Numbers 31
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 And the LORD said to Moses, | SWKCV 1 Bwana akamwambia Mose, |
| BSB 2 “Take vengeance on the Midianites for the Israelites. After that, you will be gathered to your people.” | SWKCV 2 “Uwalipize kisasi Wamidiani kwa ajili ya Waisraeli. Halafu baada ya hayo, utakufa.” |
| BSB 3 So Moses told the people, “Arm some of your men for war, that they may go against the Midianites and execute the LORD’s vengeance on them. | SWKCV 3 Kwa hiyo Mose akawaambia watu, “Waandaeni baadhi ya wanaume wenu waende vitani kupigana na Wamidiani ili wawalipize kisasi cha Bwana. |
| BSB 4 Send into battle a thousand men from each tribe of Israel.” | SWKCV 4 Peleka wanaume 1,000 vitani kutoka kila kabila la Israeli.” |
| BSB 5 So a thousand men were recruited from each tribe of Israel—twelve thousand armed for war. | SWKCV 5 Kwa hiyo waliandaliwa wanaume 12,000 kwa vita, wanaume 1,000 kutoka kila kabila, walitolewa kutoka koo za Israeli. |
| BSB 6 And Moses sent the thousand from each tribe into battle, along with Phinehas son of Eleazar the priest, who took with him the vessels of the sanctuary and the trumpets for signaling. | SWKCV 6 Mose aliwatuma vitani, watu 1,000 kutoka kila kabila, pamoja na Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, ambaye alichukua vyombo vya mahali patakatifu na tarumbeta za kuashiria. |
| BSB 7 Then they waged war against Midian, as the LORD had commanded Moses, and they killed every male. | SWKCV 7 Walipigana dhidi ya Wamidiani, kama Bwana alivyomwagiza Mose, nao waliua kila mwanaume. |
| BSB 8 Among the slain were Evi, Rekem, Zur, Hur, and Reba—the five kings of Midian. They also killed Balaam son of Beor with the sword. | SWKCV 8 Miongoni mwa watu waliouawa walikuwepo wafalme watano wa Midiani, nao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba. Vilevile walimuua Balaamu mwana wa Beori kwa upanga. |
| BSB 9 The Israelites captured the Midianite women and their children, and they plundered all their herds, flocks, and goods. | SWKCV 9 Waisraeli waliwateka wanawake wa Kimidiani pamoja na watoto wao na walichukua makundi ya ngʼombe, kondoo na mali zao kama nyara. |
| BSB 10 Then they burned all the cities where the Midianites had lived, as well as all their encampments, | SWKCV 10 Walichoma moto miji yote ambayo Wamidiani walikuwa wanaishi, pamoja na kambi zao zote. |
| BSB 11 and carried away all the plunder and spoils, both people and animals. | SWKCV 11 Walichukua nyara zote na mateka, pamoja na watu na wanyama, |
| BSB 12 They brought the captives, spoils, and plunder to Moses, to Eleazar the priest, and to the congregation of Israel at the camp on the plains of Moab, by the Jordan across from Jericho. | SWKCV 12 nao waliwaleta wafungwa mateka na nyara kwa Mose na kwa kuhani Eleazari, nao Waisraeli walikusanyika kwenye kambi zao katika tambarare za nchi ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko. |
| BSB 13 And Moses, Eleazar the priest, and all the leaders of the congregation went to meet them outside the camp. | SWKCV 13 Mose, kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya wakatoka kuwalaki nje ya kambi. |
| BSB 14 But Moses was angry with the officers of the army—the commanders of thousands and commanders of hundreds—who were returning from the battle. | SWKCV 14 Mose aliwakasirikia maafisa wa jeshi, yaani hao wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, ambao walirudi kutoka vitani. |
| BSB 15 “Have you spared all the women?” he asked them. | SWKCV 15 Mose akawauliza, “Je, mmewaacha wanawake wote hai?” |
| BSB 16 “Look, these women caused the sons of Israel, through the counsel of Balaam, to turn unfaithfully against the LORD at Peor, so that the plague struck the congregation of the LORD. | SWKCV 16 “Wanawake hao ndio waliofuata ushauri wa Balaamu, nao ndio waliowasababisha Waisraeli wamwasi Bwana kwa kile kilichotokea kule Peori, na kwa hiyo pigo liliwapata watu wa Bwana. |
