Job 19
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then Job answered: | SWKCV 1 Ndipo Ayubu akajibu: |
| BSB 2 “How long will you torment me and crush me with your words? | SWKCV 2 “Je, mtaendelea kunitesa mpaka lini, na kuniponda kwa maneno yenu? |
| BSB 3 Ten times now you have reproached me; you shamelessly mistreat me. | SWKCV 3 Mara kumi hizi mmenishutumu; bila aibu mnanishambulia. |
| BSB 4 Even if I have truly gone astray, my error concerns me alone. | SWKCV 4 Kama ni kweli nimepotoka, kosa langu ninabaki kuhusika nalo mwenyewe. |
| BSB 5 If indeed you would exalt yourselves above me and use my disgrace against me, | SWKCV 5 Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu, na kutumia unyonge wangu dhidi yangu, |
| BSB 6 then understand that it is God who has wronged me and drawn His net around me. | SWKCV 6 basi jueni kuwa Mungu amenitendea yaliyo mabaya, naye amekokota wavu wake kunizunguka. |
| BSB 7 Though I cry out, ‘Violence!’ I get no response; though I call for help, there is no justice. | SWKCV 7 “Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu; ingawa ninaomba msaada, hakuna haki. |
| BSB 8 He has blocked my way so I cannot pass; He has veiled my paths with darkness. | SWKCV 8 Yeye ameizuia njia yangu hivyo siwezi kupita; ameyafunika mapito yangu na giza. |
| BSB 9 He has stripped me of my honor and removed the crown from my head. | SWKCV 9 Amenivua heshima yangu, na kuniondolea taji kichwani pangu. |
| BSB 10 He tears me down on every side until I am gone; He uproots my hope like a tree. | SWKCV 10 Amenibomoa kila upande hadi nimeisha; amelingʼoa tegemeo langu kama mti. |
| BSB 11 His anger burns against me, and He counts me among His enemies. | SWKCV 11 Hasira yake imewaka juu yangu; amenihesabu kuwa miongoni mwa adui zake. |
| BSB 12 His troops advance together; they construct a ramp against me and encamp around my tent. | SWKCV 12 Majeshi yake yananisogelea kwa nguvu; yamenizingira, yamepiga kambi kulizunguka hema langu. |
| BSB 13 He has removed my brothers from me; my acquaintances have abandoned me. | SWKCV 13 “Amewatenga ndugu zangu mbali nami; wale tunaojuana nao wamefarakana nami kabisa. |
| BSB 14 My kinsmen have failed me, and my friends have forgotten me. | SWKCV 14 Watu wa jamaa yangu wamekwenda mbali; rafiki zangu wamenisahau. |
| BSB 15 My guests and maidservants count me as a stranger; I am a foreigner in their sight. | SWKCV 15 Wageni wangu na watumishi wangu wa kike wananiona kama mgeni; wananitazama kama mgeni. |
| BSB 16 I call for my servant, but he does not answer, though I implore him with my own mouth. | SWKCV 16 Namwita mtumishi wangu, wala haitiki, ingawa namwomba kwa kinywa changu mwenyewe. |
| BSB 17 My breath is repulsive to my wife, and I am loathsome to my own family. | SWKCV 17 Pumzi ya kinywa changu ni kinyaa kwa mke wangu; nimekuwa chukizo mno kwa ndugu zangu mwenyewe. |
| BSB 18 Even little boys scorn me; when I appear, they deride me. | SWKCV 18 Hata watoto wadogo hunidhihaki; ninapojitokeza, hunifanyia mzaha. |
| BSB 19 All my best friends despise me, and those I love have turned against me. | SWKCV 19 Rafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa; wale niwapendao wamekuwa kinyume nami. |
| BSB 20 My skin and flesh cling to my bones; I have escaped by the skin of my teeth. | SWKCV 20 Mimi nimebaki mifupa na ngozi tu; nimeponea nikiwa karibu kufa. |
| BSB 21 Have pity on me, my friends, have pity, for the hand of God has struck me. | SWKCV 21 “Nihurumieni, rafiki zangu, kuweni na huruma, kwa kuwa mkono wa Mungu umenipiga. |
| BSB 22 Why do you persecute me as God does? Will you never get enough of my flesh? | SWKCV 22 Kwa nini mnanifuatia kama Mungu afanyavyo? Hamtosheki kamwe na mwili wangu? |
| BSB 23 I wish that my words were recorded and inscribed in a book, | SWKCV 23 “Laiti maneno yangu yangewekwa kwenye kumbukumbu, laiti kwamba yangeandikwa kwenye kitabu, |
| BSB 24 by an iron stylus on lead, or chiseled in stone forever. | SWKCV 24 kwamba yangechorwa kwenye risasi kwa kifaa cha chuma, au kuyachonga juu ya mwamba milele! |
| BSB 25 But I know that my Redeemer lives, and in the end He will stand upon the earth. | SWKCV 25 Ninajua kwamba Mkombozi wangu yu hai, naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi. |
| BSB 26 Even after my skin has been destroyed, yet in my flesh I will see God. | SWKCV 26 Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa, bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu; |
| BSB 27 I will see Him for myself; my eyes will behold Him, and not as a stranger. How my heart yearns within me! | SWKCV 27 mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe: mimi, wala si mwingine. Tazama jinsi moyo wangu unavyomtamani sana! |
| BSB 28 If you say, ‘Let us persecute him, since the root of the matter lies with him,’ | SWKCV 28 “Kama mkisema, ‘Tazama tutakavyomwinda, maadamu mzizi wa tatizo uko ndani yake,’ |
| BSB 29 then you should fear the sword yourselves, because wrath brings punishment by the sword, so that you may know there is a judgment.” | SWKCV 29 ninyi wenyewe uogopeni upanga, kwa kuwa ghadhabu italeta adhabu kwa upanga, nanyi ndipo mtakapojua kwamba kuna hukumu.” |
Questions about Job 19? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.