Luke 14
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 One Sabbath, Jesus went to eat in the home of a leading Pharisee, and those in attendance were watching Him closely. | SWKCV 1 Ikawa siku moja Yesu alipokuwa amekwenda kula chakula kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo siku ya Sabato, watu walikuwa wakimchunguza kwa bidii. |
| BSB 2 Right there before Him was a man with dropsy. | SWKCV 2 Papo hapo mbele yake palikuwa na mtu mmoja mwenye ugonjwa wa kuvimba mwili. |
| BSB 3 So Jesus asked the experts in the law and the Pharisees, “Is it lawful to heal on the Sabbath or not?” | SWKCV 3 Yesu akawauliza wale Mafarisayo na walimu wa sheria, “Je, ni halali kuponya watu siku ya Sabato au la?” |
| BSB 4 But they remained silent. Then Jesus took hold of the man, healed him, and sent him on his way. | SWKCV 4 Wakakaa kimya. Hivyo Yesu akamshika yule mgonjwa mkono na kumponya, akamruhusu aende zake. |
| BSB 5 And He asked them, “Which of you whose son or ox falls into a pit on the Sabbath day will not immediately pull him out?” | SWKCV 5 Kisha akawauliza, “Kama mmoja wenu angekuwa na mtoto au ngʼombe wake aliyetumbukia katika kisima siku ya Sabato, je, hamtamvuta mara moja na kumtoa?” |
| BSB 6 And they were unable to answer these questions. | SWKCV 6 Nao hawakuwa na la kusema. |
| BSB 7 When Jesus noticed how the guests chose the places of honor, He told them a parable: | SWKCV 7 Alipoona jinsi wageni walivyokuwa wanachagua mahali pa heshima wakati wa kula, akawaambia mfano huu: |
| BSB 8 “When you are invited to a wedding banquet, do not sit in the place of honor, in case someone more distinguished than you has been invited. | SWKCV 8 “Mtu akikualika arusini, usikae mahali pa mgeni wa heshima kwa kuwa inawezekana amealikwa mtu mheshimiwa kuliko wewe. |
| BSB 9 Then the host who invited both of you will come and tell you, ‘Give this man your seat.’ And in humiliation, you will have to take the last place. | SWKCV 9 Kama mkifanya hivyo yule aliyewaalika ninyi wawili atakuja na kukuambia, ‘Mpishe huyu mtu kiti chako.’ Ndipo kwa aibu utalazimika kukaa katika nafasi ya chini kabisa. |
| BSB 10 But when you are invited, go and sit in the last place, so that your host will come and tell you, ‘Friend, move up to a better place.’ Then you will be honored in front of everyone at the table with you. | SWKCV 10 Badala yake, unapoalikwa, chagua nafasi ya chini, ili yule mwenyeji wako atakapokuona atakuja na kukuambia, ‘Rafiki yangu, nenda kwenye nafasi iliyo bora zaidi.’ Kwa jinsi hii utakuwa umepewa heshima mbele ya wageni wenzako wote. |
| BSB 11 For everyone who exalts himself will be humbled, and the one who humbles himself will be exalted.” | SWKCV 11 Kwa maana kila mtu ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa.” |
| BSB 12 Then Jesus said to the man who had invited Him, “When you host a dinner or a banquet, do not invite your friends or brothers or relatives or rich neighbors. Otherwise, they may invite you in return, and you will be repaid. | SWKCV 12 Kisha Yesu akamwambia yule aliyewaalika, “Uandaapo karamu ya chakula cha mchana au cha jioni, usialike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako walio matajiri tu. Ukifanya hivyo, wao nao wanaweza kukualika kwao, nawe ukawa umelipwa kile ulichofanya na kupata thawabu yako. |
| BSB 13 But when you host a banquet, invite the poor, the crippled, the lame, and the blind, | SWKCV 13 Bali ufanyapo karamu, waalike maskini, vilema na vipofu, |
| BSB 14 and you will be blessed. Since they cannot repay you, you will be repaid at the resurrection of the righteous.” | SWKCV 14 nawe utabarikiwa kwa sababu hawa hawana uwezo wa kukulipa. Mungu atakulipa wakati wa ufufuo wa wenye haki.” |
| BSB 15 When one of those reclining with Him heard this, he said to Jesus, “Blessed is everyone who will eat at the feast in the kingdom of God.” | SWKCV 15 Mmoja wa wale waliokuwa pamoja naye mezani aliposikia hivi akamwambia Yesu, “Amebarikiwa mtu yule atakayekula katika karamu ya Ufalme wa Mungu!” |
| BSB 16 But Jesus replied, “A certain man prepared a great banquet and invited many guests. | SWKCV 16 Yesu akamjibu, “Mtu mmoja alikuwa anaandaa karamu kubwa, akaalika watu wengi. |
| BSB 17 When it was time for the banquet, he sent his servant to tell those who had been invited, ‘Come, for everything is now ready.’ | SWKCV 17 Wakati wa karamu ulipofika, akamtuma mtumishi wake akawaambie wale walioalikwa, ‘Karibuni, kila kitu ki tayari sasa.’ |
