Mark 8
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 In those days the crowd once again became very large, and they had nothing to eat. Jesus called the disciples to Him and said, | SWKCV 1 Katika siku hizo, umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena. Kwa kuwa walikuwa hawana chakula, Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, |
| BSB 2 “I have compassion for this crowd, because they have already been with Me three days and have nothing to eat. | SWKCV 2 “Ninauhurumia huu umati wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu na hawana chakula. |
| BSB 3 If I send them home hungry, they will faint along the way. For some of them have come a great distance.” | SWKCV 3 Nikiwaaga waende nyumbani bila kula, watazimia njiani kwa sababu baadhi yao wametoka mbali.” |
| BSB 4 His disciples replied, “Where in this desolate place could anyone find enough bread to feed all these people?” | SWKCV 4 Wanafunzi wake wakamjibu, “Lakini hapa nyikani tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha?” |
| BSB 5 “How many loaves do you have?” Jesus asked. “Seven,” they replied. | SWKCV 5 Yesu akawauliza, “Mna mikate mingapi?” Wakajibu, “Tuna mikate saba.” |
| BSB 6 And He instructed the crowd to sit down on the ground. Then He took the seven loaves, gave thanks and broke them, and gave them to His disciples to set before the people. And they distributed them to the crowd. | SWKCV 6 Akawaambia watu waketi chini. Akiisha kuichukua mikate saba na kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi wake ili wawagawie watu. Wanafunzi wake wakafanya hivyo. |
| BSB 7 They also had a few small fish, and Jesus blessed them and ordered that these be set before them as well. | SWKCV 7 Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu. |
| BSB 8 The people ate and were satisfied, and the disciples picked up seven basketfuls of broken pieces that were left over. | SWKCV 8 Wale watu walikula na kutosheka. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. |
| BSB 9 And about four thousand men were present. And when Jesus had dismissed the crowd, | SWKCV 9 Watu waliokula walikuwa wapata 4,000. Akiisha kuwaaga, |
| BSB 10 He immediately got into the boat with His disciples and went to the district of Dalmanutha. | SWKCV 10 aliingia kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake, akaenda sehemu za Dalmanutha. |
| BSB 11 Then the Pharisees came and began to argue with Jesus, testing Him by demanding from Him a sign from heaven. | SWKCV 11 Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Yesu. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni. |
| BSB 12 Jesus sighed deeply in His spirit and said, “Why does this generation demand a sign? Truly I tell you, no sign will be given to this generation.” | SWKCV 12 Akahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Amin nawaambieni, hakitapewa ishara yoyote.” |
| BSB 13 And He left them, got back into the boat, and crossed to the other side. | SWKCV 13 Kisha akawaacha, akarudi kwenye mashua, akavuka hadi ngʼambo. |
| BSB 14 Now the disciples had forgotten to take bread, except for one loaf they had with them in the boat. | SWKCV 14 Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua. |
| BSB 15 “Watch out!” He cautioned them. “Beware of the leaven of the Pharisees and of Herod.” | SWKCV 15 Yesu akawaonya: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.” |
| BSB 16 So they began to discuss with one another the fact that they had no bread. | SWKCV 16 Wakajadiliana wao kwa wao, na kusema, “Anasema hivi kwa sababu hatukuleta mikate.” |
| BSB 17 Aware of their conversation, Jesus asked them, “Why are you debating about having no bread? Do you still not see or understand? Do you have such hard hearts? | SWKCV 17 Yesu, akifahamu majadiliano yao, akawauliza: “Mbona mnajadiliana kuhusu kutokuwa na mikate? Je, bado hamtambui wala hamwelewi? Je, mbona mioyo yenu ni migumu kiasi hicho? |
| BSB 18 ‘Having eyes, do you not see? And having ears, do you not hear?’ And do you not remember? | SWKCV 18 Je, mna macho lakini mnashindwa kuona, na mna masikio lakini mnashindwa kusikia? Je, hamkumbuki? |
| BSB 19 When I broke the five loaves for the five thousand, how many basketfuls of broken pieces did you collect?” “Twelve,” they answered. | SWKCV 19 Nilipoimega ile mikate mitano kuwalisha watu 5,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?” Wakamjibu, “Kumi na viwili.” |
