Numbers 28
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then the LORD said to Moses, | SWKCV 1 Bwana akamwambia Mose, |
| BSB 2 “Command the Israelites and say to them: See that you present to Me at its appointed time the food for My food offerings, as a pleasing aroma to Me. | SWKCV 2 “Wape Waisraeli agizo hili na uwaambie: ‘Hakikisheni kwamba mnaniletea mimi kwa wakati uliowekwa chakula kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, kama harufu nzuri ya kupendeza.’ |
| BSB 3 And tell them that this is the food offering you are to present to the LORD as a regular burnt offering each day: two unblemished year-old male lambs. | SWKCV 3 Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtolea Bwana: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku. |
| BSB 4 Offer one lamb in the morning and the other at twilight, | SWKCV 4 Andaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni, |
| BSB 5 along with a tenth of an ephah of fine flour as a grain offering, mixed with a quarter hin of oil from pressed olives. | SWKCV 5 kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini ya mafuta ya zeituni. |
| BSB 6 This is a regular burnt offering established at Mount Sinai as a pleasing aroma, a food offering to the LORD. | SWKCV 6 Hii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. |
| BSB 7 The drink offering accompanying each lamb shall be a quarter hin. Pour out the offering of fermented drink to the LORD in the sanctuary area. | SWKCV 7 Sadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwa Bwana mahali patakatifu. |
| BSB 8 And offer the second lamb at twilight, with the same grain offering and drink offering as in the morning. It is a food offering, a pleasing aroma to the LORD. | SWKCV 8 Andaa yule mwana-kondoo wa pili jioni, pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kama ulivyofanya kwa ile sadaka nyingine ya asubuhi. Hii ni sadaka iliyotolewa kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. |
| BSB 9 On the Sabbath day, present two unblemished year-old male lambs, accompanied by a grain offering of two-tenths of an ephah of fine flour mixed with oil, as well as a drink offering. | SWKCV 9 “ ‘Siku ya Sabato, utatoa sadaka ya wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari pamoja na sadaka yake ya kinywaji na sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta. |
| BSB 10 This is the burnt offering for every Sabbath, in addition to the regular burnt offering and its drink offering. | SWKCV 10 Hii ni sadaka ya kuteketezwa itakayotolewa kwa ajili ya kila Sabato, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya kinywaji. |
| BSB 11 At the beginning of every month, you are to present to the LORD a burnt offering of two young bulls, one ram, and seven male lambs a year old, all unblemished, | SWKCV 11 “ ‘Siku ya kwanza ya kila mwezi, mtamletea Bwana sadaka ya kuteketezwa ya fahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasiokuwa na dosari. |
| BSB 12 along with three-tenths of an ephah of fine flour mixed with oil as a grain offering with each bull, two-tenths of an ephah of fine flour mixed with oil as a grain offering with the ram, | SWKCV 12 Pamoja na kila fahali, kutakuwa na sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa, uliochanganywa na mafuta, pamoja na kondoo dume mmoja, sadaka ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta; |
| BSB 13 and a tenth of an ephah of fine flour mixed with oil as a grain offering with each lamb. This is a burnt offering, a pleasing aroma, a food offering to the LORD. | SWKCV 13 pamoja na kila mwana-kondoo, sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta. Hii ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri, sadaka ya kuteketezwa iliyotolewa kwa moto kwa Bwana. |
| BSB 14 Their drink offerings shall be half a hin of wine with each bull, a third of a hin with the ram, and a quarter hin with each lamb. This is the monthly burnt offering to be made at each new moon throughout the year. | SWKCV 14 Pamoja na kila fahali kutakuwa na sadaka ya kinywaji nusu ya hini ya divai; pamoja na kila kondoo dume, theluthi moja ya hini, na pamoja na kila mwana-kondoo robo hini. Hii ni sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi itakayotolewa kila mwandamo wa mwezi kwa mwaka. |
