Job 28
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “Surely there is a mine for silver and a place where gold is refined. | SWKCV 1 “Kuna machimbo ya fedha, na mahali dhahabu isafishwapo. |
| BSB 2 Iron is taken from the earth, and copper is smelted from ore. | SWKCV 2 Chuma hupatikana ardhini, nayo shaba huyeyushwa kutoka mawe ya madini. |
| BSB 3 Man puts an end to the darkness; he probes the farthest recesses for ore in deepest darkness. | SWKCV 3 Mwanadamu hukomesha giza; huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali, kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini katika giza jeusi sana. |
| BSB 4 Far from human habitation he cuts a shaft in places forgotten by the foot of man. Far from men he dangles and sways. | SWKCV 4 Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu, mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu; mbali na wanadamu huningʼinia na kupembea kwa kamba. |
| BSB 5 Food may come from the earth, but from below it is transformed as by fire. | SWKCV 5 Ardhi, ambako chakula hutoka, chini hugeuzwa kwa moto; |
| BSB 6 Its rocks are the source of sapphires, containing flecks of gold. | SWKCV 6 yakuti samawi hutoka katika miamba yake, nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu. |
| BSB 7 No bird of prey knows that path; no falcon’s eye has seen it. | SWKCV 7 Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika, wala hakuna jicho la mwewe lililoiona. |
| BSB 8 Proud beasts have never trodden it; no lion has ever prowled over it. | SWKCV 8 Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga, wala simba azungukaye huko. |
| BSB 9 The miner strikes the flint; he overturns mountains at their base. | SWKCV 9 Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana, na kuiacha wazi mizizi ya milima. |
| BSB 10 He hews out channels in the rocks, and his eyes spot every treasure. | SWKCV 10 Hutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba; macho yake huona hazina zake zote. |
| BSB 11 He stops up the sources of the streams to bring what is hidden to light. | SWKCV 11 Hutafuta vyanzo vya mito na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru. |
| BSB 12 But where can wisdom be found, and where does understanding dwell? | SWKCV 12 “Lakini hekima inaweza kupatikana wapi? Ufahamu unakaa wapi? |
| BSB 13 No man can know its value, nor is it found in the land of the living. | SWKCV 13 Mwanadamu hatambui thamani yake; haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai. |
| BSB 14 The ocean depths say, ‘It is not in me,’ while the sea declares, ‘It is not with me.’ | SWKCV 14 Kilindi husema, ‘Haiko ndani yangu’; bahari nayo husema, ‘Haiko pamoja nami.’ |
| BSB 15 It cannot be bought with gold, nor can its price be weighed out in silver. | SWKCV 15 Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi kuliko zote, wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha. |
| BSB 16 It cannot be valued in the gold of Ophir, in precious onyx or sapphire. | SWKCV 16 Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri, kwa shohamu ya thamani kubwa au yakuti samawi ya thamani kubwa. |
| BSB 17 Neither gold nor crystal can compare to it, nor jewels of fine gold be exchanged for it. | SWKCV 17 Dhahabu wala mawe maangavu haviwezi kulinganishwa nayo, wala haiwezi hubadilishwa na vito vya dhahabu. |
| BSB 18 Coral and quartz are unworthy of mention; the price of wisdom is beyond rubies. | SWKCV 18 Marijani na yaspi hazistahili kutajwa; thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu. |
| BSB 19 Topaz from Cush cannot compare to it, nor can it be valued in pure gold. | SWKCV 19 Yakuti manjano ipatikanayo Kushi haiwezi kulinganishwa nayo, wala haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi. |
| BSB 20 From where, then, does wisdom come, and where does understanding dwell? | SWKCV 20 “Ni wapi basi hekima itokako? Ufahamu hukaa wapi? |
| BSB 21 It is hidden from the eyes of every living thing and concealed from the birds of the air. | SWKCV 21 Imefichika machoni pa kila kitu kilicho hai, imesitiriwa hata kwa ndege wa angani. |
| BSB 22 Abaddon and Death say, ‘We have heard a rumor about it.’ | SWKCV 22 Uharibifu na Mauti husema, ‘Ni uvumi wake tu uliotufikia masikioni mwetu.’ |
| BSB 23 But God understands its way, and He knows its place. | SWKCV 23 Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa, |
| BSB 24 For He looks to the ends of the earth and sees everything under the heavens. | SWKCV 24 kwa maana yeye huitazama miisho ya dunia na huona kila kitu chini ya mbingu. |
| BSB 25 When God fixed the weight of the wind and measured out the waters, | SWKCV 25 Alipofanyiza nguvu za upepo na kuyapima maji, |
| BSB 26 when He set a limit for the rain and a path for the thunderbolt, | SWKCV 26 alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua na njia kwa ajili ya umeme wa radi, |
| BSB 27 then He looked at wisdom and appraised it; He established it and searched it out. | SWKCV 27 ndipo alipoitazama hekima na kuikadiria thamani yake, akaithibitisha na kuihakikisha. |
| BSB 28 And He said to man, ‘Behold, the fear of the Lord, that is wisdom, and to turn away from evil is understanding.’” | SWKCV 28 Naye Mungu akamwambia mwanadamu, ‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima, nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’” |
Questions about Job 28? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.