1 Timothy 4
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now the Spirit expressly states that in later times some will abandon the faith to follow deceitful spirits and the teachings of demons, | SWKCV 1 Roho asema waziwazi kwamba katika siku za mwisho baadhi ya watu wataiacha imani na kufuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. |
| BSB 2 influenced by the hypocrisy of liars, whose consciences are seared with a hot iron. | SWKCV 2 Mafundisho kama hayo huja kupitia kwa waongo ambao ni wanafiki, hali dhamiri zao zikiungua kwa kuchomwa moto. |
| BSB 3 They will prohibit marriage and require abstinence from certain foods that God has created to be received with thanksgiving by those who believe and know the truth. | SWKCV 3 Wao huwakataza watu wasioe na kuwaagiza wajiepushe na vyakula fulani, ambavyo Mungu aliviumba ili vipokewe kwa shukrani na wale wanaoamini na kuijua kweli. |
| BSB 4 For every creation of God is good, and nothing that is received with thanksgiving should be rejected, | SWKCV 4 Kwa maana kila kitu alichokiumba Mungu ni chema, wala hakuna kitu chochote cha kukataliwa kama kikipokewa kwa shukrani, |
| BSB 5 because it is sanctified by the word of God and prayer. | SWKCV 5 kwa sababu kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba. |
| BSB 6 By pointing out these things to the brothers, you will be a good servant of Christ Jesus, nourished by the words of faith and sound instruction that you have followed. | SWKCV 6 Kama ukiwakumbusha ndugu mambo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, uliyelelewa katika kweli ya imani na yale mafundisho mazuri uliyoyafuata. |
| BSB 7 But reject irreverent, silly myths. Instead, train yourself for godliness. | SWKCV 7 Usijishughulishe kamwe na hadithi za kipagani na masimulizi ya uongo ya wanawake wazee; badala yake, jizoeze kuwa mtauwa. |
| BSB 8 For physical exercise is of limited value, but godliness is valuable in every way, holding promise for the present life and for the one to come. | SWKCV 8 Kwa maana mazoezi ya mwili yana faida kwa sehemu, lakini utauwa una faida katika mambo yote, yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa na ya ule ujao. |
| BSB 9 This is a trustworthy saying, worthy of full acceptance. | SWKCV 9 Hili ni neno la kuaminiwa tena lastahili kukubaliwa kabisa, |
| BSB 10 To this end we labor and strive, because we have set our hope on the living God, who is the Savior of everyone, and especially of those who believe. | SWKCV 10 (nasi kwa ajili ya hili tunajitaabisha na kujitahidi), kwamba tumeweka tumaini letu kwa Mungu aliye hai, ambaye ni Mwokozi wa watu wote, hasa wale waaminio. |
| BSB 11 Command and teach these things. | SWKCV 11 Mambo haya yaagize na kuyafundisha. |
| BSB 12 Let no one despise your youth, but set an example for the believers in speech, in conduct, in love, in faith, in purity. | SWKCV 12 Mtu yeyote asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe kielelezo kizuri kwa waumini katika usemi, mwenendo, upendo, imani na usafi. |
| BSB 13 Until I come, devote yourself to the public reading of Scripture, to exhortation, and to teaching. | SWKCV 13 Fanya bidii kusoma Maandiko hadharani, kuhubiri na kufundisha, mpaka nitakapokuja. |
| BSB 14 Do not neglect the gift that is in you, which was given you through the prophecy spoken over you at the laying on of the hands of the elders. | SWKCV 14 Usiache kutumia kipawa kilicho ndani yako, ambacho ulipewa kwa neno la unabii wakati wazee walikuwekea mikono. |
| BSB 15 Be diligent in these matters and absorbed in them, so that your progress will be evident to all. | SWKCV 15 Uwe na bidii katika mambo haya; ujitolee kwa ajili ya mambo haya kikamilifu, ili kila mtu aone kuendelea kwako. |
| BSB 16 Pay close attention to your life and to your teaching. Persevere in these things, for by so doing you will save both yourself and those who hear you. | SWKCV 16 Jilinde sana nafsi yako na mafundisho yako. Dumu katika hayo, kwa maana kwa kufanya hivyo, utajiokoa wewe mwenyewe pamoja na wale wanaokusikia. |
Questions about 1 Timothy 4? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.