Exodus 23
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “You shall not spread a false report. Do not join the wicked by being a malicious witness. | SWKCV 1 “Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine. |
| BSB 2 You shall not follow the crowd in wrongdoing. When you testify in a lawsuit, do not pervert justice by siding with the crowd. | SWKCV 2 “Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu, |
| BSB 3 And do not show favoritism to a poor man in his lawsuit. | SWKCV 3 nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake. |
| BSB 4 If you encounter your enemy’s stray ox or donkey, you must return it to him. | SWKCV 4 “Kama ukikutana na maksai au punda wa adui yako anapotea, hakikisha umemrudisha kwake. |
| BSB 5 If you see the donkey of one who hates you fallen under its load, do not leave it there; you must help him with it. | SWKCV 5 Ukiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia. |
| BSB 6 You shall not deny justice to the poor in their lawsuits. | SWKCV 6 “Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao. |
| BSB 7 Stay far away from a false accusation. Do not kill the innocent or the just, for I will not acquit the guilty. | SWKCV 7 Ujiepushe na mashtaka ya uongo, wala usimuue mtu asiye na hatia au mtu mwaminifu, kwa maana sitamhesabia hana hatia yeye aliye na hatia. |
| BSB 8 Do not accept a bribe, for a bribe blinds those who see and twists the words of the righteous. | SWKCV 8 “Usipokee rushwa, kwa kuwa rushwa hupofusha wale waonao, na kupinda maneno ya wenye haki. |
| BSB 9 Do not oppress a foreign resident, since you yourselves know how it feels to be foreigners; for you were foreigners in the land of Egypt. | SWKCV 9 “Usimwonee mgeni; ninyi wenyewe mnajua jinsi mgeni anavyojisikia, kwa sababu mlikuwa wageni Misri. |
| BSB 10 For six years you are to sow your land and gather its produce, | SWKCV 10 “Kwa muda wa miaka sita mtapanda mashamba yenu na kuvuna mazao, |
| BSB 11 but in the seventh year you must let it rest and lie fallow, so that the poor among your people may eat from the field and the wild animals may consume what they leave. Do the same with your vineyard and olive grove. | SWKCV 11 lakini katika mwaka wa saba usiilime ardhi wala kuitumia, ili watu walio maskini miongoni mwenu waweze kupata chakula kutoka kwenye hayo mashamba, nao wanyama pori wapate chakula kwa yale mabaki watakayobakiza. Utafanya hivyo katika shamba lako la mizabibu na la mizeituni. |
| BSB 12 For six days you are to do your work, but on the seventh day you must cease, so that your ox and your donkey may rest and the son of your maidservant may be refreshed, as well as the foreign resident. | SWKCV 12 “Kwa siku sita fanya kazi zako, lakini siku ya saba usifanye kazi, ili maksai wako na punda wako wapate kupumzika, naye mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwako, pamoja na mgeni, wapate kustarehe. |
| BSB 13 Pay close attention to everything I have said to you. You must not invoke the names of other gods; they must not be heard on your lips. | SWKCV 13 “Uzingatie kutenda kila kitu nilichokuambia. Usiombe kwa majina ya miungu mingine, wala usiyaruhusu kusikika kinywani mwako. |
| BSB 14 Three times a year you are to celebrate a feast to Me. | SWKCV 14 “Mara tatu kwa mwaka utanifanyia sikukuu. |
| BSB 15 You are to keep the Feast of Unleavened Bread as I commanded you: At the appointed time in the month of Abib you are to eat unleavened bread for seven days, because that was the month you came out of Egypt. No one may appear before Me empty-handed. | SWKCV 15 “Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu; kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu kama nilivyokuagiza. Fanya jambo hili kwa wakati uliopangwa katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa sababu katika mwezi huo ulitoka Misri. “Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu. |
| BSB 16 You are also to keep the Feast of Harvest with the firstfruits of the produce from what you sow in the field. And keep the Feast of Ingathering at the end of the year, when you gather your produce from the field. | SWKCV 16 “Utaadhimisha Sikukuu ya Mavuno kwa malimbuko ya mazao yako uliyopanda katika shamba lako. “Utaadhimisha Sikukuu ya Kukusanya mavuno mwishoni mwa mwaka, unapokusanya mavuno yako toka shambani. |
| BSB 17 Three times a year all your males are to appear before the Lord GOD. | SWKCV 17 “Mara tatu kwa mwaka wanaume wote watakuja mbele za Bwana Mwenyezi. |