| BSB 18 But one after another they all began to make excuses. The first one said, ‘I have bought a field, and I need to go see it. Please excuse me.’ | SWKCV 18 “Lakini wote, kila mmoja, wakaanza kutoa udhuru: Wa kwanza akasema, ‘Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’ |
| BSB 19 Another said, ‘I have bought five yoke of oxen, and I am going to try them out. Please excuse me.’ | SWKCV 19 “Mwingine akasema, ‘Ndipo tu nimenunua jozi tano za ngʼombe wa kulimia, nami ninakwenda kuwajaribu, tafadhali niwie radhi.’ |
| BSB 20 Still another said, ‘I have married a wife, so I cannot come.’ | SWKCV 20 Naye mwingine akasema, ‘Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.’ |
| BSB 21 The servant returned and reported all this to his master. Then the owner of the house became angry and said to his servant, ‘Go out quickly into the streets and alleys of the city, and bring in the poor, the crippled, the blind, and the lame.’ | SWKCV 21 “Yule mtumishi akarudi, akampa bwana wake taarifa. Ndipo yule mwenye nyumba akakasirika, akamwagiza yule mtumishi wake, akisema, ‘Nenda upesi kwenye mitaa na vichochoro vya mjini uwalete maskini, vilema, vipofu na viwete.’ |
| BSB 22 ‘Sir,’ the servant replied, ‘what you ordered has been done, and there is still room.’ | SWKCV 22 “Yule mtumishi akamwambia, ‘Bwana, yale uliyoniagiza nimefanya, lakini bado ipo nafasi.’ |
| BSB 23 So the master told his servant, ‘Go out to the highways and hedges and compel them to come in, so that my house will be full. | SWKCV 23 “Ndipo yule bwana akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda kwenye barabara na vijia vilivyoko nje ya mji na uwalazimishe watu waingie ili nyumba yangu ipate kujaa. |
| BSB 24 For I tell you, not one of those men who were invited will taste my banquet.’” | SWKCV 24 Kwa maana nawaambia, hakuna hata mmoja wa wale walioalikwa atakayeionja karamu yangu.’” |
| BSB 25 Now large crowds were traveling with Jesus, and He turned and said to them, | SWKCV 25 Umati mkubwa wa watu ulikuwa ukisafiri pamoja na Yesu, naye akageuka, akawaambia, |
| BSB 26 “If anyone comes to Me and does not hate his father and mother and wife and children and brothers and sisters—yes, even his own life—he cannot be My disciple. | SWKCV 26 “Mtu yeyote anayekuja kwangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto wake, ndugu zake na dada zake, naam, hata maisha yake mwenyewe. |
| BSB 27 And whoever does not carry his cross and follow Me cannot be My disciple. | SWKCV 27 Yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu. |
| BSB 28 Which of you, wishing to build a tower, does not first sit down and count the cost to see if he has the resources to complete it? | SWKCV 28 “Ni nani miongoni mwenu ambaye kama anataka kujenga nyumba, hakai kwanza chini na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha? |
| BSB 29 Otherwise, if he lays the foundation and is unable to finish the work, everyone who sees it will ridicule him, | SWKCV 29 La sivyo, akiisha kuweka msingi, naye akiwa hana uwezo wa kuikamilisha, wote waionao wataanza kumdhihaki, |
| BSB 30 saying, ‘This man could not finish what he started to build.’ | SWKCV 30 wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga lakini hakuweza kukamilisha.’ |
| BSB 31 Or what king on his way to war with another king will not first sit down and consider whether he can engage with ten thousand men the one coming against him with twenty thousand? | SWKCV 31 “Au ni mfalme gani atokaye kwenda kupigana vita na mfalme mwingine, ambaye hakai chini kwanza na kufikiri iwapo akiwa na jeshi la watu 10,000 ataweza kupigana na yule anayekuja na jeshi la watu 20,000? |
| BSB 32 And if he is unable, he will send a delegation while the other king is still far off, to ask for terms of peace. | SWKCV 32 Kama hawezi, basi wakati yule mwingine akiwa bado yuko mbali, yeye hutuma ujumbe wa watu na kuomba masharti ya amani. |
| BSB 33 In the same way, any one of you who does not give up everything he has cannot be My disciple. | SWKCV 33 Vivyo hivyo, yeyote miongoni mwenu ambaye hawezi kuacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. |
| BSB 34 Salt is good, but if the salt loses its savor, with what will it be seasoned? | SWKCV 34 “Chumvi ni nzuri, lakini chumvi ikiwa imepoteza ladha yake, itafanywaje ili iweze kukolea tena? |
| BSB 35 It is fit neither for the soil nor for the manure pile, and it is thrown out. He who has ears to hear, let him hear.” | SWKCV 35 Haifai ardhi wala kwa lundo la mbolea, bali hutupwa nje. “Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.” |
Questions about Luke 14? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.