Mark 9
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then Jesus said to them, “Truly I tell you, there are some standing here who will not taste death before they see the kingdom of God arrive with power.” | SWKCV 1 Yesu akaendelea kuwaambia, “Amin, nawaambia, kuna watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.” |
| BSB 2 After six days Jesus took with Him Peter, James, and John, and led them up a high mountain by themselves. There He was transfigured before them. | SWKCV 2 Baada ya siku sita, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. |
| BSB 3 His clothes became radiantly white, brighter than any launderer on earth could bleach them. | SWKCV 3 Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. |
| BSB 4 And Elijah and Moses appeared before them, talking with Jesus. | SWKCV 4 Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu. |
| BSB 5 Peter said to Jesus, “Rabbi, it is good for us to be here. Let us put up three shelters—one for You, one for Moses, and one for Elijah.” | SWKCV 5 Petro akamwambia Yesu, “Rabi, ni vyema sisi tukae hapa. Turuhusu tujenge vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Mose na kingine cha Eliya.” |
| BSB 6 For they were all so terrified that Peter did not know what else to say. | SWKCV 6 Petro hakujua aseme nini kwa maana yeye na wenzake walikuwa wameogopa sana. |
| BSB 7 Then a cloud appeared and enveloped them, and a voice came from the cloud: “This is My beloved Son. Listen to Him!” | SWKCV 7 Ndipo pakatokea wingu, likawafunika, nayo sauti kutoka lile wingu ikasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Msikieni yeye.” |
| BSB 8 Suddenly, when they looked around, they saw no one with them except Jesus. | SWKCV 8 Mara walipotazama huku na huku, hawakuona tena mtu mwingine yeyote pamoja nao isipokuwa Yesu. |
| BSB 9 As they were coming down the mountain, Jesus admonished them not to tell anyone what they had seen until the Son of Man had risen from the dead. | SWKCV 9 Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Yesu akawakataza wasimwambie mtu yeyote mambo waliyoona, mpaka Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka kutoka kwa wafu. |
| BSB 10 So they kept this matter to themselves, discussing what it meant to rise from the dead. | SWKCV 10 Wakalihifadhi jambo hilo wao wenyewe, lakini wakawa wanajiuliza, “Huku kufufuka kwa wafu maana yake nini?” |
| BSB 11 And they asked Jesus, “Why do the scribes say that Elijah must come first?” | SWKCV 11 Wakamuuliza, “Kwa nini walimu wa sheria husema kwamba ni lazima Eliya aje kwanza?” |
| BSB 12 He replied, “Elijah does indeed come first, and he restores all things. Why then is it written that the Son of Man must suffer many things and be rejected? | SWKCV 12 Yesu akawajibu, “Ni kweli, Eliya yuaja kwanza ili kutengeneza mambo yote. Mbona basi imeandikwa kwamba Mwana wa Adamu ni lazima ateseke sana na kudharauliwa? |
| BSB 13 But I tell you that Elijah has indeed come, and they have done to him whatever they wished, just as it is written about him.” | SWKCV 13 Lakini ninawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtendea walivyopenda, kama ilivyoandikwa kumhusu yeye.” |
| BSB 14 When they returned to the other disciples, they saw a large crowd around them, and scribes arguing with them. | SWKCV 14 Walipowafikia wale wanafunzi wengine, wakawakuta wamezungukwa na umati mkubwa wa watu na baadhi ya walimu wa sheria wakibishana nao. |
| BSB 15 As soon as all the people saw Jesus, they were filled with awe and ran to greet Him. | SWKCV 15 Mara wale watu walipomwona Yesu, wakastaajabu sana, wakamkimbilia ili kumsalimu. |
| BSB 16 “What are you disputing with them?” He asked. | SWKCV 16 Akawauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nao kuhusu nini?” |
| BSB 17 Someone in the crowd replied, “Teacher, I brought You my son, who has a spirit that makes him mute. | SWKCV 17 Mtu mmoja miongoni mwa ule umati wa watu akajibu, “Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea. |
