Numbers 26
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 After the plague had ended, the LORD said to Moses and Eleazar son of Aaron the priest, | SWKCV 1 Baada ya hiyo tauni, Bwana akamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni, |
| BSB 2 “Take a census of the whole congregation of Israel by the houses of their fathers—all those twenty years of age or older who can serve in the army of Israel.” | SWKCV 2 “Hesabu jumuiya yote ya Kiisraeli kwa jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao wanaweza kutumika katika jeshi la Israeli.” |
| BSB 3 So on the plains of Moab by the Jordan, across from Jericho, Moses and Eleazar the priest issued the instruction, | SWKCV 3 Hivyo Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ngʼambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema, |
| BSB 4 “Take a census of the men twenty years of age or older, as the LORD has commanded Moses.” And these were the Israelites who came out of the land of Egypt: | SWKCV 4 “Hesabuni wanaume wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama Bwana alivyomwagiza Mose.” Hawa ndio Waisraeli waliotoka Misri: |
| BSB 5 Reuben was the firstborn of Israel. These were the descendants of Reuben: The Hanochite clan from Hanoch, the Palluite clan from Pallu, | SWKCV 5 Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa: kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki; kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu; |
| BSB 6 the Hezronite clan from Hezron, and the Carmite clan from Carmi. | SWKCV 6 kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni; kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi. |
| BSB 7 These were the clans of Reuben, and their registration numbered 43,730. | SWKCV 7 Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730. |
| BSB 8 Now the son of Pallu was Eliab, | SWKCV 8 Mwana wa Palu alikuwa Eliabu, |
| BSB 9 and the sons of Eliab were Nemuel, Dathan, and Abiram. It was Dathan and Abiram, chosen by the congregation, who rebelled against Moses and Aaron with the followers of Korah who rebelled against the LORD. | SWKCV 9 nao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Mose na Aroni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walimwasi Bwana. |
| BSB 10 And the earth opened its mouth and swallowed them along with Korah, whose followers died when the fire consumed 250 men. They serve as a warning sign. | SWKCV 10 Ardhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume 250. Nao walikuwa kama alama ya onyo. |
| BSB 11 However, the line of Korah did not die out. | SWKCV 11 Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa. |
| BSB 12 These were the descendants of Simeon by their clans: The Nemuelite clan from Nemuel, the Jaminite clan from Jamin, the Jachinite clan from Jachin, | SWKCV 12 Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli; kutoka kwa Yamini, ukoo wa Wayamini; kutoka wa Yakini, ukoo wa Wayakini; |
| BSB 13 the Zerahite clan from Zerah, and the Shaulite clan from Shaul. | SWKCV 13 kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera; kutoka kwa Shauli, ukoo wa Washauli. |
| BSB 14 These were the clans of Simeon, and there were 22,200 men. | SWKCV 14 Hizi ndizo koo za Simeoni; walikuwa 22,200. |
| BSB 15 These were the descendants of Gad by their clans: The Zephonite clan from Zephon, the Haggite clan from Haggi, the Shunite clan from Shuni, | SWKCV 15 Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Sifoni, ukoo wa Wasifoni; kutoka kwa Hagi, ukoo wa Wahagi; kutoka kwa Shuni, ukoo wa Washuni; |
| BSB 16 the Oznite clan from Ozni, the Erite clan from Eri, | SWKCV 16 kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni; kutoka kwa Eri, ukoo wa Waeri; |
| BSB 17 the Arodite clan from Arod, and the Arelite clan from Areli. | SWKCV 17 kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi; kutoka kwa Areli, ukoo wa Waareli. |
| BSB 18 These were the clans of Gad, and their registration numbered 40,500. | SWKCV 18 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa 40,500. |
| BSB 19 The sons of Judah were Er and Onan, but they died in the land of Canaan. | SWKCV 19 Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani. |
| BSB 20 These were the descendants of Judah by their clans: The Shelanite clan from Shelah, the Perezite clan from Perez, and the Zerahite clan from Zerah. | SWKCV 20 Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Shela, ukoo wa Washela; kutoka kwa Peresi, ukoo wa Waperesi; kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera. |
| BSB 21 And these were the descendants of Perez: the Hezronite clan from Hezron and the Hamulite clan from Hamul. | SWKCV 21 Wazao wa Peresi walikuwa: kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni; kutoka kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli. |
| BSB 22 These were the clans of Judah, and their registration numbered 76,500. | SWKCV 22 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda; wale waliohesabiwa walikuwa 76,500. |
