Proverbs 27
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Do not boast about tomorrow, for you do not know what a day may bring. | SWKCV 1 Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja. |
| BSB 2 Let another praise you, and not your own mouth—a stranger, and not your own lips. | SWKCV 2 Mwache mwingine akusifu, wala si kinywa chako mwenyewe; mtu mwingine afanye hivyo na si midomo yako mwenyewe. |
| BSB 3 A stone is heavy and sand is a burden, but aggravation from a fool outweighs them both. | SWKCV 3 Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo, lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito kuliko vyote viwili. |
| BSB 4 Wrath is cruel and anger is like a flood, but who can withstand jealousy? | SWKCV 4 Hasira ni ukatili na ghadhabu kali ni gharika, lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu? |
| BSB 5 Better an open rebuke than love that is concealed. | SWKCV 5 Afadhali karipio la wazi kuliko upendo uliofichika. |
| BSB 6 The wounds of a friend are faithful, but the kisses of an enemy are deceitful. | SWKCV 6 Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu, bali kubusu kwa adui ni kwingi sana. |
| BSB 7 The soul that is full loathes honey, but to a hungry soul, any bitter thing is sweet. | SWKCV 7 Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali, bali kwa mwenye njaa hata kile kilicho kichungu kwake ni kitamu. |
| BSB 8 Like a bird that strays from its nest is a man who wanders from his home. | SWKCV 8 Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake, ndivyo alivyo mtu atangatangaye mbali na nyumbani mwake. |
| BSB 9 Oil and incense bring joy to the heart, and the counsel of a friend is sweetness to the soul. | SWKCV 9 Manukato na uvumba huleta furaha moyoni, nao uzuri wa rafiki huchipuka kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu. |
| BSB 10 Do not forsake your friend or your father’s friend, and do not go to your brother’s house in the day of your calamity; better a neighbor nearby than a brother far away. | SWKCV 10 Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako, tena usiende nyumbani mwa ndugu yako wakati umepatwa na maafa. Bora jirani wa karibu kuliko ndugu aliye mbali. |
| BSB 11 Be wise, my son, and bring joy to my heart, so that I can answer him who taunts me. | SWKCV 11 Mwanangu, uwe na hekima, nawe ulete furaha moyoni mwangu, ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote anitendaye kwa dharau. |
| BSB 12 The prudent see danger and take cover, but the simple keep going and pay the penalty. | SWKCV 12 Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele nayo ikamtesa. |
| BSB 13 Take the garment of him who posts security for a stranger; get collateral if it is for a foreigner. | SWKCV 13 Chukua vazi la yule awekaye dhamana kwa ajili ya mgeni; lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo kwa ajili ya mwanamke mpotovu. |
| BSB 14 If one blesses his neighbor with a loud voice early in the morning, it will be counted to him as a curse. | SWKCV 14 Kama mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu asubuhi na mapema, itahesabiwa kama ni laana. |
| BSB 15 A constant dripping on a rainy day and a contentious woman are alike— | SWKCV 15 Mke mgomvi ni kama matone yasiyokoma ya siku ya mvua. |
| BSB 16 restraining her is like holding back the wind or grasping oil with one’s right hand. | SWKCV 16 Kumzuia yeye ni kama kuuzuia upepo au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono. |
| BSB 17 As iron sharpens iron, so one man sharpens another. | SWKCV 17 Kama vile chuma kinoavyo chuma, ndivyo mtu amnoavyo mwenzake. |
| BSB 18 Whoever tends a fig tree will eat its fruit, and he who looks after his master will be honored. | SWKCV 18 Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake, naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa. |
| BSB 19 As water reflects the face, so the heart reflects the true man. | SWKCV 19 Kama uso uonekanavyo kwenye maji, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonyesha alivyo. |
| BSB 20 Sheol and Abaddon are never satisfied; so the eyes of man are never satisfied. | SWKCV 20 Kuzimu na Uharibifu havishibi kadhalika macho ya mwanadamu. |
| BSB 21 A crucible for silver and a furnace for gold, but a man is tested by the praise accorded him. | SWKCV 21 Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru kwa ajili ya dhahabu, bali mtu hupimwa kwa sifa azipokeazo. |
| BSB 22 Though you grind a fool like grain with mortar and a pestle, yet his folly will not depart from him. | SWKCV 22 Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, hutauondoa upumbavu wake. |
| BSB 23 Be sure to know the state of your flocks, and pay close attention to your herds; | SWKCV 23 Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi, angalia kwa bidii ngʼombe zako. |
| BSB 24 for riches are not forever, nor does a crown endure to every generation. | SWKCV 24 Kwa kuwa utajiri haudumu milele, nayo taji haidumu vizazi vyote. |
| BSB 25 When hay is removed and new growth appears and the grass from the hills is gathered, | SWKCV 25 Wakati majani makavu yameondolewa na mapya yamechipua, nayo majani toka milimani yamekusanywa, |
| BSB 26 the lambs will provide you with clothing, and the goats with the price of a field. | SWKCV 26 wana-kondoo watakupatia mavazi na mbuzi thamani ya shamba. |
| BSB 27 You will have plenty of goats’ milk to feed you—food for your household and nourishment for your maidservants. | SWKCV 27 Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi kukulisha wewe na jamaa yako, na kuwalisha watumishi wako wa kike. |
Questions about Proverbs 27? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.