| BSB 18 Whenever it seizes him, it throws him to the ground. He foams at the mouth, gnashes his teeth, and becomes rigid. I asked Your disciples to drive it out, but they were unable.” | SWKCV 18 Kila mara huyo pepo mchafu ampagaapo mwanangu, humwangusha chini na kumfanya atokwe povu mdomoni na kusaga meno, kisha mwili wake hukauka. Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza.” |
| BSB 19 “O unbelieving generation!” Jesus replied. “How long must I remain with you? How long must I put up with you? Bring the boy to Me.” | SWKCV 19 Yesu akawaambia, “Enyi kizazi kisicho na imani! Nitakuwa pamoja nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni mvulana kwangu.” |
| BSB 20 So they brought him, and seeing Jesus, the spirit immediately threw the boy into a convulsion. He fell to the ground and rolled around, foaming at the mouth. | SWKCV 20 Nao wakamleta yule mvulana. Yule pepo mchafu alipomwona Yesu, mara akamtia yule mvulana kifafa, akaanguka, akagaagaa chini huku akitokwa na povu kinywani. |
| BSB 21 Jesus asked the boy’s father, “How long has this been with him?” “From childhood,” he said. | SWKCV 21 Yesu akamuuliza baba yake, “Mwanao amekuwa katika hali hii tangu lini?” Akamjibu, “Tangu utoto wake. |
| BSB 22 “It often throws him into the fire or into the water, trying to kill him. But if You can do anything, have compassion on us and help us.” | SWKCV 22 Mara kwa mara huyo pepo mchafu amekuwa akimwangusha kwenye moto au kwenye maji ili kumwangamiza. Lakini kama unaweza kufanya jambo lolote, tafadhali tuhurumie utusaidie.” |
| BSB 23 “If You can?” echoed Jesus. “All things are possible to him who believes!” | SWKCV 23 Yesu akamwambia, “Kama ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye.” |
| BSB 24 Immediately the boy’s father cried out, “I do believe; help my unbelief!” | SWKCV 24 Mara baba yake yule mvulana akapiga kelele akisema, “Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!” |
| BSB 25 When Jesus saw that a crowd had come running, He rebuked the unclean spirit. “You deaf and mute spirit,” He said, “I command you to come out and never enter him again.” | SWKCV 25 Yesu alipoona kwamba umati wa watu unakusanyika pamoja mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akimwambia, “Wewe pepo bubu na kiziwi, nakuamuru umtoke, wala usimwingie tena!” |
| BSB 26 After shrieking and convulsing him violently, the spirit came out. The boy became like a corpse, so that many said, “He is dead.” | SWKCV 26 Yule pepo mchafu akiisha kupiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu, na akamtoka. Yule mvulana alikuwa kama maiti, hivyo watu wengi wakasema, “Amekufa.” |
| BSB 27 But Jesus took him by the hand and helped him to his feet, and he stood up. | SWKCV 27 Lakini Yesu akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama. |
| BSB 28 After Jesus had gone into the house, His disciples asked Him privately, “Why couldn’t we drive it out?” | SWKCV 28 Baada ya Yesu kuingia ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamuuliza wakiwa peke yao, “Mbona sisi hatukuweza kumtoa huyo pepo mchafu?” |
| BSB 29 Jesus answered, “This kind cannot come out, except by prayer.” | SWKCV 29 Yesu akawajibu, “Hali hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa kuomba na kufunga.” |
| BSB 30 Going on from there, they passed through Galilee. But Jesus did not want anyone to know, | SWKCV 30 Wakaondoka huko, wakapitia Galilaya. Yesu hakutaka mtu yeyote afahamu mahali walipo, |
| BSB 31 because He was teaching His disciples. He told them, “The Son of Man will be delivered into the hands of men. They will kill Him, and after three days He will rise.” | SWKCV 31 kwa maana alikuwa anawafundisha wanafunzi wake. Akawaambia, “Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu. Nao watamuua, lakini siku tatu baada ya kuuawa atafufuka.” |
| BSB 32 But they did not understand this statement, and they were afraid to ask Him about it. | SWKCV 32 Lakini wao hawakuelewa kile alimaanisha, nao waliogopa kumuuliza maana yake. |
| BSB 33 Then they came to Capernaum. While Jesus was in the house, He asked them, “What were you discussing on the way?” | SWKCV 33 Basi wakafika Kapernaumu na baada ya kuingia nyumbani akawauliza, “Mlikuwa mnabishana nini kule njiani?” |
