2 Samuel 22
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 And David sang this song to the LORD on the day the LORD had delivered him from the hand of all his enemies and from the hand of Saul. | SWKCV 1 Daudi alimwimbia Bwana maneno ya wimbo huu wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. |
| BSB 2 He said: “The LORD is my rock, my fortress, and my deliverer. | SWKCV 2 Akasema: “Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, |
| BSB 3 My God is my rock, in whom I take refuge, my shield, and the horn of my salvation. My stronghold, my refuge, and my Savior, You save me from violence. | SWKCV 3 Mungu wangu ni mwamba wangu, ambaye kwake ninakimbilia, ngao yangu na pembe ya wokovu wangu. Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu na mwokozi wangu, huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri. |
| BSB 4 I will call upon the LORD, who is worthy to be praised; so shall I be saved from my enemies. | SWKCV 4 Ninamwita Bwana, anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu. |
| BSB 5 For the waves of death engulfed me; the torrents of chaos overwhelmed me. | SWKCV 5 “Mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea. |
| BSB 6 The cords of Sheol entangled me; the snares of death confronted me. | SWKCV 6 Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili. |
| BSB 7 In my distress I called upon the LORD; I cried out to my God. And from His temple He heard my voice, and my cry for help reached His ears. | SWKCV 7 Katika shida yangu nalimwita Bwana, nilimlilia Mungu wangu. Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika masikioni mwake. |
| BSB 8 Then the earth shook and quaked; the foundations of the heavens trembled; they were shaken because He burned with anger. | SWKCV 8 “Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya mbingu ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika. |
| BSB 9 Smoke rose from His nostrils, and consuming fire came from His mouth; glowing coals blazed forth. | SWKCV 9 Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake. |
| BSB 10 He parted the heavens and came down with dark clouds beneath His feet. | SWKCV 10 Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake. |
| BSB 11 He mounted a cherub and flew; He soared on the wings of the wind. | SWKCV 11 Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo. |
| BSB 12 He made darkness a canopy around Him, a gathering of water and thick clouds. | SWKCV 12 Alifanya giza hema lake la kujifunika: mawingu meusi ya mvua ya angani. |
| BSB 13 From the brightness of His presence coals of fire blazed forth. | SWKCV 13 Kutokana na mwanga wa uwepo wake mawingu yalisogea, ikanyesha mvua ya mawe na umeme wa radi. |
| BSB 14 The LORD thundered from heaven; the voice of the Most High resounded. | SWKCV 14 Bwana alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika. |
| BSB 15 He shot His arrows and scattered the foes; He hurled lightning and routed them. | SWKCV 15 Aliipiga mishale na kutawanya adui, umeme wa radi na kuwafukuza. |
| BSB 16 The channels of the sea appeared, and the foundations of the world were exposed at the rebuke of the LORD, at the blast of the breath of His nostrils. | SWKCV 16 Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwake Bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake. |
| BSB 17 He reached down from on high and took hold of me; He drew me out of deep waters. | SWKCV 17 “Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu. |
| BSB 18 He rescued me from my powerful enemy, from foes too mighty for me. | SWKCV 18 Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi. |
| BSB 19 They confronted me in my day of calamity, but the LORD was my support. | SWKCV 19 Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini Bwana alikuwa msaada wangu. |
| BSB 20 He brought me out into the open; He rescued me because He delighted in me. | SWKCV 20 Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami. |
| BSB 21 The LORD has rewarded me according to my righteousness; He has repaid me according to the cleanness of my hands. | SWKCV 21 “Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa. |
| BSB 22 For I have kept the ways of the LORD and have not wickedly departed from my God. | SWKCV 22 Kwa maana nimezishika njia za Bwana; sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu. |
| BSB 23 For all His ordinances are before me; I have not disregarded His statutes. | SWKCV 23 Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake. |
| BSB 24 And I have been blameless before Him and kept myself from iniquity. | SWKCV 24 Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi. |
| BSB 25 So the LORD has repaid me according to my righteousness, according to my cleanness in His sight. | SWKCV 25 Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu, sawasawa na usafi wangu machoni pake. |
