Jonah 2
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 From inside the fish, Jonah prayed to the LORD his God, | SWKCV 1 Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwomba Bwana Mungu wake. |
| BSB 2 saying: “In my distress I called to the LORD, and He answered me. From the belly of Sheol I called for help, and You heard my voice. | SWKCV 2 Akasema: “Katika shida yangu nalimwita Bwana, naye akanijibu. Kutoka kina cha kaburi niliomba msaada, nawe ukasikiliza kilio changu. |
| BSB 3 For You cast me into the deep, into the heart of the seas, and the current swirled about me; all Your breakers and waves swept over me. | SWKCV 3 Ulinitupa kwenye kilindi, ndani kabisa ya moyo wa bahari, mikondo ya maji ilinizunguka, mawimbi yako yote na viwimbi vilipita juu yangu. |
| BSB 4 At this, I said, ‘I have been banished from Your sight; yet I will look once more toward Your holy temple.’ | SWKCV 4 Nikasema, ‘Nimefukuziwa mbali na uso wako, hata hivyo nitatazama tena kuelekea Hekalu lako takatifu.’ |
| BSB 5 The waters engulfed me to take my life; the watery depths closed around me; the seaweed wrapped around my head. | SWKCV 5 Maji yaliyonimeza yalinitisha, kilindi kilinizunguka; mwani ulijisokota kichwani pangu. |
| BSB 6 To the roots of the mountains I descended; the earth beneath me barred me in forever! But You raised my life from the pit, O LORD my God! | SWKCV 6 Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima, makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele. Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni, Ee Bwana Mungu wangu. |
| BSB 7 As my life was fading away, I remembered the LORD. My prayer went up to You, to Your holy temple. | SWKCV 7 “Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka, nilikukumbuka wewe, Bwana, nayo maombi yangu yalikufikia wewe, katika Hekalu lako takatifu. |
| BSB 8 Those who cling to worthless idols forsake His loving devotion. | SWKCV 8 “Wale watu wanaongʼangʼana na sanamu zisizofaa hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao. |
| BSB 9 But I, with the voice of thanksgiving, will sacrifice to You. I will fulfill what I have vowed. Salvation is from the LORD!” | SWKCV 9 Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani, nitakutolea dhabihu. Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza. Wokovu watoka kwa Bwana.” |
| BSB 10 And the LORD commanded the fish, and it vomited Jonah onto dry land. | SWKCV 10 Basi Bwana akamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu. |
Questions about Jonah 2? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.