Proverbs 24
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Do not envy wicked men or desire their company; | SWKCV 1 Usiwaonee wivu watu waovu, usitamani ushirika nao; |
| BSB 2 for their hearts devise violence, and their lips declare trouble. | SWKCV 2 kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, nayo midomo yao husema juu ya kuleta madhara. |
| BSB 3 By wisdom a house is built and by understanding it is established; | SWKCV 3 Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kwa njia ya ufahamu huimarishwa |
| BSB 4 through knowledge its rooms are filled with every precious and beautiful treasure. | SWKCV 4 kwa njia ya maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza. |
| BSB 5 A wise man is strong, and a man of knowledge enhances his strength. | SWKCV 5 Mtu mwenye hekima ana uwezo mkubwa, naye mtu mwenye maarifa huongeza nguvu, |
| BSB 6 Only with sound guidance should you wage war, and victory lies in a multitude of counselors. | SWKCV 6 kwa kufanya vita unahitaji uongozi na kwa ushindi washauri wengi. |
| BSB 7 Wisdom is too high for a fool; he does not open his mouth in the meeting place. | SWKCV 7 Hekima i juu mno kwa mpumbavu, katika kusanyiko langoni hana lolote la kusema. |
| BSB 8 He who plots evil will be called a schemer. | SWKCV 8 Yeye apangaye mabaya atajulikana kama mtu wa hila. |
| BSB 9 A foolish scheme is sin, and a mocker is detestable to men. | SWKCV 9 Mipango ya upumbavu ni dhambi, watu huchukizwa na mwenye dhihaka. |
| BSB 10 If you faint in the day of distress, how small is your strength! | SWKCV 10 Ukikata tamaa wakati wa taabu, jinsi gani nguvu zako ni kidogo! |
| BSB 11 Rescue those being led away to death, and restrain those stumbling toward the slaughter. | SWKCV 11 Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo; wazuie wote wanaojikokota kuelekea machinjoni. |
| BSB 12 If you say, “Behold, we did not know about this,” does not He who weighs hearts consider it? Does not the One who guards your life know? Will He not repay a man according to his deeds? | SWKCV 12 Kama mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,” je, yule apimaye mioyo halitambui hili? Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili? Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda? |
| BSB 13 Eat honey, my son, for it is good, and the honeycomb is sweet to your taste. | SWKCV 13 Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri; asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja. |
| BSB 14 Know therefore that wisdom is sweet to your soul. If you find it, there is a future for you, and your hope will never be cut off. | SWKCV 14 Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako, kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo, nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali. |
| BSB 15 Do not lie in wait, O wicked man, near the dwelling of the righteous; do not destroy his resting place. | SWKCV 15 Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia makao ya mwenye haki, wala usiyavamie makazi yake, |
| BSB 16 For though a righteous man may fall seven times, he still gets up; but the wicked stumble in bad times. | SWKCV 16 Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena, lakini waovu huangushwa chini na maafa. |
| BSB 17 Do not gloat when your enemy falls, and do not let your heart rejoice when he stumbles, | SWKCV 17 Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati ajikwaapo, usiruhusu moyo wako ushangilie. |
| BSB 18 or the LORD will see and disapprove, and turn His wrath away from him. | SWKCV 18 Bwana asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye. |
| BSB 19 Do not fret over evildoers, and do not be envious of the wicked. | SWKCV 19 Usikasirike kwa sababu ya watu wabaya wala usiwaonee wivu waovu, |
| BSB 20 For the evil man has no future; the lamp of the wicked will be extinguished. | SWKCV 20 kwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo, nayo taa ya waovu itazimwa. |
| BSB 21 My son, fear the LORD and the king, and do not associate with the rebellious. | SWKCV 21 Mwanangu, mche Bwana na mfalme, wala usijiunge na waasi, |
| BSB 22 For they will bring sudden destruction. Who knows what ruin they can bring? | SWKCV 22 kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao, naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta? |
| BSB 23 These also are sayings of the wise: To show partiality in judgment is not good. | SWKCV 23 Hii pia ni misemo ya wenye hekima: Kuonyesha upendeleo katika hukumu si vyema: |
| BSB 24 Whoever tells the guilty, “You are innocent”—peoples will curse him, and nations will denounce him; | SWKCV 24 Yeyote amwambiaye mwenye hatia, “Wewe huna hatia,” Kabila zitamlaani na mataifa yatamkana. |
| BSB 25 but it will go well with those who convict the guilty, and rich blessing will come upon them. | SWKCV 25 Bali itakuwa vyema kwa wale watakaowatia hatiani wenye hatia, nazo baraka tele zitawajilia juu yao. |
| BSB 26 An honest answer given is like a kiss on the lips. | SWKCV 26 Jawabu la uaminifu ni kama busu la midomoni. |
| BSB 27 Complete your outdoor work and prepare your field; after that, you may build your house. | SWKCV 27 Maliza kazi zako za nje, nawe uweke mashamba yako tayari, baada ya hayo, jenga nyumba yako. |
| BSB 28 Do not testify against your neighbor without cause, and do not deceive with your lips. | SWKCV 28 Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu, au kutumia midomo yako kudanganya. |
| BSB 29 Do not say, “I will do to him as he has done to me; I will repay the man according to his work.” | SWKCV 29 Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.” |
| BSB 30 I went past the field of a slacker and by the vineyard of a man lacking judgment. | SWKCV 30 Nilipita karibu na shamba la mvivu, karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili, |
| BSB 31 Thorns had grown up everywhere, thistles had covered the ground, and the stone wall was broken down. | SWKCV 31 miiba ilikuwa imeota kila mahali, ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka. |
| BSB 32 I observed and took it to heart; I looked and received instruction: | SWKCV 32 Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona, nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona: |
| BSB 33 A little sleep, a little slumber, a little folding of the hands to rest, | SWKCV 33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika: |
| BSB 34 and poverty will come upon you like a robber, and need like a bandit. | SWKCV 34 hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha. |
Questions about Proverbs 24? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.