Hebrews 13
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Continue in brotherly love. | SWKCV 1 Endeleeni kupendana kama ndugu. |
| BSB 2 Do not neglect to show hospitality to strangers, for by so doing some people have entertained angels without knowing it. | SWKCV 2 Msisahau kuwakaribisha wageni, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, watu wengine waliwakaribisha malaika pasipo kujua. |
| BSB 3 Remember those in prison as if you were bound with them, and those who are mistreated as if you were suffering with them. | SWKCV 3 Wakumbukeni wale waliofungwa gerezani kana kwamba ninyi mmefungwa pamoja nao. Pia wakumbukeni wale wanaotendewa vibaya, kana kwamba ni ninyi wenyewe mnateswa. |
| BSB 4 Marriage should be honored by all and the marriage bed kept undefiled, for God will judge the sexually immoral and adulterers. | SWKCV 4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote. |
| BSB 5 Keep your lives free from the love of money and be content with what you have, for God has said: “Never will I leave you, never will I forsake you.” | SWKCV 5 Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema, “Kamwe sitakuacha, wala sitakupungukia.” |
| BSB 6 So we say with confidence: “The Lord is my helper; I will not be afraid. What can man do to me?” | SWKCV 6 Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri, “Bwana ni msaada wangu; sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini?” |
| BSB 7 Remember your leaders who spoke the word of God to you. Consider the outcome of their way of life and imitate their faith. | SWKCV 7 Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Angalieni matokeo ya mwenendo wa maisha yao mkaiige imani yao. |
| BSB 8 Jesus Christ is the same yesterday and today and forever. | SWKCV 8 Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata milele. |
| BSB 9 Do not be carried away by all kinds of strange teachings, for it is good for the heart to be strengthened by grace and not by foods of no value to those devoted to them. | SWKCV 9 Msichukuliwe na kila aina ya mafundisho ya kigeni. Ni vyema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, wala si kwa sheria kuhusu utaratibu wa vyakula, ambavyo havina faida kwa wale wanaozishika hizo sheria. |
| BSB 10 We have an altar from which those who serve at the tabernacle have no right to eat. | SWKCV 10 Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaohudumu katika hema hawana haki ya kula vile vitu vilivyowekwa juu yake. |
| BSB 11 Although the high priest brings the blood of animals into the Holy Place as a sacrifice for sin, the bodies are burned outside the camp. | SWKCV 11 Kuhani mkuu huchukua damu ya wanyama na kuiingiza Patakatifu pa Patakatifu, kama sadaka ya dhambi, lakini miili ya hao wanyama huteketezwa nje ya kambi. |
| BSB 12 And so Jesus also suffered outside the city gate, to sanctify the people by His own blood. | SWKCV 12 Vivyo hivyo, Yesu naye aliteswa nje ya lango la mji ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe. |
| BSB 13 Therefore let us go to Him outside the camp, bearing the disgrace He bore. | SWKCV 13 Kwa hiyo, basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba. |
| BSB 14 For here we do not have a permanent city, but we are looking for the city that is to come. | SWKCV 14 Kwa kuwa hapa hatuna mji udumuo, bali tunautafuta ule ujao. |
| BSB 15 Through Jesus, therefore, let us continually offer to God a sacrifice of praise, the fruit of lips that confess His name. | SWKCV 15 Basi kwa njia ya Yesu, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani matunda ya midomo inayolikiri Jina lake. |
| BSB 16 And do not neglect to do good and to share with others, for with such sacrifices God is pleased. | SWKCV 16 Na msiache kutenda mema na kushirikiana vile vitu mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mungu. |
| BSB 17 Obey your leaders and submit to them, for they watch over your souls as those who must give an account. To this end, allow them to lead with joy and not with grief, for that would be of no advantage to you. | SWKCV 17 Watiini viongozi wenu na kujinyenyekeza chini ya mamlaka yao. Kwa maana wao wanakesha kwa ajili yenu kama watu watakaopaswa kutoa hesabu. Watiini ili wafanye kazi yao kwa furaha, wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu. |
| BSB 18 Pray for us; we are convinced that we have a clear conscience and desire to live honorably in every way. | SWKCV 18 Tuombeeni. Tuna hakika kuwa tunayo dhamiri safi na shauku ya kuishi kwa uadilifu kwa kila njia. |
| BSB 19 And I especially urge you to pray that I may be restored to you soon. | SWKCV 19 Ninawasihi zaidi mniombee ili nipate kurudishwa kwenu upesi. |
| BSB 20 Now may the God of peace, who through the blood of the eternal covenant brought back from the dead our Lord Jesus, that great Shepherd of the sheep, | SWKCV 20 Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya Agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo, |
| BSB 21 equip you with every good thing to do His will. And may He accomplish in us what is pleasing in His sight through Jesus Christ, to whom be glory forever and ever. Amen. | SWKCV 21 awafanye ninyi wakamilifu mkiwa mmekamilishwa katika kila jambo jema ili mpate kutenda mapenzi yake, naye atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni Pake, kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu una yeye milele na milele. Amen. |
| BSB 22 I urge you, brothers, to bear with my word of exhortation, for I have only written to you briefly. | SWKCV 22 Ndugu zangu, nawasihi mchukuliane na maneno yangu ya maonyo, kwa kuwa nimewaandikia waraka mfupi tu. |
| BSB 23 Be aware that our brother Timothy has been released. If he arrives soon, I will come with him to see you. | SWKCV 23 Nataka ninyi mjue kwamba ndugu yetu Timotheo amefunguliwa kutoka gerezani. Akifika mapema, nitakuja pamoja naye kuwaona. |
| BSB 24 Greet all your leaders and all the saints. Those from Italy send you greetings. | SWKCV 24 Wasalimuni viongozi wenu wote na watakatifu wote. Wale wa kutoka Italia wanawasalimu. |
| BSB 25 Grace be with all of you. | SWKCV 25 Neema iwe nanyi nyote. Amen. |
Questions about Hebrews 13? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.