| BSB 17 So now, kill all the boys, as well as every woman who has had relations with a man, | SWKCV 17 Sasa waue wavulana wote. Pia muue kila mwanamke ambaye alikwisha fanya tendo la ndoa, |
| BSB 18 but spare for yourselves every girl who has never had relations with a man. | SWKCV 18 lakini mwacheni hai kwa ajili yenu kila msichana ambaye kamwe hajawahi kuzini na mwanaume. |
| BSB 19 All of you who have killed a person or touched the dead are to remain outside the camp for seven days. On the third day and the seventh day you are to purify both yourselves and your captives. | SWKCV 19 “Ninyi nyote ambao mmeua mtu yeyote au kumgusa mtu yeyote ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu. |
| BSB 20 And purify every garment and leather good, everything made of goat’s hair, and every article of wood.” | SWKCV 20 Takaseni kila vazi pamoja na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi, kwa singa za mbuzi au kwa mti.” |
| BSB 21 Then Eleazar the priest said to the soldiers who had gone into battle, “This is the statute of the law which the LORD has commanded Moses: | SWKCV 21 Kisha kuhani Eleazari aliwaambia askari waliokuwa wamekwenda vitani, “Haya ndiyo matakwa ya sheria ambayo Bwana alimpa Mose: |
| BSB 22 Only the gold, silver, bronze, iron, tin, and lead— | SWKCV 22 Dhahabu, fedha, shaba, chuma, bati, risasi, |
| BSB 23 everything that can withstand the fire—must be put through the fire, and it will be clean. But it must still be purified with the water of purification. And everything that cannot withstand the fire must pass through the water. | SWKCV 23 na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu chochote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso. |
| BSB 24 On the seventh day you are to wash your clothes, and you will be clean. After that you may enter the camp.” | SWKCV 24 Katika siku ya saba fueni nguo zenu, nanyi mtakuwa safi. Kisha mtaweza kuingia kambini.” |
| BSB 25 The LORD said to Moses, | SWKCV 25 Bwana akamwambia Mose, |
| BSB 26 “You and Eleazar the priest and the family heads of the congregation are to take a count of what was captured, both of man and beast. | SWKCV 26 “Wewe na kuhani Eleazari pamoja na viongozi wa jamaa ya jumuiya mtahesabu watu wote na wanyama ambao walitekwa. |
| BSB 27 Then divide the captives between the troops who went out to battle and the rest of the congregation. | SWKCV 27 Gawanyeni hizo nyara kati ya askari ambao walishiriki katika vita na kwa jumuiya. |
| BSB 28 Set aside a tribute for the LORD from what belongs to the soldiers who went into battle: one out of every five hundred, whether persons, cattle, donkeys, or sheep. | SWKCV 28 Kutoka fungu la wale waliokwenda kupigana vitani, tenga kama ushuru kwa ajili ya Bwana kitu kimoja kati ya kila mia tano, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo au mbuzi. |
| BSB 29 Take it from their half and give it to Eleazar the priest as an offering to the LORD. | SWKCV 29 Chukua ushuru huu kutoka fungu lao, umpe kuhani Eleazari kama sehemu ya Bwana. |
| BSB 30 From the Israelites’ half, take one out of every fifty, whether persons, cattle, donkeys, sheep, or other animals, and give them to the Levites who keep charge of the tabernacle of the LORD.” | SWKCV 30 Kutoka fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani ya Bwana.” |
| BSB 31 So Moses and Eleazar the priest did as the LORD had commanded Moses, | SWKCV 31 Kwa hiyo Mose na kuhani Eleazari wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Mose. |
| BSB 32 and this plunder remained from the spoils the soldiers had taken: 675,000 sheep, | SWKCV 32 Nyara zilizobaki kutoka mateka ambayo askari walichukua ni kondoo 675,000, |
| BSB 33 72,000 cattle, | SWKCV 33 ngʼombe 72,000, |
| BSB 34 61,000 donkeys, | SWKCV 34 punda 61,000, |
