Psalms 59
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 For the choirmaster. To the tune of “Do Not Destroy.” A Miktam of David, when Saul sent men to watch David’s house in order to kill him. Deliver me from my enemies, O my God; protect me from those who rise against me. | SWKCV 1 Ee Mungu, uniokoe na adui zangu, unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu. |
| BSB 2 Deliver me from workers of iniquity, and save me from men of bloodshed. | SWKCV 2 Uniponye na watu watendao mabaya, uniokoe kutokana na wamwagao damu. |
| BSB 3 See how they lie in wait for me. Fierce men conspire against me for no transgression or sin of my own, O LORD. | SWKCV 3 Tazama wanavyonivizia! Watu wakali wananifanyia hila, ingawa Ee Bwana, mimi sijakosea wala kutenda dhambi. |
| BSB 4 For no fault of my own, they move swiftly to attack me. Arise to help me, and take notice. | SWKCV 4 Sijatenda kosa; hata hivyo wako tayari kunishambulia. Inuka unisaidie, uone hali yangu mbaya! |
| BSB 5 O LORD God of Hosts, the God of Israel, rouse Yourself to punish all the nations; show no mercy to the wicked traitors. Selah | SWKCV 5 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli! Zinduka uyaadhibu mataifa yote, usionyeshe huruma kwa wasaliti. |
| BSB 6 They return in the evening, snarling like dogs and prowling around the city. | SWKCV 6 Hurudi wakati wa jioni, wakibweka kama mbwa, wakiuzurura mji. |
| BSB 7 See what they spew from their mouths—sharp words from their lips: “For who can hear us?” | SWKCV 7 Tazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao, hutema upanga kutoka midomo yao, nao husema, “Ni nani atakayetusikia?” |
| BSB 8 But You, O LORD, laugh at them; You scoff at all the nations. | SWKCV 8 Lakini wewe, Bwana, uwacheke; unayadharau mataifa hayo yote. |
| BSB 9 I will keep watch for You, O my strength, because You, O God, are my fortress. | SWKCV 9 Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe, wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, |
| BSB 10 My God of loving devotion will come to meet me; God will let me stare down my foes. | SWKCV 10 Mungu wangu unipendaye. Mungu atanitangulia, naye atanifanya niwachekelee wale wanaonisingizia. |
| BSB 11 Do not kill them, or my people will forget. Scatter them by Your power, and bring them down, O Lord, our shield. | SWKCV 11 Lakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu, au sivyo watu wangu watasahau. Katika uwezo wako wafanye watangetange na uwashushe chini. |
| BSB 12 By the sins of their mouths and the words of their lips, let them be trapped in their pride, in the curses and lies they utter. | SWKCV 12 Kwa ajili ya dhambi za vinywa vyao, kwa ajili ya maneno ya midomo yao, waache wanaswe katika kiburi chao. Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka, |
| BSB 13 Consume them in wrath; consume them till they are no more, so it may be known to the ends of the earth that God rules over Jacob. Selah | SWKCV 13 wateketeze katika ghadhabu, wateketeze hadi wasiwepo tena. Ndipo itakapofahamika katika miisho ya dunia kwamba Mungu anatawala juu ya Yakobo. |
| BSB 14 They return in the evening, snarling like dogs and prowling around the city. | SWKCV 14 Hurudi jioni, wakibweka kama mbwa, wakiuzurura mji. |
| BSB 15 They scavenge for food, and growl if they are not satisfied. | SWKCV 15 Wanatangatanga wakitafuta chakula, wasipotosheka hubweka kama mbwa. |
| BSB 16 But I will sing of Your strength and proclaim Your loving devotion in the morning. For You are my fortress, my refuge in times of trouble. | SWKCV 16 Lakini mimi nitaziimba nguvu zako, asubuhi nitaimba juu ya upendo wako; kwa maana wewe ndiwe ngome yangu na kimbilio langu wakati wa shida. |
| BSB 17 To You, O my strength, I sing praises, for You, O God, are my fortress, my God of loving devotion. | SWKCV 17 Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa. Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, Mungu unipendaye. |
Questions about Psalms 59? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.