| BSB 26 To the faithful You show Yourself faithful, to the blameless You show Yourself blameless; | SWKCV 26 “Kwa yeye aliye mwaminifu unajionyesha kuwa mwaminifu, kwa asiye na hatia unajionyesha kutokuwa na hatia, |
| BSB 27 to the pure You show Yourself pure, but to the crooked You show Yourself shrewd. | SWKCV 27 kwa aliye mtakatifu unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi. |
| BSB 28 You save an afflicted people, but Your eyes are on the haughty to bring them down. | SWKCV 28 Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini macho yako ni juu ya wenye kiburi ili uwashushe. |
| BSB 29 For You, O LORD, are my lamp; the LORD lights up my darkness. | SWKCV 29 Wewe ni taa yangu, Ee Bwana. Bwana hulifanya giza langu kuwa mwanga. |
| BSB 30 For in You I can charge an army; with my God I can scale a wall. | SWKCV 30 Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, nikiwa pamoja na Mungu wangu nitaweza kuruka ukuta. |
| BSB 31 As for God, His way is perfect; the word of the LORD is flawless. He is a shield to all who take refuge in Him. | SWKCV 31 “Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; neno la Bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake. |
| BSB 32 For who is God besides the LORD? And who is the Rock except our God? | SWKCV 32 Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu? |
| BSB 33 God is my strong fortress, and He makes my way clear. | SWKCV 33 Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. |
| BSB 34 He makes my feet like those of a deer and stations me upon the heights. | SWKCV 34 Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu. |
| BSB 35 He trains my hands for battle; my arms can bend a bow of bronze. | SWKCV 35 Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba. |
| BSB 36 You have given me Your shield of salvation, and Your gentleness exalts me. | SWKCV 36 Hunipa ngao yako ya ushindi, unajishusha chini ili kuniinua. |
| BSB 37 You broaden the path beneath me so that my ankles do not give way. | SWKCV 37 Huyapanua mapito yangu, ili miguu yangu isiteleze. |
| BSB 38 I pursued my enemies and destroyed them; I did not turn back until they were consumed. | SWKCV 38 “Niliwafuatia adui zangu na nikawaseta, sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa. |
| BSB 39 I devoured and crushed them so they could not rise; they have fallen under my feet. | SWKCV 39 Niliwaseta kabisa, nao hawakuweza kuinuka tena; walianguka chini ya miguu yangu. |
| BSB 40 You have armed me with strength for battle; You have subdued my foes beneath me. | SWKCV 40 Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu. |
| BSB 41 You have made my enemies retreat before me; I destroyed those who hated me. | SWKCV 41 Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, nami nikawaangamiza adui zangu. |
| BSB 42 They looked, but there was no one to save them—to the LORD, but He did not answer. | SWKCV 42 Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa; walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu. |
| BSB 43 I ground them as the dust of the earth; I crushed and trampled them like mud in the streets. | SWKCV 43 Niliwaponda kama mavumbi ya nchi; niliwaponda na kuwakanyaga kama tope barabarani. |
| BSB 44 You have delivered me from the strife of my people; You have preserved me as the head of nations; a people I had not known shall serve me. | SWKCV 44 “Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu wangu; umenihifadhi mimi kama kiongozi wa mataifa. Watu ambao sikuwajua wananitumikia, |
| BSB 45 Foreigners cower before me; when they hear me, they obey me. | SWKCV 45 nao wageni huja wakininyenyekea, mara wanisikiapo, hunitii. |
| BSB 46 Foreigners lose heart and come trembling from their strongholds. | SWKCV 46 Wote wanalegea, wanatoka katika ngome zao wakitetemeka. |
| BSB 47 The LORD lives, and blessed be my Rock! And may God, the Rock of my salvation, be exalted— | SWKCV 47 “Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! Atukuzwe Mungu, Mwamba, Mwokozi wangu! |
| BSB 48 the God who avenges me and brings down nations beneath me, | SWKCV 48 Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi, ayawekaye mataifa chini yangu, |
| BSB 49 who frees me from my enemies. You exalt me above my foes; You rescue me from violent men. | SWKCV 49 aniwekaye huru toka kwa adui zangu. Uliniinua juu ya adui zangu; uliniokoa toka kwa watu wajeuri. |
| BSB 50 Therefore I will praise You, O LORD, among the nations; I will sing praises to Your name. | SWKCV 50 Kwa hiyo nitakusifu, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaliimbia sifa jina lako. |
| BSB 51 Great salvation He brings to His king. He shows loving devotion to His anointed, to David and his descendants forever.” | SWKCV 51 Humpa mfalme wake ushindi mkuu; huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake, kwa Daudi na wazao wake milele.” |
Questions about 2 Samuel 22? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.