| BSB 35 and 32,000 women who had not slept with a man. | SWKCV 35 na wanawake 32,000 ambao hawakumjua mume kwa kufanya tendo la ndoa. |
| BSB 36 This was the half portion for those who had gone to war: 337,500 sheep, | SWKCV 36 Nusu ya fungu la wale waliokwenda kupigana vitani lilikuwa: Kondoo 337,500 |
| BSB 37 including a tribute to the LORD of 675, | SWKCV 37 ambayo ushuru kwa ajili ya Bwana ilikuwa kondoo 675; |
| BSB 38 36,000 cattle, including a tribute to the LORD of 72, | SWKCV 38 ngʼombe 36,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa ngʼombe 72; |
| BSB 39 30,500 donkeys, including a tribute to the LORD of 61, | SWKCV 39 punda 30,500 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa punda 61; |
| BSB 40 and 16,000 people, including a tribute to the LORD of 32. | SWKCV 40 Watu 16,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa watu 32. |
| BSB 41 Moses gave the tribute to Eleazar the priest as an offering for the LORD, as the LORD had commanded Moses. | SWKCV 41 Mose alimpa kuhani Eleazari ushuru kama sehemu ya Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Mose. |
| BSB 42 From the Israelites’ half, which Moses had set apart from the men who had gone to war, | SWKCV 42 Ile nusu iliyokuwa ya Waisraeli, ambayo Mose aliitenga kutoka kwa ile ya watu waliokwenda vitani, |
| BSB 43 this half belonged to the congregation: 337,500 sheep, | SWKCV 43 nusu iliyokuwa ya jumuiya, ilikuwa kondoo 337,500, |
| BSB 44 36,000 cattle, | SWKCV 44 ngʼombe 36,000, |
| BSB 45 30,500 donkeys, | SWKCV 45 punda 30,500, |
| BSB 46 and 16,000 people. | SWKCV 46 na wanadamu 16,000. |
| BSB 47 From the Israelites’ half, Moses took one out of every fifty persons and animals and gave them to the Levites who kept charge of the tabernacle of the LORD, as the LORD had commanded him. | SWKCV 47 Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Mose alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama Bwana alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya Bwana. |
| BSB 48 Then the officers who were over the units of the army—the commanders of thousands and of hundreds—approached Moses | SWKCV 48 Kisha maafisa waliokuwa juu ya vikosi vya jeshi, wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, walimwendea Mose |
| BSB 49 and said, “Your servants have counted the soldiers under our command, and not one of us is missing. | SWKCV 49 na kumwambia, “Watumishi wako wamehesabu askari walio chini ya amri yetu na hakuna hata mmoja aliyekosekana. |
| BSB 50 So we have brought to the LORD an offering of the gold articles each man acquired—armlets, bracelets, rings, earrings, and necklaces—to make atonement for ourselves before the LORD.” | SWKCV 50 Kwa hiyo tumeleta kama sadaka kwa Bwana vyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele za Bwana.” |
| BSB 51 So Moses and Eleazar the priest received from them all the articles made out of gold. | SWKCV 51 Mose na kuhani Eleazari wakapokea kutoka kwao dhahabu, yaani vyombo vyote vilivyonakshiwa. |
| BSB 52 All the gold that the commanders of thousands and of hundreds presented as an offering to the LORD weighed 16,750 shekels. | SWKCV 52 Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Mose na kuhani Eleazari walimletea Bwana kama zawadi ilikuwa shekeli 16,750 |
| BSB 53 Each of the soldiers had taken plunder for himself. | SWKCV 53 Kila askari alikuwa amejichukulia nyara zake binafsi. |
| BSB 54 And Moses and Eleazar the priest received the gold from the commanders of thousands and of hundreds and brought it into the Tent of Meeting as a memorial for the Israelites before the LORD. | SWKCV 54 Mose na kuhani Eleazari walipokea dhahabu kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, wakazileta katika Hema la Kukutania kama ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Bwana. |
Questions about Numbers 31? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.