| BSB 15 In addition to the regular burnt offering with its drink offering, one male goat is to be presented to the LORD as a sin offering. | SWKCV 15 Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwa Bwana kama sadaka ya dhambi. |
| BSB 16 The fourteenth day of the first month is the LORD’s Passover. | SWKCV 16 “ ‘Katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, itafanyika Pasaka ya Bwana. |
| BSB 17 On the fifteenth day of this month, there shall be a feast; for seven days unleavened bread is to be eaten. | SWKCV 17 Katika siku ya kumi na tano ya mwezi huo itakuwa sikukuu; kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu. |
| BSB 18 On the first day there is to be a sacred assembly; you must not do any regular work. | SWKCV 18 Katika siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu, msifanye kazi za kawaida. |
| BSB 19 Present to the LORD a food offering, a burnt offering of two young bulls, one ram, and seven male lambs a year old, all unblemished. | SWKCV 19 Leteni mbele za Bwana sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo dume saba wenye umri wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. |
| BSB 20 The grain offering shall consist of fine flour mixed with oil; offer three-tenths of an ephah with each bull, two-tenths of an ephah with the ram, | SWKCV 20 Pamoja na kila fahali, andaa sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa; |
| BSB 21 and a tenth of an ephah with each of the seven lambs. | SWKCV 21 pia pamoja na kila mmoja wa wale wana-kondoo saba, andaa sehemu ya kumi ya efa. |
| BSB 22 Include one male goat as a sin offering to make atonement for you. | SWKCV 22 Pia mtoe beberu mmoja kama sadaka ya dhambi ambaye atafanya upatanisho kwa ajili yenu. |
| BSB 23 You are to present these in addition to the regular morning burnt offering. | SWKCV 23 Andaa hizi licha ya zile sadaka za kawaida za kuteketezwa za kila asubuhi. |
| BSB 24 Offer the same food each day for seven days as a food offering, a pleasing aroma to the LORD. It is to be offered with its drink offering and the regular burnt offering. | SWKCV 24 Kwa njia hii andaa chakula cha sadaka ya kuteketezwa kila siku, kwa siku saba kama harufu nzuri impendezayo Bwana. Hii itaandaliwa licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa ya kila siku pamoja na sadaka yake ya kinywaji. |
| BSB 25 On the seventh day you shall hold a sacred assembly; you must not do any regular work. | SWKCV 25 Siku ya saba mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida. |
| BSB 26 On the day of firstfruits, when you present an offering of new grain to the LORD during the Feast of Weeks, you are to hold a sacred assembly; you must not do any regular work. | SWKCV 26 “ ‘Siku ya malimbuko, mnapomletea Bwana sadaka ya nafaka mpya wakati wa Sikukuu ya Majuma, mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida. |
| BSB 27 Present a burnt offering of two young bulls, one ram, and seven male lambs a year old as a pleasing aroma to the LORD, | SWKCV 27 Mlete sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na pia wana-kondoo saba wenye umri wa mwaka mmoja, kama harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. |
| BSB 28 together with their grain offerings of fine flour mixed with oil—three-tenths of an ephah with each bull, two-tenths of an ephah with the ram, | SWKCV 28 Pamoja na kila fahali itatolewa sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini; |
| BSB 29 and a tenth of an ephah with each of the seven lambs. | SWKCV 29 na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba. |
| BSB 30 Include one male goat to make atonement for you. | SWKCV 30 Ongeza beberu mmoja kwa kufanya upatanisho kwa ajili yenu. |
| BSB 31 Offer them with their drink offerings in addition to the regular burnt offering and its grain offering. The animals must be unblemished. | SWKCV 31 Andaa hizi sadaka pamoja na sadaka zake za vinywaji, kuwa nyongeza ya sadaka za kawaida za kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka. Hakikisha kuwa wanyama hao hawana dosari. |
Questions about Numbers 28? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.