Mark 14
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now the Passover and the Feast of Unleavened Bread were two days away, and the chief priests and scribes were looking for a covert way to arrest Jesus and kill Him. | SWKCV 1 Zilikuwa zimebaki siku mbili tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka, na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumkamata Yesu kwa hila na kumuua. |
| BSB 2 “But not during the feast,” they said, “or there may be a riot among the people.” | SWKCV 2 Lakini walisema, “Tusilifanye jambo hili wakati wa Sikukuu, maana watu wanaweza wakafanya ghasia.” |
| BSB 3 While Jesus was in Bethany reclining at the table in the home of Simon the Leper, a woman came with an alabaster jar of expensive perfume, made of pure nard. She broke open the jar and poured it on Jesus’ head. | SWKCV 3 Yesu alikuwa Bethania nyumbani kwa Simoni aliyekuwa na ukoma. Wakati alipokuwa ameketi mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akamiminia hayo manukato kichwani mwa Yesu. |
| BSB 4 Some of those present, however, expressed their indignation to one another: “Why this waste of perfume? | SWKCV 4 Baadhi ya watu waliokuwepo pale walikuwa wakisemezana wao kwa wao, “Upotevu huu wote ni wa nini? |
| BSB 5 It could have been sold for over three hundred denarii and the money given to the poor.” And they scolded her. | SWKCV 5 Mafuta haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari 300, na fedha hizo wakapewa maskini.” Wakamkemea vikali huyo mwanamke. |
| BSB 6 But Jesus said, “Leave her alone; why are you bothering her? She has done a beautiful deed to Me. | SWKCV 6 Lakini Yesu akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Mwacheni! Yeye amenitendea jambo zuri sana. |
| BSB 7 The poor you will always have with you, and you can help them whenever you want. But you will not always have Me. | SWKCV 7 Maskini mtakuwa nao siku zote na mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaotaka. Lakini mimi hamtakuwa nami siku zote. |
| BSB 8 She has done what she could to anoint My body in advance of My burial. | SWKCV 8 Huyu mwanamke amenitendea lile aliloweza. Ameumiminia mwili wangu manukato ili kuniandaa kwa maziko yangu. |
| BSB 9 And truly I tell you, wherever the gospel is preached in all the world, what she has done will also be told in memory of her.” | SWKCV 9 Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.” |
| BSB 10 Then Judas Iscariot, one of the Twelve, went to the chief priests to betray Jesus to them. | SWKCV 10 Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akaenda kwa viongozi wa makuhani ili kumsaliti Yesu kwao. |
| BSB 11 They were delighted to hear this, and they promised to give him money. So Judas began to look for an opportunity to betray Jesus. | SWKCV 11 Walifurahi sana kusikia jambo hili na wakaahidi kumpa fedha. Hivyo yeye akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti. |
| BSB 12 On the first day of the Feast of Unleavened Bread, when the Passover lamb was to be sacrificed, Jesus’ disciples asked Him, “Where do You want us to prepare for You to eat the Passover?” | SWKCV 12 Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo kwa desturi mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wa Yesu wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?” |
| BSB 13 So He sent two of His disciples and told them, “Go into the city, and a man carrying a jug of water will meet you. Follow him, | SWKCV 13 Basi akawatuma wawili miongoni mwa wanafunzi wake, akawaambia, “Nendeni mjini. Huko mtakutana na mwanaume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni. |
| BSB 14 and whichever house he enters, say to the owner, ‘The Teacher asks: Where is My guest room, where I may eat the Passover with My disciples?’ | SWKCV 14 Mwambieni mwenye nyumba ile atakayoingia, ‘Mwalimu anauliza: Kiko wapi chumba changu cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka?’ |
| BSB 15 And he will show you a large upper room, furnished and ready. Make preparations for us there.” | SWKCV 15 Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani, kilichopambwa tena kilicho tayari. Tuandalieni humo.” |
| BSB 16 So the disciples left and went into the city, where they found everything as Jesus had described. And they prepared the Passover. | SWKCV 16 Wale wanafunzi wakaondoka na kwenda mjini, nao wakakuta kila kitu kama Yesu alivyowaambia. Hivyo wakaiandaa Pasaka. |