| BSB 18 You must not offer the blood of My sacrifices with anything leavened, nor may the fat of My feast remain until morning. | SWKCV 18 “Msitoe damu ya dhabihu kwangu pamoja na kitu chochote kilicho na chachu. “Mafuta ya mnyama wa sadaka ya sikukuu yangu yasibakizwe mpaka asubuhi. |
| BSB 19 Bring the best of the firstfruits of your soil to the house of the LORD your God. You must not cook a young goat in its mother’s milk. | SWKCV 19 “Utaleta malimbuko bora ya ardhi yako katika nyumba ya Bwana Mungu wako. “Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake. |
| BSB 20 Behold, I am sending an angel before you to protect you along the way and to bring you to the place I have prepared. | SWKCV 20 “Tazama, ninamtuma malaika akutangulie mbele yako akulinde njiani na kukuleta mpaka mahali nilipoandaa. |
| BSB 21 Pay attention to him and listen to his voice; do not defy him, for he will not forgive rebellion, since My Name is in him. | SWKCV 21 Mtamtii na kusikiliza kile anachokisema. Usiasi dhidi yake; hatakusamehe uasi wako, kwa maana Jina langu limo ndani yake. |
| BSB 22 But if you will listen carefully to his voice and do everything I say, I will be an enemy to your enemies and a foe to your foes. | SWKCV 22 Kama ukitii kweli kweli kile asemacho na kufanya yote nisemayo, nitakuwa adui wa adui zako, na nitawapinga wale wakupingao. |
| BSB 23 For My angel will go before you and bring you into the land of the Amorites, Hittites, Perizzites, Canaanites, Hivites, and Jebusites, and I will annihilate them. | SWKCV 23 Malaika wangu atatangulia mbele yako na kukuleta katika nchi ya Waamori, Wahiti, Waperizi, Wakanaani, Wahivi na Wayebusi, nami nitawafutilia mbali. |
| BSB 24 You must not bow down to their gods or serve them or follow their practices. Instead, you are to demolish them and smash their sacred stones to pieces. | SWKCV 24 Usiisujudie miungu yao, au kuiabudu, wala kufuata desturi yao. Utayabomoa kabisa na kuvunjavunja mawe yao ya ibada vipande vipande. |
| BSB 25 So you shall serve the LORD your God, and He will bless your bread and your water. And I will take away sickness from among you. | SWKCV 25 Utamwabudu Bwana Mungu wako, na baraka zake zitakuwa juu ya vyakula vyako na maji yako. Nami nitaondoa maradhi miongoni mwako, |
| BSB 26 No woman in your land will miscarry or be barren; I will fulfill the number of your days. | SWKCV 26 na hakuna atakayeharibu mimba wala atakayekuwa tasa katika nchi yako. Nami nitakupa maisha makamilifu. |
| BSB 27 I will send My terror ahead of you and throw into confusion every nation you encounter. I will make all your enemies turn and run. | SWKCV 27 “Nitapeleka utisho wangu mbele yako na kufadhaisha kila taifa utakalolifikia. Nitafanya adui zako wote wakupe kisogo na kukimbia. |
| BSB 28 I will send the hornet before you to drive the Hivites and Canaanites and Hittites out of your way. | SWKCV 28 Nitatanguliza manyigu mbele yako kuwafukuza Wahivi, Wakanaani na Wahiti waondoke njiani mwako. |
| BSB 29 I will not drive them out before you in a single year; otherwise the land would become desolate and wild animals would multiply against you. | SWKCV 29 Lakini sitawafukuza kwa mara moja, kwa sababu nchi itabaki ukiwa na wanyama pori watakuwa wengi mno kwako. |
| BSB 30 Little by little I will drive them out ahead of you, until you become fruitful and possess the land. | SWKCV 30 Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, mpaka uwe umeongezeka kiasi cha kutosha kuimiliki nchi. |
| BSB 31 And I will establish your borders from the Red Sea to the Sea of the Philistines, and from the desert to the Euphrates. For I will deliver the inhabitants into your hand, and you will drive them out before you. | SWKCV 31 “Nitaweka mipaka ya nchi yako kuanzia Bahari ya Shamu hadi Bahari ya Wafilisti, na kuanzia jangwani hadi Mto Frati. Nitawatia watu wanaoishi katika nchi hizo mikononi mwako, nawe utawafukuza watoke mbele yako. |
| BSB 32 You shall make no covenant with them or with their gods. | SWKCV 32 Usifanye agano lolote nao wala na miungu yao. |
| BSB 33 They must not remain in your land, lest they cause you to sin against Me. For if you serve their gods, it will surely be a snare to you.” | SWKCV 33 Usiwaache waishi katika nchi yako, la sivyo watakusababisha utende dhambi dhidi yangu, kwa sababu ibada ya miungu yao hakika itakuwa mtego kwako.” |
Questions about Exodus 23? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.