoja aandaliwe na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume wawili, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini; |
| BSB 15 and a tenth of an ephah with each of the fourteen lambs. | SWKCV 15 na kwa wana-kondoo kumi na wanne, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi ya efa ya unga laini. |
| BSB 16 Include one male goat as a sin offering, in addition to the regular burnt offering with its grain offering and drink offering. | SWKCV 16 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka ya vinywaji. |
| BSB 17 On the second day you are to present twelve young bulls, two rams, and fourteen male lambs a year old, all unblemished, | SWKCV 17 “ ‘Katika siku ya pili andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. |
| BSB 18 along with the grain and drink offerings for the bulls, rams, and lambs, according to the number prescribed. | SWKCV 18 Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. |
| BSB 19 Include one male goat as a sin offering, in addition to the regular burnt offering with its grain offering and drink offering. | SWKCV 19 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji. |
| BSB 20 On the third day you are to present eleven bulls, two rams, and fourteen male lambs a year old, all unblemished, | SWKCV 20 “ ‘Katika siku ya tatu andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. |
| BSB 21 along with the grain and drink offerings for the bulls, rams, and lambs, according to the number prescribed. | SWKCV 21 Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. |
| BSB 22 Include one male goat as a sin offering, in addition to the regular burnt offering with its grain offering and drink offering. | SWKCV 22 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji. |
| BSB 23 On the fourth day you are to present ten bulls, two rams, and fourteen male lambs a year old, all unblemished, | SWKCV 23 “ ‘Katika siku ya nne andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. |
| BSB 24 along with the grain and drink offerings for the bulls, rams, and lambs, according to the number prescribed. | SWKCV 24 Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. |
| BSB 25 Include one male goat as a sin offering, in addition to the regular burnt offering with its grain offering and drink offering. | SWKCV 25 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji. |
| BSB 26 On the fifth day you are to present nine bulls, two rams, and fourteen male lambs a year old, all unblemished, | SWKCV 26 “ ‘Katika siku ya tano andaeni mafahali tisa, kondoo dume wawili na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. |
| BSB 27 along with the grain and drink offerings for the bulls, rams, and lambs, according to the number prescribed. | SWKCV 27 Pamoja na mafahali, kondoo dume na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za kinywaji kulingana na idadi iliyoainishwa. |
| BSB 28 Include one male goat as a sin offering, in addition to the regular burnt offering with its grain offering and drink offering. | SWKCV 28 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi katika nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka pamoja na sadaka ya kinywaji. |
| BSB 29 On the sixth day you are to present eight bulls, two rams, and fourteen male lambs a year old, all unblemished, | SWKCV 29 “ ‘Katika siku ya sita andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. |
| BSB 30 along with the grain and drink offerings for the bulls, rams, and lambs, according to the number prescribed. | SWKCV 30 Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. |
| BSB 31 Include one male goat as a sin offering, in addition to the regular burnt offering with its grain offering and drink offering. | SWKCV 31 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji. |
| BSB 32 On the seventh day you are to present seven bulls, two rams, and fourteen male lambs a year old, all unblemished, | SWKCV 32 “ ‘Katika siku ya saba andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. |
| BSB 33 along with the grain and drink offerings for the bulls, rams, and lambs, according to the number prescribed. | SWKCV 33 Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. |
| BSB 34 Include one male goat as a sin offering, in addition to the regular burnt offering with its grain offering and drink offering. | SWKCV 34 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji. |
| BSB 35 On the eighth day you are to hold a solemn assembly; you must not do any regular work. | SWKCV 35 “ ‘Katika siku ya nane mtakuwa na kusanyiko, na msifanye kazi ya kawaida. |
| BSB 36 As a pleasing aroma to the LORD, you are to present a food offering, a burnt offering of one bull, one ram, and seven male lambs a year old, all unblemished, | SWKCV 36 Toeni sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri inayompendeza Bwana, sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. |
| BSB 37 along with the grain and drink offerings for the bulls, rams, and lambs, according to the number prescribed. | SWKCV 37 Pamoja na fahali, kondoo dume na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka, na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. |
| BSB 38 Include one male goat as a sin offering, in addition to the regular burnt offering with its grain offering and drink offering. | SWKCV 38 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka pamoja na sadaka ya kinywaji. |
| BSB 39 You are to present these offerings to the LORD at your appointed times, in addition to your vow and freewill offerings, whether burnt offerings, grain offerings, drink offerings, or peace offerings.” | SWKCV 39 “ ‘Zaidi ya kile unachoweka nadhiri na sadaka zenu za hiari, andaeni hizi kwa ajili ya Bwana kwenye sikukuu zenu zilizoamriwa: sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za nafaka, sadaka za vinywaji, pamoja na sadaka zenu za amani.’” |
| BSB 40 So Moses spoke all this to the Israelites just as the LORD had commanded him. | SWKCV 40 Mose akawaambia Waisraeli yale yote Bwana alimwagiza. |
Questions about Numbers 29? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.