Leviticus 3
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “If one’s offering is a peace offering and he offers an animal from the herd, whether male or female, he must present it without blemish before the LORD. | SWKCV 1 “ ‘Kama sadaka ya mtu ni sadaka ya amani, naye akatoa ngʼombe kutoka kundi, akiwa dume au jike, atamleta mnyama asiye na dosari mbele za Bwana. |
| BSB 2 He is to lay his hand on the head of the offering and slaughter it at the entrance to the Tent of Meeting. Then Aaron’s sons the priests shall splatter the blood on all sides of the altar. | SWKCV 2 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake na kumchinja penye ingilio la Hema la Kukutania. Ndipo makuhani wana wa Aroni watanyunyiza damu yake pande zote za madhabahu. |
| BSB 3 From the peace offering he is to bring a food offering to the LORD: the fat that covers the entrails, all the fat that is on them, | SWKCV 3 Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto: mafuta yote ya mnyama yafunikayo sehemu za ndani, ama yanayoungana na hizo sehemu za ndani, |
| BSB 4 both kidneys with the fat on them near the loins, and the lobe of the liver, which he is to remove with the kidneys. | SWKCV 4 figo zote pamoja na mafuta yote yanayozizunguka karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo. |
| BSB 5 Then Aaron’s sons are to burn it on the altar atop the burnt offering that is on the burning wood, as a food offering, a pleasing aroma to the LORD. | SWKCV 5 Kisha wana wa Aroni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni zinazowaka, kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. |
| BSB 6 If, however, one’s peace offering to the LORD is from the flock, he must present a male or female without blemish. | SWKCV 6 “ ‘Kama akitoa kondoo au mbuzi kutoka kundi kama sadaka ya amani kwa Bwana, atamtoa dume au jike asiye na dosari. |
| BSB 7 If he is presenting a lamb for his offering, he must present it before the LORD. | SWKCV 7 Kama akimtoa mwana-kondoo, atamleta mbele za Bwana. |
| BSB 8 He is to lay his hand on the head of his offering and slaughter it in front of the Tent of Meeting. Then Aaron’s sons shall splatter its blood on all sides of the altar. | SWKCV 8 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake, naye atamchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote. |
| BSB 9 And from the peace offering he shall bring a food offering to the LORD consisting of its fat: the entire fat tail cut off close to the backbone, the fat that covers the entrails, all the fat that is on them, | SWKCV 9 Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwa Bwana kwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo, |
| BSB 10 both kidneys with the fat on them near the loins, and the lobe of the liver, which he is to remove with the kidneys. | SWKCV 10 figo mbili pamoja na mafuta yanayozizunguka yaliyo karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayatoa pamoja na figo. |
| BSB 11 Then the priest is to burn them on the altar as food, a food offering to the LORD. | SWKCV 11 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. |
| BSB 12 If one’s offering is a goat, he is to present it before the LORD. | SWKCV 12 “ ‘Kama sadaka yake ni mbuzi, ataileta mbele za Bwana. |
| BSB 13 He must lay his hand on its head and slaughter it in front of the Tent of Meeting. Then Aaron’s sons shall splatter its blood on all sides of the altar. | SWKCV 13 Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote. |
| BSB 14 And from his offering he shall present a food offering to the LORD: the fat that covers the entrails, all the fat that is on them, | SWKCV 14 Kutokana na ile sadaka anayotoa, atatoa sadaka hii kwa Bwana kwa moto: mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani na yale yanayoungana nazo, |
| BSB 15 both kidneys with the fat on them near the loins, and the lobe of the liver, which he is to remove with the kidneys. | SWKCV 15 figo zote mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno na yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo. |
| BSB 16 Then the priest is to burn the food on the altar as a food offering, a pleasing aroma. All the fat is the LORD’s. | SWKCV 16 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri. Mafuta yote ya mnyama ni ya Bwana. |
| BSB 17 This is a permanent statute for the generations to come, wherever you live: You must not eat any fat or any blood.” | SWKCV 17 “ ‘Hii ni kanuni ya kudumu kwa vizazi vijavyo, popote muishipo: Msile mafuta yoyote ya mnyama wala damu.’” |
Questions about Leviticus 3? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.