| BSB 20 “And when I broke the seven loaves for the four thousand, how many basketfuls of broken pieces did you collect?” “Seven,” they said. | SWKCV 20 “Je, nilipoimega ile mikate saba kuwalisha watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?” Wakamjibu, “Saba.” |
| BSB 21 Then He asked them, “Do you still not understand?” | SWKCV 21 Ndipo akawauliza, “Je, bado hamwelewi?” |
| BSB 22 When they arrived at Bethsaida, some people brought a blind man and begged Jesus to touch him. | SWKCV 22 Wakafika Bethsaida na baadhi ya watu wakamleta mtu mmoja kipofu wakamsihi Yesu amguse. |
| BSB 23 So He took the blind man by the hand and led him out of the village. Then He spit on the man’s eyes and placed His hands on him. “Can you see anything?” He asked. | SWKCV 23 Yesu akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Yesu akamuuliza, “Unaona chochote?” |
| BSB 24 The man looked up and said, “I can see the people, but they look like trees walking around.” | SWKCV 24 Yule kipofu akaangalia, akasema, “Ninaona watu, wanaonekana kama miti inayotembea.” |
| BSB 25 Once again Jesus placed His hands on the man’s eyes, and when he opened them his sight was restored, and he could see everything clearly. | SWKCV 25 Yesu akamwekea tena mikono machoni. Kisha macho yake yakafunguka, kuona kwake kukarejea naye akaona kila kitu dhahiri. |
| BSB 26 Jesus sent him home and said, “Do not go back into the village.” | SWKCV 26 Yesu akamuaga aende nyumbani kwake, akimwambia, “Hata kijijini usiingie.” |
| BSB 27 Then Jesus and His disciples went on to the villages around Caesarea Philippi. On the way, He questioned His disciples: “Who do people say I am?” | SWKCV 27 Yesu na wanafunzi wake wakaondoka kwenda katika vijiji vya Kaisaria-Filipi. Walipokuwa njiani, Yesu akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?” |
| BSB 28 They replied, “Some say John the Baptist; others say Elijah; and still others, one of the prophets.” | SWKCV 28 Wakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya, na bado wengine husema wewe ni mmojawapo wa manabii.” |
| BSB 29 “But what about you?” Jesus asked. “Who do you say I am?” Peter answered, “You are the Christ.” | SWKCV 29 Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?” Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo.” |
| BSB 30 And Jesus warned them not to tell anyone about Him. | SWKCV 30 Yesu akawaonya wasimwambie mtu yeyote habari zake. |
| BSB 31 Then He began to teach them that the Son of Man must suffer many things and be rejected by the elders, chief priests, and scribes, and that He must be killed and after three days rise again. | SWKCV 31 Ndipo akaanza kuwafundisha wanafunzi wake kuwa Mwana wa Adamu lazima atapata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na kwamba itampasa auawe lakini baada ya siku tatu afufuke. |
| BSB 32 He spoke this message quite frankly, and Peter took Him aside and began to rebuke Him. | SWKCV 32 Aliyasema haya waziwazi, ndipo Petro akamchukua kando na akaanza kumkemea. |
| BSB 33 But Jesus, turning and looking at His disciples, rebuked Peter and said, “Get behind Me, Satan! For you do not have in mind the things of God, but the things of men.” | SWKCV 33 Lakini Yesu alipogeuka na kuwaangalia wanafunzi wake, akamkemea Petro. Akasema, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.” |
| BSB 34 Then Jesus called the crowd to Him along with His disciples, and He told them, “If anyone wants to come after Me, he must deny himself and take up his cross and follow Me. | SWKCV 34 Ndipo akauita ule umati wa watu pamoja na wanafunzi wake, akasema, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. |
| BSB 35 For whoever wants to save his life will lose it, but whoever loses his life for My sake and for the gospel will save it. | SWKCV 35 Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili atayaokoa. |
| BSB 36 What does it profit a man to gain the whole world, yet forfeit his soul? | SWKCV 36 Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? |
| BSB 37 Or what can a man give in exchange for his soul? | SWKCV 37 Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? |
| BSB 38 If anyone is ashamed of Me and My words in this adulterous and sinful generation, the Son of Man will also be ashamed of him when He comes in His Father’s glory with the holy angels.” | SWKCV 38 Mtu yeyote akinionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.” |
Questions about Mark 8? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.