Matthew 12
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 At that time Jesus went through the grainfields on the Sabbath. His disciples were hungry and began to pick the heads of grain and eat them. | SWKCV 1 Wakati huo Yesu alipitia kwenye mashamba ya nafaka siku ya Sabato. Wanafunzi wake walikuwa na njaa, nao wakaanza kuvunja masuke ya nafaka na kuyala. |
| BSB 2 When the Pharisees saw this, they said to Him, “Look, Your disciples are doing what is unlawful on the Sabbath.” | SWKCV 2 Lakini Mafarisayo walipoona jambo hili, wakamwambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato.” |
| BSB 3 Jesus replied, “Have you not read what David did when he and his companions were hungry? | SWKCV 3 Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma alichofanya Daudi na wenzake walipokuwa na njaa? |
| BSB 4 He entered the house of God, and he and his companions ate the consecrated bread, which was not lawful for them to eat, but only for the priests. | SWKCV 4 Aliingia katika nyumba ya Mungu, akala mikate iliyowekwa wakfu, yeye na wenzake, jambo ambalo halikuwa halali kwao kufanya, isipokuwa makuhani peke yao. |
| BSB 5 Or haven’t you read in the Law that on the Sabbath the priests in the temple break the Sabbath and yet are innocent? | SWKCV 5 Au hamjasoma katika Sheria kwamba siku ya Sabato makuhani huvunja sheria ya Sabato Hekaluni lakini hawahesabiwi kuwa na hatia? |
| BSB 6 But I tell you that One greater than the temple is here. | SWKCV 6 Nawaambia wazi kwamba, yeye aliye mkuu kuliko Hekalu yupo hapa. |
| BSB 7 If only you had known the meaning of ‘I desire mercy, not sacrifice,’ you would not have condemned the innocent. | SWKCV 7 Kama mngekuwa mmejua maana ya maneno haya, ‘Nataka rehema, wala si dhabihu,’ msingewalaumu watu wasio na hatia, |
| BSB 8 For the Son of Man is Lord of the Sabbath.” | SWKCV 8 kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” |
| BSB 9 Moving on from there, Jesus entered their synagogue, | SWKCV 9 Yesu akaondoka mahali hapo, akaingia ndani ya sinagogi lao, |
| BSB 10 and a man with a withered hand was there. In order to accuse Jesus, they asked Him, “Is it lawful to heal on the Sabbath?” | SWKCV 10 na huko alikuwepo mtu aliyepooza mkono. Wakitafuta sababu ya kumshtaki Yesu, wakamuuliza, “Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?” |
| BSB 11 He replied, “If one of you has a sheep and it falls into a pit on the Sabbath, will he not take hold of it and lift it out? | SWKCV 11 Yesu akawaambia, “Ni nani miongoni mwenu, mwenye kondoo wake ambaye huyo kondoo akitumbukia shimoni siku ya Sabato hatamtoa? |
| BSB 12 How much more valuable is a man than a sheep! Therefore it is lawful to do good on the Sabbath.” | SWKCV 12 Mtu ana thamani kubwa kuliko kondoo. Kwa hiyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato.” |
| BSB 13 Then Jesus said to the man, “Stretch out your hand.” So he stretched it out, and it was restored to full use, just like the other. | SWKCV 13 Ndipo akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukaponywa ukawa mzima kama ule mwingine. |
| BSB 14 But the Pharisees went out and plotted how they might kill Jesus. | SWKCV 14 Lakini Mafarisayo wakatoka nje, wakafanya shauri baya juu ya Yesu jinsi watakavyoweza kumuua. |
| BSB 15 Aware of this, Jesus withdrew from that place. Large crowds followed Him, and He healed them all, | SWKCV 15 Lakini Yesu alipoyatambua mawazo yao, akaondoka mahali hapo. Watu wengi wakamfuata, naye akawaponya wagonjwa wao wote, |
| BSB 16 warning them not to make Him known. | SWKCV 16 akiwakataza wasiseme yeye ni nani. |
| BSB 17 This was to fulfill what was spoken through the prophet Isaiah: | SWKCV 17 Hii ilikuwa ili litimie lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kusema: |
| BSB 18 “Here is My Servant, whom I have chosen, My beloved, in whom My soul delights. I will put My Spirit on Him, and He will proclaim justice to the nations. | SWKCV 18 “Tazama mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Nitaweka Roho wangu juu yake, naye atatangaza haki kwa mataifa. |
| BSB 19 He will not quarrel or cry out; no one will hear His voice in the streets. | SWKCV 19 Hatagombana wala hatapiga kelele, wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani. |