| BSB 17 When evening came, Jesus arrived with the Twelve. | SWKCV 17 Ilipofika jioni, Yesu akaja pamoja na wale wanafunzi wake kumi na wawili. |
| BSB 18 And while they were reclining and eating, Jesus said, “Truly I tell you, one of you who is eating with Me will betray Me.” | SWKCV 18 Walipoketi mezani wakila, Yesu akawaambia, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti, mmoja anayekula pamoja nami.” |
| BSB 19 They began to be grieved and to ask Him one after another, “Surely not I?” | SWKCV 19 Wakaanza kuhuzunika na kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi Bwana?” |
| BSB 20 He answered, “It is one of the Twelve—the one who is dipping his hand into the bowl with Me. | SWKCV 20 Akawajibu, “Ni mmoja miongoni mwenu ninyi kumi na wawili, yule anayechovya mkate kwenye bakuli pamoja nami. |
| BSB 21 The Son of Man will go just as it is written about Him, but woe to that man by whom He is betrayed! It would be better for him if he had not been born.” | SWKCV 21 Mwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa.” |
| BSB 22 While they were eating, Jesus took bread, spoke a blessing and broke it, and gave it to the disciples, saying, “Take it; this is My body.” | SWKCV 22 Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni mle; huu ndio mwili wangu.” |
| BSB 23 Then He took the cup, gave thanks, and gave it to them, and they all drank from it. | SWKCV 23 Kisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, nao wote wakanywa kutoka humo. |
| BSB 24 He said to them, “This is My blood of the covenant, which is poured out for many. | SWKCV 24 Akawaambia, “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. |
| BSB 25 Truly I tell you, I will no longer drink of the fruit of the vine until that day when I drink it anew in the kingdom of God.” | SWKCV 25 Amin, nawaambia, sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya katika Ufalme wa Mungu.” |
| BSB 26 And when they had sung a hymn, they went out to the Mount of Olives. | SWKCV 26 Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni. |
| BSB 27 Then Jesus said to them, “You will all fall away, for it is written: ‘I will strike the Shepherd, and the sheep will be scattered.’ | SWKCV 27 Yesu akawaambia, “Ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa: “ ‘Nitampiga mchungaji, nao kondoo watatawanyika.’ |
| BSB 28 But after I have risen, I will go ahead of you into Galilee.” | SWKCV 28 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.” |
| BSB 29 Peter declared, “Even if all fall away, I never will.” | SWKCV 29 Petro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.” |
| BSB 30 “Truly I tell you,” Jesus replied, “this very night, before the rooster crows twice, you will deny Me three times.” | SWKCV 30 Yesu akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, wewe mwenyewe utanikana mara tatu.” |
| BSB 31 But Peter kept insisting, “Even if I have to die with You, I will never deny You.” And all the others said the same thing. | SWKCV 31 Lakini Petro akasisitiza zaidi, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wale wengine wote wakasema vivyo hivyo. |
| BSB 32 Then they came to a place called Gethsemane, and Jesus told His disciples, “Sit here while I pray.” | SWKCV 32 Wakaenda mahali paitwapo Gethsemane. Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa, nami niende nikaombe.” |
| BSB 33 He took with Him Peter, James, and John, and began to be deeply troubled and distressed. | SWKCV 33 Kisha akawachukua pamoja naye Petro, Yakobo na Yohana. Akaanza kuhuzunika sana na kutaabika. |
| BSB 34 Then He said to them, “My soul is consumed with sorrow to the point of death. Stay here and keep watch.” | SWKCV 34 Akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe.” |
| BSB 35 Going a little farther, He fell to the ground and prayed that, if it were possible, the hour would pass from Him. | SWKCV 35 Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba kwamba kama ingewezekana saa hiyo ya mateso imwondokee. |
| BSB 36 “Abba, Father,” He said, “all things are possible for You. Take this cup from Me. Yet not what I will, but what You will.” | SWKCV 36 Akasema, “Abba, Baba, mambo yote yawezekana kwako. Niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo mimi, bali vile upendavyo wewe.” |