| BSB 23 These were the descendants of Issachar by their clans: The Tolaite clan from Tola, the Punite clan from Puvah, | SWKCV 23 Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Tola, ukoo wa Watola; kutoka kwa Puva, ukoo wa Wapuva; |
| BSB 24 the Jashubite clan from Jashub, and the Shimronite clan from Shimron. | SWKCV 24 kutoka kwa Yashubu, ukoo wa Wayashubu; kutoka kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni. |
| BSB 25 These were the clans of Issachar, and their registration numbered 64,300. | SWKCV 25 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Isakari; wale waliohesabiwa walikuwa 64,300. |
| BSB 26 These were the descendants of Zebulun by their clans: The Seredite clan from Sered, the Elonite clan from Elon, and the Jahleelite clan from Jahleel. | SWKCV 26 Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Seredi, ukoo wa Waseredi; kutoka kwa Eloni, ukoo wa Waeloni; kutoka kwa Yaleeli, ukoo wa Wayaleeli. |
| BSB 27 These were the clans of Zebulun, and their registration numbered 60,500. | SWKCV 27 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Zabuloni, wale waliohesabiwa walikuwa 60,500. |
| BSB 28 The descendants of Joseph included the clans of Manasseh and Ephraim. | SWKCV 28 Wazao wa Yosefu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa: |
| BSB 29 These were the descendants of Manasseh: The Machirite clan from Machir, the father of Gilead, and the Gileadite clan from Gilead. | SWKCV 29 Wazao wa Manase: kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi); kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi. |
| BSB 30 These were the descendants of Gilead: the Iezerite clan from Iezer, the Helekite clan from Helek, | SWKCV 30 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Gileadi: kutoka kwa Iezeri, ukoo wa Waiezeri; kutoka kwa Heleki, ukoo wa Waheleki; |
| BSB 31 the Asrielite clan from Asriel, the Shechemite clan from Shechem, | SWKCV 31 kutoka kwa Asirieli, ukoo wa Waasirieli; kutoka kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu; |
| BSB 32 the Shemidaite clan from Shemida, and the Hepherite clan from Hepher. | SWKCV 32 kutoka kwa Shemida, ukoo wa Washemida; kutoka kwa Heferi, ukoo wa Waheferi. |
| BSB 33 Now Zelophehad son of Hepher had no sons but only daughters. The names of his daughters were Mahlah, Noah, Hoglah, Milcah, and Tirzah. | SWKCV 33 (Selofehadi mwana wa Heferi hakuzaa wana, bali alikuwa na watoto wa kike tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.) |
| BSB 34 These were the clans of Manasseh, and their registration numbered 52,700. | SWKCV 34 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Manase; wale waliohesabiwa walikuwa 52,700. |
| BSB 35 These were the descendants of Ephraim by their clans: The Shuthelahite clan from Shuthelah, the Becherite clan from Becher, and the Tahanite clan from Tahan. | SWKCV 35 Hawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao: kutoka kwa Shuthela, ukoo wa Washuthela; kutoka kwa Bekeri, ukoo wa Wabekeri; kutoka kwa Tahani, ukoo wa Watahani; |
| BSB 36 And the descendants of Shuthelah were the Eranite clan from Eran. | SWKCV 36 Hawa ndio walikuwa wazao wa Shuthela: kutoka kwa Erani, ukoo wa Waerani. |
| BSB 37 These were the clans of Ephraim, and their registration numbered 32,500. These clans were the descendants of Joseph. | SWKCV 37 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa 32,500. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yosefu kwa koo zao. |
| BSB 38 These were the descendants of Benjamin by their clans: The Belaite clan from Bela, the Ashbelite clan from Ashbel, the Ahiramite clan from Ahiram, | SWKCV 38 Wazao wa Benyamini kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Bela, ukoo wa Wabela; kutoka kwa Ashbeli, ukoo wa Waashbeli; kutoka kwa Ahiramu, ukoo wa Waahiramu; |
| BSB 39 the Shuphamite clan from Shupham, and the Huphamite clan from Hupham. | SWKCV 39 kutoka kwa Shufamu, ukoo wa Washufamu; kutoka kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu. |
| BSB 40 And the descendants of Bela from Ard and Naaman were the Ardite clan from Ard and the Naamite clan from Naaman. | SWKCV 40 Wazao wa Bela kutoka kwa Ardi na Naamani walikuwa: kutoka kwa Ardi, ukoo wa Waardi; kutoka kwa Naamani, ukoo wa Wanaamani. |
| BSB 41 These were the clans of Benjamin, and their registration numbered 45,600. | SWKCV 41 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Benyamini; wale waliohesabiwa walikuwa 45,600. |
| BSB 42 These were the descendants of Dan by their clans: The Shuhamite clan from Shuham. These were the clans of Dan. | SWKCV 42 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Dani kwa koo zao: kutoka kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Dani: |
| BSB 43 All of them were Shuhamite clans, and their registration numbered 64,400. | SWKCV 43 Wote walikuwa koo za Washuhamu; wale waliohesabiwa walikuwa 64,400. |
| BSB 44 These were the descendants of Asher by their clans: The Imnite clan from Imnah, the Ishvite clan from Ishvi, and the Beriite clan from Beriah. | SWKCV 44 Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Imna, ukoo wa Waimna; kutoka kwa Ishvi, ukoo wa Waishvi; kutoka kwa Beria, ukoo wa Waberia; |