| BSB 20 A bruised reed He will not break, and a smoldering wick He will not extinguish, till He leads justice to victory. | SWKCV 20 Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya haki ishinde. |
| BSB 21 In His name the nations will put their hope.” | SWKCV 21 Katika Jina lake mataifa wataweka tumaini lao.” |
| BSB 22 Then a demon-possessed man who was blind and mute was brought to Jesus, and He healed the man so that he could speak and see. | SWKCV 22 Kisha wakamletea mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, na alikuwa kipofu na bubu. Yesu akamponya, hata akaweza kusema na kuona. |
| BSB 23 The crowds were astounded and asked, “Could this be the Son of David?” | SWKCV 23 Watu wote wakashangaa na kusema, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi?” |
| BSB 24 But when the Pharisees heard this, they said, “Only by Beelzebul, the prince of demons, does this man drive out demons.” | SWKCV 24 Lakini Mafarisayo waliposikia jambo hili wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli, mkuu wa pepo wachafu.” |
| BSB 25 Knowing their thoughts, Jesus said to them, “Every kingdom divided against itself will be laid waste, and every city or household divided against itself will not stand. | SWKCV 25 Yesu alijua walichokuwa wakiwaza, hivyo akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Hali kadhalika kila mji au watu wa nyumba moja waliogawanyika dhidi yao wenyewe hawawezi kusimama. |
| BSB 26 If Satan drives out Satan, he is divided against himself. How then can his kingdom stand? | SWKCV 26 Kama Shetani akimtoa Shetani, atakuwa amegawanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utawezaje kusimama? |
| BSB 27 And if I drive out demons by Beelzebul, by whom do your sons drive them out? So then, they will be your judges. | SWKCV 27 Nami kama natoa pepo wachafu kwa nguvu za Beelzebuli, watu wenu je, wao hutoa pepo wachafu kwa uwezo wa nani? Hivyo basi, wao ndio watakaowahukumu. |
| BSB 28 But if I drive out demons by the Spirit of God, then the kingdom of God has come upon you. | SWKCV 28 Lakini kama mimi ninatoa pepo wachafu kwa Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekuja juu yenu. |
| BSB 29 Or again, how can anyone enter a strong man’s house and steal his possessions, unless he first ties up the strong man? Then he can plunder his house. | SWKCV 29 “Au tena, mtu awezaje kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Akishamfunga, ndipo hakika anaweza kuteka nyara mali zake. |
| BSB 30 He who is not with Me is against Me, and he who does not gather with Me scatters. | SWKCV 30 “Mtu asiyekuwa pamoja nami yu kinyume nami, na mtu ambaye hakusanyi pamoja nami, hutawanya. |
| BSB 31 Therefore I tell you, every sin and blasphemy will be forgiven men, but the blasphemy against the Spirit will not be forgiven. | SWKCV 31 Kwa hiyo nawaambia, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, lakini mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. |
| BSB 32 Whoever speaks a word against the Son of Man will be forgiven, but whoever speaks against the Holy Spirit will not be forgiven, either in this age or in the one to come. | SWKCV 32 Mtu yeyote atakayesema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini yeyote anenaye neno dhidi ya Roho Mtakatifu hatasamehewa, iwe katika ulimwengu huu au katika ulimwengu ujao. |
| BSB 33 Make a tree good and its fruit will be good, or make a tree bad and its fruit will be bad, for a tree is known by its fruit. | SWKCV 33 “Ufanye mti kuwa mzuri, nayo matunda yake yatakuwa mazuri. Au ufanye mti kuwa mbaya, na matunda yake yatakuwa mabaya. Kwa maana mti hutambulika kwa matunda yake. |
| BSB 34 You brood of vipers, how can you who are evil say anything good? For out of the overflow of the heart the mouth speaks. | SWKCV 34 Enyi uzao wa nyoka! Mnawezaje kunena mambo mema, wakati ninyi ni waovu? Kwa maana kinywa cha mtu huyanena yale yaliyoujaza moyo wake. |
| BSB 35 The good man brings good things out of his good store of treasure, and the evil man brings evil things out of his evil store of treasure. | SWKCV 35 Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka hazina ya mambo mema yaliyohifadhiwa ndani yake, naye mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutoka hazina ya mambo maovu yaliyohifadhiwa ndani yake. |