| BSB 37 Then Jesus returned and found them sleeping. “Simon, are you asleep?” He asked. “Were you not able to keep watch for one hour? | SWKCV 37 Akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, “Simoni, umelala? Je, hukuweza kukesha hata kwa saa moja? |
| BSB 38 Watch and pray so that you will not enter into temptation. For the spirit is willing, but the body is weak.” | SWKCV 38 Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu.” |
| BSB 39 Again He went away and prayed, saying the same thing. | SWKCV 39 Akaenda tena kuomba, akisema maneno yale yale. |
| BSB 40 And again Jesus returned and found them sleeping, for their eyes were heavy. And they did not know what to answer Him. | SWKCV 40 Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. Nao hawakujua la kumwambia. |
| BSB 41 When Jesus returned the third time, He said, “Are you still sleeping and resting? That is enough! The hour has come. Look, the Son of Man is betrayed into the hands of sinners. | SWKCV 41 Akaja mara ya tatu, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imewadia. Tazameni, Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi. |
| BSB 42 Rise, let us go. See, My betrayer is approaching!” | SWKCV 42 Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!” |
| BSB 43 While Jesus was still speaking, Judas, one of the Twelve, arrived, accompanied by a crowd armed with swords and clubs, sent from the chief priests, scribes, and elders. | SWKCV 43 Yesu alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili, akatokea. Alikuwa amefuatana na umati wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, na wazee. |
| BSB 44 Now the betrayer had arranged a signal with them: “The One I kiss is the man; arrest Him and lead Him away securely.” | SWKCV 44 Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni, mkamchukue chini ya ulinzi.” |
| BSB 45 Going directly to Jesus, he said, “Rabbi!” and kissed Him. | SWKCV 45 Mara Yuda akamjia Yesu na kusema, “Rabi.” Akambusu. |
| BSB 46 Then the men seized Jesus and arrested Him. | SWKCV 46 Wale watu wakamkamata Yesu, wakamweka chini ya ulinzi. |
| BSB 47 And one of the bystanders drew his sword and struck the servant of the high priest, cutting off his ear. | SWKCV 47 Ndipo mmoja wa wale waliokuwa wamesimama karibu aliuchomoa upanga wake na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. |
| BSB 48 Jesus asked the crowd, “Have you come out with swords and clubs to arrest Me as you would an outlaw? | SWKCV 48 Kisha Yesu akawaambia, “Mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyangʼanyi? |
| BSB 49 Every day I was with you, teaching in the temple courts, and you did not arrest Me. But this has happened that the Scriptures would be fulfilled.” | SWKCV 49 Siku kwa siku nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni, wala hamkunikamata. Lakini Maandiko sharti yatimie.” |
| BSB 50 Then everyone deserted Him and fled. | SWKCV 50 Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia. |
| BSB 51 One young man who had been following Jesus was wearing a linen cloth around his body. They caught hold of him, | SWKCV 51 Kijana mmoja, ambaye hakuwa amevaa kitu isipokuwa alijitanda nguo ya kitani, alikuwa akimfuata Yesu. Walipomkamata, |
| BSB 52 but he pulled free of the linen cloth and ran away naked. | SWKCV 52 alikimbia uchi, akaliacha vazi lake. |
| BSB 53 They led Jesus away to the high priest, and all the chief priests, elders, and scribes assembled. | SWKCV 53 Wakampeleka Yesu kwa kuhani mkuu, nao viongozi wa makuhani wote, na wazee na walimu wa sheria wote wakakusanyika pamoja. |
| BSB 54 Peter followed Him at a distance, right into the courtyard of the high priest. And he sat with the officers and warmed himself by the fire. | SWKCV 54 Petro akamfuata kwa mbali, hadi uani kwa kuhani mkuu. Huko akaketi pamoja na walinzi, akiota moto. |
| BSB 55 Now the chief priests and the whole Sanhedrin were seeking testimony against Jesus to put Him to death, but they did not find any. | SWKCV 55 Viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi lote wakatafuta ushahidi dhidi ya Yesu ili wapate kumuua. Lakini hawakupata jambo lolote. |
