Hebrews 3
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Therefore, holy brothers, who share in the heavenly calling, set your focus on Jesus, the apostle and high priest whom we confess. | SWKCV 1 Kwa hiyo ndugu watakatifu, mnaoshiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini Yesu, mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu. |
| BSB 2 He was faithful to the One who appointed Him, just as Moses was faithful in all God’s house. | SWKCV 2 Alikuwa mwaminifu kwa yeye aliyemweka, kama vile Mose alivyokuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu. |
| BSB 3 For Jesus has been counted worthy of greater glory than Moses, just as the builder of a house has greater honor than the house itself. | SWKCV 3 Yesu ameonekana anastahili heshima kubwa kuliko Mose, kama vile mjenzi wa nyumba alivyo wa heshima kubwa kuliko nyumba yenyewe. |
| BSB 4 And every house is built by someone, but God is the builder of everything. | SWKCV 4 Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini Mungu ni mjenzi wa kila kitu. |
| BSB 5 Now Moses was faithful as a servant in all God’s house, testifying to what would be spoken later. | SWKCV 5 Basi Mose kama mtumishi alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu, akishuhudia kwa yale ambayo yangetamkwa baadaye. |
| BSB 6 But Christ is faithful as the Son over God’s house. And we are His house, if we hold firmly to our confidence and the hope of which we boast. | SWKCV 6 Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana katika nyumba ya Mungu. Sisi ndio nyumba yake, kama tutashikilia sana ujasiri wetu na tumaini tunalojivunia. |
| BSB 7 Therefore, as the Holy Spirit says: “Today, if you hear His voice, | SWKCV 7 Kwa hiyo, kama Roho Mtakatifu asemavyo: “Leo, kama mkiisikia sauti yake, |
| BSB 8 do not harden your hearts, as you did in the rebellion, in the day of testing in the wilderness, | SWKCV 8 msiifanye mioyo yenu migumu, kama mlivyofanya katika uasi, wakati ule wa kujaribiwa jangwani, |
| BSB 9 where your fathers tested and tried Me, and for forty years saw My works. | SWKCV 9 ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima ingawa kwa miaka arobaini walikuwa wameyaona matendo yangu. |
| BSB 10 Therefore I was angry with that generation, and I said, ‘Their hearts are always going astray, and they have not known My ways.’ | SWKCV 10 Hiyo ndiyo sababu nilikasirikia kizazi kile, nami nikasema, ‘Siku zote mioyo yao imepotoka, nao hawajazijua njia zangu.’ |
| BSB 11 So I swore on oath in My anger, ‘They shall never enter My rest.’” | SWKCV 11 Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu, ‘Kamwe hawataingia rahani mwangu.’” |
| BSB 12 See to it, brothers, that none of you has a wicked heart of unbelief that turns away from the living God. | SWKCV 12 Ndugu zangu, angalieni, asiwepo miongoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, unaojitenga na Mungu aliye hai. |
| BSB 13 But exhort one another daily, as long as it is called today, so that none of you may be hardened by sin’s deceitfulness. | SWKCV 13 Lakini mtiane moyo mtu na mwenzake kila siku, maadamu iitwapo Leo, ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. |
| BSB 14 We have come to share in Christ if we hold firmly to the end the assurance we had at first. | SWKCV 14 Kwa kuwa tumekuwa washiriki wa Kristo, kama tukishikamana tu kwa uthabiti na tumaini letu la kwanza hadi mwisho. |
| BSB 15 As it has been said: “Today, if you hear His voice, do not harden your hearts, as you did in the rebellion.” | SWKCV 15 Kama ilivyonenwa: “Leo, kama mkiisikia sauti yake, msiifanye mioyo yenu migumu kama mlivyofanya wakati wa kuasi.” |
| BSB 16 For who were the ones who heard and rebelled? Were they not all those Moses led out of Egypt? | SWKCV 16 Basi ni nani waliosikia lakini bado wakaasi? Je, si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Mose? |
| BSB 17 And with whom was God angry for forty years? Was it not with those who sinned, whose bodies fell in the wilderness? | SWKCV 17 Lakini ni nani aliowakasirikia miaka arobaini? Je, si wale waliofanya dhambi ambao miili yao ilianguka jangwani? |
| BSB 18 And to whom did He swear that they would never enter His rest? Was it not to those who disobeyed? | SWKCV 18 Ni nani hao ambao Mungu aliapa kuwa kamwe hawataingia rahani mwake isipokuwa ni wale waliokataa kutii? |
| BSB 19 So we see that it was because of their unbelief that they were unable to enter. | SWKCV 19 Hivyo tunaona kwamba hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao. |
Questions about Hebrews 3? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.