| BSB 36 But I tell you that men will give an account on the day of judgment for every careless word they have spoken. | SWKCV 36 Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu kuhusu kila neno lisilo maana walilonena. |
| BSB 37 For by your words you will be acquitted, and by your words you will be condemned.” | SWKCV 37 Kwa maana kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.” |
| BSB 38 Then some of the scribes and Pharisees said to Him, “Teacher, we want to see a sign from You.” | SWKCV 38 Kisha baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria wakamwambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” |
| BSB 39 Jesus replied, “A wicked and adulterous generation demands a sign, but none will be given it except the sign of the prophet Jonah. | SWKCV 39 Lakini yeye akawajibu, “Kizazi kiovu na cha uzinzi kinaomba ishara! Lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya nabii Yona. |
| BSB 40 For as Jonah was three days and three nights in the belly of the great fish, so the Son of Man will be three days and three nights in the heart of the earth. | SWKCV 40 Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la nyangumi kwa siku tatu, usiku na mchana, vivyo hivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika moyo wa nchi siku tatu, usiku na mchana. |
| BSB 41 The men of Nineveh will stand at the judgment with this generation and condemn it; for they repented at the preaching of Jonah, and now One greater than Jonah is here. | SWKCV 41 Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu waliposikia mahubiri ya Yona. Na tazama, hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona. |
| BSB 42 The Queen of the South will rise at the judgment with this generation and condemn it; for she came from the ends of the earth to hear the wisdom of Solomon, and now One greater than Solomon is here. | SWKCV 42 Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kukihukumu kizazi hiki. Kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Solomoni. Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Solomoni.” |
| BSB 43 When an unclean spirit comes out of a man, it passes through arid places seeking rest and does not find it. | SWKCV 43 “Pepo mchafu amtokapo mtu, hutangatanga katika sehemu zisizo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini hapati. |
| BSB 44 Then it says, ‘I will return to the house I left.’ On its return, it finds the house vacant, swept clean, and put in order. | SWKCV 44 Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu nilikotoka.’ Naye arudipo huikuta ile nyumba ikiwa tupu, imefagiliwa na kupangwa vizuri. |
| BSB 45 Then it goes and brings with it seven other spirits more wicked than itself, and they go in and dwell there. And the final plight of that man is worse than the first. So will it be with this wicked generation.” | SWKCV 45 Kisha huenda na kuwaleta pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya kuliko ile ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kiovu.” |
| BSB 46 While Jesus was still speaking to the crowds, His mother and brothers stood outside, wanting to speak to Him. | SWKCV 46 Wakati alikuwa angali anazungumza na makutano, mama yake na ndugu zake wakasimama nje wakitaka kuongea naye. |
| BSB 47 Someone told Him, “Look, Your mother and brothers are standing outside, wanting to speak to You.” | SWKCV 47 Ndipo mtu mmoja akamwambia, “Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kuongea na wewe.” |
| BSB 48 But Jesus replied, “Who is My mother, and who are My brothers?” | SWKCV 48 Lakini yeye akamjibu na kumwambia yule mtu, “Mama yangu ni nani, nao ndugu zangu ni nani?” |
| BSB 49 Pointing to His disciples, He said, “Here are My mother and My brothers. | SWKCV 49 Akawanyooshea mkono wanafunzi wake, akasema, “Hawa hapa ndio mama yangu na ndugu zangu! |
| BSB 50 For whoever does the will of My Father in heaven is My brother and sister and mother.” | SWKCV 50 Kwa maana yeyote afanyaye mapenzi ya Baba yangu wa mbinguni, huyo ndiye ndugu yangu, na dada yangu na mama yangu.” |
Questions about Matthew 12? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.