| BSB 56 For many bore false witness against Jesus, but their testimony was inconsistent. | SWKCV 56 Wengi walitoa ushahidi wa uongo dhidi yake, lakini maelezo yao hayakukubaliana. |
| BSB 57 Then some men stood up and testified falsely against Him: | SWKCV 57 Ndipo wengine wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo dhidi yake, wakisema: |
| BSB 58 “We heard Him say, ‘I will destroy this man-made temple, and in three days I will build another that is made without hands.’” | SWKCV 58 “Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitalibomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga jingine ambalo halikujengwa na wanadamu.’” |
| BSB 59 But even their testimony was inconsistent. | SWKCV 59 Lakini hata hivyo, ushahidi wao haukukubaliana. |
| BSB 60 So the high priest stood up before them and questioned Jesus, “Have You no answer? What are these men testifying against You?” | SWKCV 60 Basi kuhani mkuu akasimama mbele yao, akamuuliza Yesu, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?” |
| BSB 61 But Jesus remained silent and made no reply. Again the high priest questioned Him, “Are You the Christ, the Son of the Blessed One?” | SWKCV 61 Lakini Yesu akakaa kimya, hakusema neno lolote. Kuhani mkuu akamuuliza tena, “Je, wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu Aliyebarikiwa?” |
| BSB 62 “I am,” said Jesus, “and you will see the Son of Man sitting at the right hand of Power and coming with the clouds of heaven.” | SWKCV 62 Yesu akajibu, “Mimi ndimi. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.” |
| BSB 63 At this, the high priest tore his clothes and declared, “Why do we need any more witnesses? | SWKCV 63 Kuhani mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? |
| BSB 64 You have heard the blasphemy. What is your verdict?” And they all condemned Him as deserving of death. | SWKCV 64 Ninyi mmesikia hayo makufuru. Uamuzi wenu ni gani?” Wote wakamhukumu kwamba anastahili kifo. |
| BSB 65 Then some of them began to spit on Him. They blindfolded Him, struck Him with their fists, and said to Him, “Prophesy!” And the officers received Him with slaps in His face. | SWKCV 65 Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa machoni, wakampiga kwa ngumi na kumwambia, “Tabiri!” Walinzi wakamchukua na kumpiga makofi. |
| BSB 66 While Peter was in the courtyard below, one of the servant girls of the high priest came down | SWKCV 66 Petro alipokuwa bado yuko chini kwenye ua wa jumba la kifalme, tazama akaja mmoja wa watumishi wa kike wa kuhani mkuu. |
| BSB 67 and saw him warming himself there. She looked at Peter and said, “You also were with Jesus the Nazarene.” | SWKCV 67 Alipomwona Petro akiota moto, akamtazama sana, akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu, Mnazareti.” |
| BSB 68 But he denied it. “I do not know or even understand what you are talking about,” he said. Then he went out to the gateway, and the rooster crowed. | SWKCV 68 Lakini Petro akakana, akasema, “Sijui wala sielewi unalosema.” Naye akaondoka kuelekea kwenye njia ya kuingilia. |
| BSB 69 There the servant girl saw him and again said to those standing nearby, “This man is one of them.” | SWKCV 69 Yule mtumishi wa kike alipomwona mahali pale, akawaambia tena wale waliokuwa wamesimama hapo, “Huyu mtu ni mmoja wao.” |
| BSB 70 But he denied it again. After a little while, those standing nearby said once more to Peter, “Surely you are one of them, for you too are a Galilean.” | SWKCV 70 Lakini Petro akakana tena. Baada ya muda kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo karibu na Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!” |
| BSB 71 But he began to curse and swear, “I do not know this man of whom you speak!” | SWKCV 71 Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, “Mimi simjui huyu mtu mnayesema habari zake!” |
| BSB 72 And immediately the rooster crowed a second time. Then Peter remembered the word that Jesus had spoken to him: “Before the rooster crows twice, you will deny Me three times.” And he broke down and wept. | SWKCV 72 Papo hapo jogoo akawika mara ya pili. Ndipo Petro akakumbuka lile neno Yesu alikuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akavunjika moyo, akalia sana. |
Questions about Mark 14? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.