| BSB 34 But they were silent, for on the way they had been arguing about which of them was the greatest. | SWKCV 34 Lakini hawakumjibu, kwa sababu njiani walikuwa wakibishana kuhusu nani miongoni mwao alikuwa mkuu zaidi ya wote. |
| BSB 35 Sitting down, Jesus called the Twelve and said, “If anyone wants to be first, he must be the last of all and the servant of all.” | SWKCV 35 Akaketi chini, akawaita wote kumi na wawili, akawaambia: “Kama mtu yeyote akitaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa wa mwisho na mtumishi wa wote.” |
| BSB 36 Then He had a little child stand among them. Taking the child in His arms, He said to them, | SWKCV 36 Kisha akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha katikati yao. Akamkumbatia, akawaambia, |
| BSB 37 “Whoever welcomes one of these little children in My name welcomes Me, and whoever welcomes Me welcomes not only Me, but the One who sent Me.” | SWKCV 37 “Mtu yeyote amkaribishaye mmoja wa hawa watoto wadogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi. Naye anikaribishaye mimi, amkaribisha Baba yangu aliyenituma.” |
| BSB 38 John said to Him, “Teacher, we saw someone else driving out demons in Your name, and we tried to stop him, because he does not accompany us.” | SWKCV 38 Yohana akamwambia, “Mwalimu, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamkataza, kwa sababu yeye si mmoja wetu.” |
| BSB 39 “Do not stop him,” Jesus replied. “For no one who performs a miracle in My name can turn around and speak evil of Me. | SWKCV 39 Yesu akasema, “Msimkataze, kwa kuwa hakuna yeyote atendaye miujiza kwa Jina langu ambaye baada ya kitambo kidogo aweza kunena lolote baya dhidi yangu. |
| BSB 40 For whoever is not against us is for us. | SWKCV 40 Kwa maana yeyote asiye kinyume chetu, yuko upande wetu. |
| BSB 41 Indeed, if anyone gives you even a cup of water because you bear the name of Christ, truly I tell you, he will never lose his reward. | SWKCV 41 Amin, nawaambia, yeyote awapaye ninyi kikombe cha maji kwa Jina langu kwa sababu ninyi ni mali ya Kristo, hakika hataikosa thawabu yake.” |
| BSB 42 But if anyone causes one of these little ones who believe in Me to stumble, it would be better for him to have a large millstone hung around his neck and to be thrown into the sea. | SWKCV 42 “Kama mtu yeyote akimsababisha mmojawapo wa wadogo hawa wanaoniamini kutenda dhambi, ingekuwa bora kwake afungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake, na kutoswa baharini. |
| BSB 43 If your hand causes you to sin, cut it off. It is better for you to enter life crippled than to have two hands and go into hell, into the unquenchable fire. | SWKCV 43 Kama mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili lakini ukaingia jehanamu, mahali ambako moto hauzimiki. [ |
| BSB | SWKCV 44 Mahali ambako funza wake hawafi wala moto wake hauzimiki.] |
| BSB 45 If your foot causes you to sin, cut it off. It is better for you to enter life lame than to have two feet and be thrown into hell. | SWKCV 45 Kama mguu wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili lakini ukaingia jehanamu. [ |
| BSB | SWKCV 46 Mahali ambako funza wake hawafi wala moto hauzimiki.] |
| BSB 47 And if your eye causes you to sin, pluck it out. It is better for you to enter the kingdom of God with one eye than to have two eyes and be thrown into hell, | SWKCV 47 Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe. Ni afadhali kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa jehanamu, |
| BSB 48 where ‘their worm never dies, and the fire is never quenched.’ | SWKCV 48 mahali ambako “ ‘funza wake hawafi, wala moto wake hauzimiki.’ |
| BSB 49 For everyone will be salted with fire. | SWKCV 49 Kila mmoja atatiwa chumvi kwa moto. |
| BSB 50 Salt is good, but if the salt loses its saltiness, with what will you season it? Have salt among yourselves, and be at peace with one another.” | SWKCV 50 “Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake utaifanyaje ili iweze kukolea tena? Mwe na chumvi ndani yenu, mkaishi kwa amani, kila mmoja na mwenzake.” |
Questions about Mark 9? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.