Proverbs 17
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Better a dry morsel in quietness than a house full of feasting with strife. | SWKCV 1 Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi. |
| BSB 2 A wise servant will rule over a disgraceful son and share his inheritance as one of the brothers. | SWKCV 2 Mtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye, naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu. |
| BSB 3 A crucible for silver and a furnace for gold, but the LORD is the tester of hearts. | SWKCV 3 Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu, bali Bwana huujaribu moyo. |
| BSB 4 A wicked man listens to evil lips; a liar gives ear to a destructive tongue. | SWKCV 4 Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya; mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara. |
| BSB 5 He who mocks the poor insults their Maker; whoever gloats over calamity will not go unpunished. | SWKCV 5 Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake; yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa. |
| BSB 6 Grandchildren are the crown of the aged, and the glory of a son is his father. | SWKCV 6 Wana wa wana ni taji la wazee, nao wazazi ni fahari ya watoto wao. |
| BSB 7 Eloquent words are unfit for a fool; how much worse are lying lips to a ruler! | SWKCV 7 Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu: je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala! |
| BSB 8 A bribe is a charm to its giver; wherever he turns, he succeeds. | SWKCV 8 Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; kokote kigeukiapo, hufanikiwa. |
| BSB 9 Whoever conceals an offense promotes love, but he who brings it up separates friends. | SWKCV 9 Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo, bali yeyote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu. |
| BSB 10 A rebuke cuts into a man of discernment deeper than a hundred lashes cut into a fool. | SWKCV 10 Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua kuliko mapigo mia kwa mpumbavu. |
| BSB 11 An evil man seeks only rebellion; a cruel messenger will be sent against him. | SWKCV 11 Mtu mbaya hupenda kuasi tu; mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake. |
| BSB 12 It is better to meet a bear robbed of her cubs than a fool in his folly. | SWKCV 12 Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyangʼanywa watoto wake, kuliko mpumbavu katika upumbavu wake. |
| BSB 13 If anyone returns evil for good, evil will never leave his house. | SWKCV 13 Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema, kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake. |
| BSB 14 To start a quarrel is to release a flood; so abandon the dispute before it breaks out. | SWKCV 14 Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji; kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza. |
| BSB 15 Acquitting the guilty and condemning the righteous—both are detestable to the LORD. | SWKCV 15 Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki, naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki: Bwana huwachukia sana wote wawili. |
| BSB 16 Why should the fool have money in his hand with no intention of buying wisdom? | SWKCV 16 Fedha ina faida gani mikononi mwa mpumbavu, wakati yeye hana haja ya kupata hekima? |
| BSB 17 A friend loves at all times, and a brother is born for adversity. | SWKCV 17 Rafiki hupenda wakati wote naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida. |
| BSB 18 A man lacking judgment strikes hands in pledge and puts up security for his neighbor. | SWKCV 18 Mtu mjinga hupana mkono ili kuweka rehani, naye huweka dhamana kwa jirani yake. |
| BSB 19 He who loves transgression loves strife; he who builds his gate high invites destruction. | SWKCV 19 Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi; naye ainuaye sana lango lake hutafuta uharibifu. |
| BSB 20 The one with a perverse heart finds no good, and he whose tongue is deceitful falls into trouble. | SWKCV 20 Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa; naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu. |
| BSB 21 A man fathers a fool to his own grief; the father of a fool has no joy. | SWKCV 21 Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni; hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu. |
| BSB 22 A joyful heart is good medicine, but a broken spirit dries up the bones. | SWKCV 22 Moyo wenye furaha ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka hukausha mifupa. |
| BSB 23 A wicked man takes a covert bribe to subvert the course of justice. | SWKCV 23 Mtu mwovu hukubali rushwa kwa siri ili kupotosha njia ya haki. |
| BSB 24 Wisdom is the focus of the discerning, but the eyes of a fool wander to the ends of the earth. | SWKCV 24 Mtu wa ufahamu huitazama hekima, lakini macho ya mpumbavu huhangaika hadi kwenye miisho ya dunia. |
| BSB 25 A foolish son brings grief to his father and bitterness to her who bore him. | SWKCV 25 Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake na uchungu kwa yeye aliyemzaa. |
| BSB 26 It is surely not good to punish the innocent or to flog a noble for his honesty. | SWKCV 26 Si vizuri kumwadhibu mtu asiye na hatia, au kuwapiga sana maafisa kwa ajili ya uadilifu wao. |
| BSB 27 A man of knowledge restrains his words, and a man of understanding maintains a calm spirit. | SWKCV 27 Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia, naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu. |
| BSB 28 Even a fool is considered wise if he keeps silent, and discerning when he holds his tongue. | SWKCV 28 Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima kama akinyamaza, na mwenye ufahamu kama akiuzuia ulimi wake. |
Questions about Proverbs 17? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.