James 2
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 My brothers, as you hold out your faith in our glorious Lord Jesus Christ, do not show favoritism. | SWKCV 1 Ndugu zangu, kama waaminio katika imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe na upendeleo kwa watu. |
| BSB 2 Suppose a man comes into your meeting wearing a gold ring and fine clothes, and a poor man in shabby clothes also comes in. | SWKCV 2 Kwa maana kama akija mtu katika kusanyiko lenu akiwa amevaa pete ya dhahabu na mavazi mazuri, pia akaingia mtu maskini mwenye mavazi yaliyochakaa, |
| BSB 3 If you lavish attention on the man in fine clothes and say, “Here is a seat of honor,” but say to the poor man, “You must stand” or “Sit at my feet,” | SWKCV 3 nanyi mkampa heshima yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia, “Keti hapa mahali pazuri,” lakini yule maskini mkamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti hapa sakafuni karibu na miguu yangu,” |
| BSB 4 have you not discriminated among yourselves and become judges with evil thoughts? | SWKCV 4 je, hamjawabagua na kuwa mahakimu mioyoni mwenu mkihukumu kwa mawazo yenu maovu? |
| BSB 5 Listen, my beloved brothers: Has not God chosen the poor of this world to be rich in faith and to inherit the kingdom He promised those who love Him? | SWKCV 5 Ndugu zangu, sikilizeni: Je, Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi Ufalme aliowaahidi wale wampendao? |
| BSB 6 But you have dishonored the poor. Is it not the rich who oppress you and drag you into court? | SWKCV 6 Lakini ninyi mmemdharau yule aliye maskini. Je, hao matajiri si ndio wanaowadhulumu na kuwaburuta mahakamani? |
| BSB 7 Are they not the ones who blaspheme the noble name by which you have been called? | SWKCV 7 Je, si wao wanaolikufuru Jina lile lililo bora sana mliloitiwa? |
| BSB 8 If you really fulfill the royal law stated in Scripture, “Love your neighbor as yourself,” you are doing well. | SWKCV 8 Kama kweli mnaitimiza ile sheria ya kifalme inayopatikana katika Maandiko isemayo, “Mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako,” mnafanya vyema. |
| BSB 9 But if you show favoritism, you sin and are convicted by the law as transgressors. | SWKCV 9 Lakini kama mnakuwa na upendeleo kwa watu, mnatenda dhambi, na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji. |
| BSB 10 Whoever keeps the whole law but stumbles at just one point is guilty of breaking all of it. | SWKCV 10 Kwa maana mtu yeyote anayeishika sheria yote lakini akajikwaa katika kipengele kimoja tu, ana hatia ya kuivunja sheria yote. |
| BSB 11 For He who said, “Do not commit adultery,” also said, “Do not murder.” If you do not commit adultery, but do commit murder, you have become a lawbreaker. | SWKCV 11 Kwa sababu yeye aliyesema, “Usizini,” alisema pia, “Usiue.” Basi kama huzini lakini unaua, umekuwa mvunjaji wa sheria. |
| BSB 12 Speak and act as those who are going to be judged by the law that gives freedom. | SWKCV 12 Hivyo semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ile iletayo uhuru. |
| BSB 13 For judgment without mercy will be shown to anyone who has not been merciful. Mercy triumphs over judgment. | SWKCV 13 Kwa kuwa hukumu bila huruma itatolewa kwa mtu yeyote asiyekuwa na huruma. Huruma huishinda hukumu. |
| BSB 14 What good is it, my brothers, if someone claims to have faith, but has no deeds? Can such faith save him? | SWKCV 14 Ndugu zangu, yafaa nini ikiwa mtu atadai kuwa anayo imani lakini hana matendo? Je, imani kama hiyo yaweza kumwokoa? |
| BSB 15 Suppose a brother or sister is without clothes and daily food. | SWKCV 15 Ikiwa ndugu yako au dada hana mavazi wala chakula, |
| BSB 16 If one of you tells him, “Go in peace; stay warm and well fed,” but does not provide for his physical needs, what good is that? | SWKCV 16 mmoja wenu akamwambia, “Enenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba,” pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini? |
| BSB 17 So too, faith by itself, if it does not result in action, is dead. | SWKCV 17 Vivyo hivyo, imani peke yake kama haikuambatana na matendo, imekufa. |
| BSB 18 But someone will say, “You have faith and I have deeds.” Show me your faith without deeds, and I will show you my faith by my deeds. | SWKCV 18 Lakini mtu mwingine atasema, “Wewe unayo imani; mimi ninayo matendo.” Nionyeshe imani yako pasipo matendo nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo. |
| BSB 19 You believe that God is one. Good for you! Even the demons believe that—and shudder. | SWKCV 19 Unaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Vyema! Hata mashetani yanaamini hivyo na kutetemeka. |
| BSB 20 O foolish man, do you want evidence that faith without deeds is worthless? | SWKCV 20 Ewe mpumbavu! Je, wataka kujua kwamba imani bila matendo haifai kitu? |
| BSB 21 Was not our father Abraham justified by what he did when he offered his son Isaac on the altar? | SWKCV 21 Je, Abrahamu baba yetu hakuhesabiwa haki kwa kile alichotenda, alipomtoa mwanawe Isaki madhabahuni? |
| BSB 22 You see that his faith was working with his actions, and his faith was perfected by what he did. | SWKCV 22 Unaona jinsi ambavyo imani yake na matendo yake vilikuwa vinatenda kazi pamoja, nayo imani yake ikakamilishwa na kile alichotenda. |
| BSB 23 And the Scripture was fulfilled that says, “Abraham believed God, and it was credited to him as righteousness,” and he was called a friend of God. | SWKCV 23 Kwa njia hiyo yakatimizwa yale Maandiko yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki,” naye akaitwa rafiki wa Mungu. |
| BSB 24 As you can see, a man is justified by his deeds and not by faith alone. | SWKCV 24 Mnaona ya kwamba mtu huhesabiwa haki kwa yale anayotenda wala si kwa imani peke yake. |
| BSB 25 In the same way, was not even Rahab the prostitute justified by her actions when she welcomed the spies and sent them off on another route? | SWKCV 25 Vivyo hivyo, hata Rahabu, yule kahaba, hakuhesabiwa haki kwa yale aliyotenda alipowapokea wale wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine? |
| BSB 26 As the body without the spirit is dead, so faith without deeds is dead. | SWKCV 26 Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa. |
Questions about James 2? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.