Deuteronomy 27
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then Moses and the elders of Israel commanded the people: “Keep all the commandments I am giving you today. | SWKCV 1 Mose na wazee wa Israeli wakawaagiza watu: “Yashikeni maagizo haya yote ninayowaagiza leo. |
| BSB 2 And on the day you cross the Jordan into the land that the LORD your God is giving you, set up large stones and coat them with plaster. | SWKCV 2 Mtakapokuwa mmevuka Mto Yordani na kuingia katika nchi awapayo Bwana Mungu wenu, msimamishe mawe makubwa na mkayatie lipu. |
| BSB 3 Write on them all the words of this law when you have crossed over to enter the land that the LORD your God is giving you, a land flowing with milk and honey, just as the LORD, the God of your fathers, has promised you. | SWKCV 3 Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi awapayo Bwana Mungu wenu, nchi itiririkayo maziwa na asali, kama vile Bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi. |
| BSB 4 And when you have crossed the Jordan, you are to set up these stones on Mount Ebal, as I am commanding you today, and you are to coat them with plaster. | SWKCV 4 Mtakapokuwa mmevuka Yordani, simamisheni mawe haya juu ya Mlima Ebali, kama ninavyowaagiza leo, mkayatie lipu. |
| BSB 5 Moreover, you are to build there an altar to the LORD your God, an altar of stones. You must not use any iron tool on them. | SWKCV 5 Huko mjengeeni Bwana Mungu wenu madhabahu, madhabahu ya mawe. Msitumie kifaa chochote cha chuma juu yake. |
| BSB 6 You shall build the altar of the LORD your God with uncut stones and offer upon it burnt offerings to the LORD your God. | SWKCV 6 Jengeni madhabahu ya Bwana Mungu wenu kwa mawe ya shambani, na mtoe sadaka za kuteketezwa juu yake kwa Bwana Mungu wenu. |
| BSB 7 There you are to sacrifice your peace offerings, eating them and rejoicing in the presence of the LORD your God. | SWKCV 7 Toeni sadaka za amani juu yake, mkizila na kufurahia mbele za Bwana Mungu wenu. |
| BSB 8 And you shall write distinctly upon these stones all the words of this law.” | SWKCV 8 Nanyi mtaandika maneno yote ya sheria hii kwa wazi sana juu ya mawe haya ambayo mmesimamisha.” |
| BSB 9 Then Moses and the Levitical priests spoke to all Israel: “Be silent, O Israel, and listen! This day you have become the people of the LORD your God. | SWKCV 9 Kisha Mose na makuhani, ambao ni Walawi, wakawaambia Israeli wote, “Nyamaza ee Israeli, sikiliza! Sasa umekuwa taifa la Bwana Mungu wako. |
| BSB 10 You shall therefore obey the voice of the LORD your God and follow His commandments and statutes I am giving you today.” | SWKCV 10 Mtii Bwana Mungu wako, na kufuata amri zake na maagizo ninayokupa leo.” |
| BSB 11 On that day Moses commanded the people: | SWKCV 11 Siku ile ile Mose akawaagiza watu: |
| BSB 12 “When you have crossed the Jordan, these tribes shall stand on Mount Gerizim to bless the people: Simeon, Levi, Judah, Issachar, Joseph, and Benjamin. | SWKCV 12 Mtakapovuka Mto Yordani, makabila haya yatasimama juu ya Mlima Gerizimu kubariki watu: Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Yosefu na Benyamini. |
| BSB 13 And these tribes shall stand on Mount Ebal to deliver the curse: Reuben, Gad, Asher, Zebulun, Dan, and Naphtali. | SWKCV 13 Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali. |
| BSB 14 Then the Levites shall proclaim in a loud voice to every Israelite: | SWKCV 14 Nao Walawi watawasomea watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa: |
| BSB 15 ‘Cursed is the man who makes a carved idol or molten image—an abomination to the LORD, the work of the hands of a craftsman—and sets it up in secret.’ And let all the people say, ‘Amen!’ | SWKCV 15 “Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
| BSB 16 ‘Cursed is he who dishonors his father or mother.’ And let all the people say, ‘Amen!’ | SWKCV 16 “Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
| BSB 17 ‘Cursed is he who moves his neighbor’s boundary stone.’ And let all the people say, ‘Amen!’ | SWKCV 17 “Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
| BSB 18 ‘Cursed is he who lets a blind man wander in the road.’ And let all the people say, ‘Amen!’ | SWKCV 18 “Alaaniwe mtu ampotoshaye kipofu njiani.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
| BSB 19 ‘Cursed is he who withholds justice from the foreigner, the fatherless, or the widow.’ And let all the people say, ‘Amen!’ | SWKCV 19 “Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
| BSB 20 ‘Cursed is he who sleeps with his father’s wife, for he has violated his father’s marriage bed.’ And let all the people say, ‘Amen!’ | SWKCV 20 “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
| BSB 21 ‘Cursed is he who lies with any animal.’ And let all the people say, ‘Amen!’ | SWKCV 21 “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama yeyote.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
| BSB 22 ‘Cursed is he who sleeps with his sister, the daughter of his father or the daughter of his mother.’ And let all the people say, ‘Amen!’ | SWKCV 22 “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na dada yake, binti wa baba yake au binti wa mama yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
| BSB 23 ‘Cursed is he who sleeps with his mother-in-law.’ And let all the people say, ‘Amen!’ | SWKCV 23 “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mama mkwe wake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
| BSB 24 ‘Cursed is he who strikes down his neighbor in secret.’ And let all the people say, ‘Amen!’ | SWKCV 24 “Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
| BSB 25 ‘Cursed is he who accepts a bribe to kill an innocent person.’ And let all the people say, ‘Amen!’ | SWKCV 25 “Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumuua mtu asiye na hatia.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
| BSB 26 ‘Cursed is he who does not put the words of this law into practice.’ And let all the people say, ‘Amen!’ | SWKCV 26 “Alaaniwe mtu yule ambaye hatashikilia maneno ya sheria hii kwa kuyatekeleza.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” |
Questions about Deuteronomy 27? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.