| BSB 45 And these were the descendants of Beriah: the Heberite clan from Heber and the Malchielite clan from Malchiel. | SWKCV 45 kutoka kwa wazao wa Beria: kutoka kwa Heberi, ukoo wa Waheberi; kutoka kwa Malkieli, ukoo wa Wamalkieli. |
| BSB 46 And the name of Asher’s daughter was Serah. | SWKCV 46 (Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.) |
| BSB 47 These were the clans of Asher, and their registration numbered 53,400. | SWKCV 47 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa 53,400. |
| BSB 48 These were the descendants of Naphtali by their clans: The Jahzeelite clan from Jahzeel, the Gunite clan from Guni, | SWKCV 48 Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Yaseeli, ukoo wa Wayaseeli; kutoka kwa Guni, ukoo wa Waguni; |
| BSB 49 the Jezerite clan from Jezer, and the Shillemite clan from Shillem. | SWKCV 49 kutoka kwa Yeseri, ukoo wa Wayeseri; kutoka kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu. |
| BSB 50 These were the clans of Naphtali, and their registration numbered 45,400. | SWKCV 50 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Naftali; wale waliohesabiwa walikuwa 45,400. |
| BSB 51 These men of Israel numbered 601,730 in all. | SWKCV 51 Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa 601,730. |
| BSB 52 Then the LORD said to Moses, | SWKCV 52 Bwana akamwambia Mose, |
| BSB 53 “The land is to be divided among the tribes as an inheritance, according to the number of names. | SWKCV 53 “Watagawiwa nchi kama urithi kwa kulingana na hesabu ya majina. |
| BSB 54 Increase the inheritance for a large tribe and decrease it for a small one; each tribe is to receive its inheritance according to the number of those registered. | SWKCV 54 Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa. |
| BSB 55 Indeed, the land must be divided by lot; they shall receive their inheritance according to the names of the tribes of their fathers. | SWKCV 55 Hakikisha kuwa nchi inagawanywa kwa kura. Kile kitakachorithiwa na kila kikundi kitakuwa kwa kulingana na majina ya kabila la babu yao. |
| BSB 56 Each inheritance is to be divided by lot among the larger and smaller tribes.” | SWKCV 56 Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.” |
| BSB 57 Now these were the Levites numbered by their clans: The Gershonite clan from Gershon, the Kohathite clan from Kohath, and the Merarite clan from Merari. | SWKCV 57 Hawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao: kutoka kwa Gershoni, ukoo wa Wagershoni; kutoka kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi; kutoka kwa Merari, ukoo wa Wamerari. |
| BSB 58 These were the families of the Levites: The Libnite clan, the Hebronite clan, the Mahlite clan, the Mushite clan, and the Korahite clan. Now Kohath was the father of Amram, | SWKCV 58 Hizi pia zilikuwa koo za Walawi: ukoo wa Walibni; ukoo wa Wahebroni; ukoo wa Wamahli; ukoo wa Wamushi; ukoo wa wana wa Kora. (Kohathi alikuwa baba aliyemzaa Amramu; |
| BSB 59 and Amram’s wife was named Jochebed. She was also a daughter of Levi, born to Levi in Egypt. To Amram she bore Aaron, Moses, and their sister Miriam. | SWKCV 59 jina la mke wa Amramu ni Yokebedi, naye pia alikuwa mzao wa Lawi, ambaye alizaliwa kwa Walawi nchini Misri. Alimzalia Amramu: Aroni, Mose na dada yao Miriamu. |
| BSB 60 Nadab, Abihu, Eleazar, and Ithamar were born to Aaron, | SWKCV 60 Aroni alikuwa baba yake Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari. |
| BSB 61 but Nadab and Abihu died when they offered unauthorized fire before the LORD. | SWKCV 61 Lakini Nadabu na Abihu walikufa wakati walitoa sadaka mbele za Bwana kwa moto usioruhusiwa.) |
| BSB 62 The registration of the Levites totaled 23,000, every male a month old or more; they were not numbered among the other Israelites, because no inheritance was given to them among the Israelites. | SWKCV 62 Wanaume wote wa Walawi wa umri wa mwezi mmoja na zaidi walikuwa 23,000. Wao hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu hawakupokea urithi miongoni mwao. |
| BSB 63 These were the ones numbered by Moses and Eleazar the priest when they counted the Israelites on the plains of Moab by the Jordan, across from Jericho. | SWKCV 63 Hawa ndio walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko. |
| BSB 64 Among all these, however, there was not one who had been numbered by Moses and Aaron the priest when they counted the Israelites in the Wilderness of Sinai. | SWKCV 64 Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa miongoni mwa wale waliohesabiwa na Mose na kuhani Aroni wakati waliwahesabu Waisraeli katika Jangwa la Sinai. |
| BSB 65 For the LORD had told them that they would surely die in the wilderness. Not one was left except Caleb son of Jephunneh and Joshua son of Nun. | SWKCV 65 Kwa maana Bwana alikuwa amewaambia hao Waisraeli hakika wangekufa huko jangwani, wala hakuna mmoja wao aliyeachwa, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni. |
Questions about Numbers 26? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.