Exodus 20
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 And God spoke all these words: | SWKCV 1 Ndipo Mungu akasema maneno haya yote: |
| BSB 2 “I am the LORD your God, who brought you out of the land of Egypt, out of the house of slavery. | SWKCV 2 “Mimi ndimi Bwana Mungu wako, niliyekutoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. |
| BSB 3 You shall have no other gods before Me. | SWKCV 3 Usiwe na miungu mingine ila mimi. |
| BSB 4 You shall not make for yourself an idol in the form of anything in the heavens above, on the earth below, or in the waters beneath. | SWKCV 4 Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. |
| BSB 5 You shall not bow down to them or worship them; for I, the LORD your God, am a jealous God, visiting the iniquity of the fathers on their children to the third and fourth generations of those who hate Me, | SWKCV 5 Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, |
| BSB 6 but showing loving devotion to a thousand generations of those who love Me and keep My commandments. | SWKCV 6 lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu. |
| BSB 7 You shall not take the name of the LORD your God in vain, for the LORD will not leave anyone unpunished who takes His name in vain. | SWKCV 7 Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure. |
| BSB 8 Remember the Sabbath day by keeping it holy. | SWKCV 8 Ikumbuke siku ya Sabato, uitakase. |
| BSB 9 Six days you shall labor and do all your work, | SWKCV 9 Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote, |
| BSB 10 but the seventh day is a Sabbath to the LORD your God, on which you must not do any work—neither you, nor your son or daughter, nor your manservant or maidservant or livestock, nor the foreigner within your gates. | SWKCV 10 lakini siku ya saba ni Sabato kwa Bwana Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike, wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. |
| BSB 11 For in six days the LORD made the heavens and the earth and the sea and all that is in them, but on the seventh day He rested. Therefore the LORD blessed the Sabbath day and set it apart as holy. | SWKCV 11 Kwa kuwa kwa siku sita, Bwana aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo Bwana akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu. |
| BSB 12 Honor your father and mother, so that your days may be long in the land that the LORD your God is giving you. | SWKCV 12 Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako. |
| BSB 13 You shall not murder. | SWKCV 13 Usiue. |
| BSB 14 You shall not commit adultery. | SWKCV 14 Usizini. |
| BSB 15 You shall not steal. | SWKCV 15 Usiibe. |
| BSB 16 You shall not bear false witness against your neighbor. | SWKCV 16 Usimshuhudie jirani yako uongo. |
| BSB 17 You shall not covet your neighbor’s house. You shall not covet your neighbor’s wife, or his manservant or maidservant, or his ox or donkey, or anything that belongs to your neighbor.” | SWKCV 17 Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ngʼombe wake au punda wake, wala chochote kile alicho nacho jirani yako.” |
| BSB 18 When all the people witnessed the thunder and lightning, the sounding of the ram’s horn, and the mountain enveloped in smoke, they trembled and stood at a distance. | SWKCV 18 Watu walipoona ngurumo na radi, na kusikia mlio wa tarumbeta, na kuuona mlima katika moshi, walitetemeka kwa woga. Wakasimama mbali |
| BSB 19 “Speak to us yourself and we will listen,” they said to Moses. “But do not let God speak to us, or we will die.” | SWKCV 19 na wakamwambia Mose, “Sema nasi wewe mwenyewe, nasi tutakusikiliza. Lakini usimwache Mungu aseme nasi, la sivyo tutakufa.” |
| BSB 20 “Do not be afraid,” Moses replied. “For God has come to test you, so that the fear of Him may be before you, to keep you from sinning.” | SWKCV 20 Mose akawaambia watu, “Msiogope! Mungu amekuja kuwajaribu, ili kwamba hofu ya Mungu iwakalie, msitende dhambi.” |
| BSB 21 And the people stood at a distance as Moses approached the thick darkness where God was. | SWKCV 21 Watu wakabaki mbali, wakati Mose alipolisogelea lile giza nene mahali pale Mungu alipokuwa. |
| BSB 22 Then the LORD said to Moses, “This is what you are to tell the Israelites: ‘You have seen for yourselves that I have spoken to you from heaven. | SWKCV 22 Kisha Bwana akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli hivi: ‘Mmejionea wenyewe kwamba nimesema nanyi kutoka mbinguni: |
| BSB 23 You are not to make any gods alongside Me; you are not to make for yourselves gods of silver or gold. | SWKCV 23 Msijifanyizie miungu yoyote na kuilinganisha nami, msijitengenezee miungu ya fedha wala miungu ya dhahabu. |
| BSB 24 You are to make for Me an altar of earth, and sacrifice on it your burnt offerings and peace offerings, your sheep and goats and cattle. In every place where I cause My name to be remembered, I will come to you and bless you. | SWKCV 24 “ ‘Utanitengenezea madhabahu ya udongo, na juu yake utoe sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani, kondoo zako, mbuzi na ngʼombe zako. Popote nitakapofanya Jina langu liheshimiwe, nitakuja kwenu na kuwabariki. |
| BSB 25 Now if you make an altar of stones for Me, you must not build it with stones shaped by tools; for if you use a chisel on it, you will defile it. | SWKCV 25 Ikiwa unanitengenezea madhabahu ya mawe, usiijenge kwa mawe ya kuchonga, maana mkitumia chombo cha kuchongea mtaitia unajisi. |
| BSB 26 And you must not go up to My altar on steps, lest your nakedness be exposed on it.’ | SWKCV 26 Msitumie ngazi kupandia kwenye madhabahu yangu, uchi wako usije ukadhihirika kwa chini.’ |
Questions about Exodus 20? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.