Job 33
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “But now, O Job, hear my speech, and listen to all my words. | SWKCV 1 “Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu; zingatia kila kitu nitakachosema. |
| BSB 2 Behold, I will open my mouth; my address is on the tip of my tongue. | SWKCV 2 Karibu nitafungua kinywa changu; maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu. |
| BSB 3 My words are from an upright heart, and my lips speak sincerely what I know. | SWKCV 3 Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu; midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo. |
| BSB 4 The Spirit of God has made me, and the breath of the Almighty gives me life. | SWKCV 4 Roho wa Mungu ameniumba; pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai. |
| BSB 5 Refute me if you can; prepare your case and confront me. | SWKCV 5 Unijibu basi, kama unaweza; jiandae kunikabili mimi. |
| BSB 6 I am just like you before God; I was also formed from clay. | SWKCV 6 Mimi ni kama wewe mbele za Mungu; mimi pia nimetolewa kwenye udongo. |
| BSB 7 Surely no fear of me should terrify you; nor will my hand be heavy upon you. | SWKCV 7 Huna sababu ya kuniogopa, wala mkono wangu haupaswi kukulemea. |
| BSB 8 Surely you have spoken in my hearing, and I have heard these very words: | SWKCV 8 “Lakini umesema nikiwa ninakusikia, nami nilisikia maneno yenyewe: |
| BSB 9 ‘I am pure, without transgression; I am clean, with no iniquity in me. | SWKCV 9 ‘Mimi ni safi na sina dhambi; mimi ni safi na sina hatia. |
| BSB 10 Yet God finds occasions against me; He counts me as His enemy. | SWKCV 10 Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu, naye ananiona kama adui yake. |
| BSB 11 He puts my feet in the stocks; He watches over all my paths.’ | SWKCV 11 Ananifunga miguu kwa pingu, tena anaziangalia njia zangu zote kwa karibu.’ |
| BSB 12 Behold, you are not right in this matter. I will answer you, for God is greater than man. | SWKCV 12 “Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa, kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu. |
| BSB 13 Why do you complain to Him that He answers nothing a man asks? | SWKCV 13 Kwa nini unamlalamikia kwamba yeye hamjibu mwanadamu? |
| BSB 14 For God speaks in one way and in another, yet no one notices. | SWKCV 14 Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, au wakati mwingine kwa njia nyingine, ingawa mwanadamu anaweza asielewe. |
| BSB 15 In a dream, in a vision in the night, when deep sleep falls upon men as they slumber on their beds, | SWKCV 15 Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu wasinziapo vitandani mwao, |
| BSB 16 He opens their ears and terrifies them with warnings | SWKCV 16 anaweza akasemea masikioni mwao, na kuwatia hofu kwa maonyo, |
| BSB 17 to turn a man from wrongdoing and keep him from pride, | SWKCV 17 ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya na kumwepusha na kiburi, |
| BSB 18 to preserve his soul from the Pit and his life from perishing by the sword. | SWKCV 18 kuiokoa nafsi yake na shimo, uhai wake usiangamizwe kwa upanga. |
| BSB 19 A man is also chastened on his bed with pain and constant distress in his bones, | SWKCV 19 Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake, |
| BSB 20 so that he detests his bread, and his soul loathes his favorite food. | SWKCV 20 kiasi kwamba maisha yake yenyewe yanakataa chakula nayo nafsi yake ikakichukia kabisa hata chakula kizuri. |
| BSB 21 His flesh wastes away from sight, and his hidden bones protrude. | SWKCV 21 Nyama ya mwili wake huisha kwa kukonda, nayo mifupa yake ambayo mwanzoni ilikuwa imefichika, sasa inatokeza nje. |
| BSB 22 He draws near to the Pit, and his life to the messengers of death. | SWKCV 22 Nafsi yake inakaribia kaburi, nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo. |
| BSB 23 Yet if there is a messenger on his side, one mediator in a thousand, to tell a man what is right for him, | SWKCV 23 “Kama bado kuna malaika upande wake kama mtetezi, mmoja miongoni mwa elfu, wa kumwambia mwanadamu lililo jema kwake, |
| BSB 24 to be gracious to him and say, ‘Spare him from going down to the Pit; I have found his ransom,’ | SWKCV 24 kumwonea huruma na kusema, ‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni; nimepata ukombozi kwa ajili yake’: |
| BSB 25 then his flesh is refreshed like a child’s; he returns to the days of his youth. | SWKCV 25 ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto; hurudishwa upya kama siku za ujana wake. |
| BSB 26 He prays to God and finds favor; he sees God’s face and shouts for joy, and God restores His righteousness to that man. | SWKCV 26 Humwomba Mungu, akapata kibali kwake, huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha; Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu. |
| BSB 27 Then he sings before men with these words: ‘I have sinned and perverted what was right; yet I did not get what I deserved. | SWKCV 27 Ndipo huja mbele za watu na kusema, ‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki, lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili. |
| BSB 28 He redeemed my soul from going down to the Pit, and I will live to see the light.’ | SWKCV 28 Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni, nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’ |
| BSB 29 Behold, all these things God does to a man, two or even three times, | SWKCV 29 “Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu; mara mbili hata mara tatu, |
| BSB 30 to bring back his soul from the Pit, that he may be enlightened with the light of life. | SWKCV 30 ili aigeuze nafsi yake toka shimoni, ili nuru ya uzima imwangazie. |
| BSB 31 Pay attention, Job, and listen to me; be silent, and I will speak. | SWKCV 31 “Ayubu, zingatia, nisikilize mimi; nyamaza, nami nitanena. |
| BSB 32 But if you have something to say, answer me; speak up, for I would like to vindicate you. | SWKCV 32 Kama unalo lolote la kusema, unijibu; sema, kwa maana ninataka uonekane huna hatia. |
| BSB 33 But if not, then listen to me; be quiet, and I will teach you wisdom.” | SWKCV 33 Lakini kama huna la kusema, basi nisikilize mimi; nyamaza, nami nitakufundisha hekima.” |
Questions about Job 33? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.