Proverbs 9
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Wisdom has built her house; she has carved out her seven pillars. | SWKCV 1 Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo zake saba. |
| BSB 2 She has prepared her meat and mixed her wine; she has also set her table. | SWKCV 2 Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake; pia ameandaa meza yake. |
| BSB 3 She has sent out her maidservants; she calls out from the heights of the city. | SWKCV 3 Amewatuma watumishi wake wa kike, naye huita kutoka mahali pa juu sana pa mji. |
| BSB 4 “Whoever is simple, let him turn in here!” she says to him who lacks judgment. | SWKCV 4 Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa! |
| BSB 5 “Come, eat my bread and drink the wine I have mixed. | SWKCV 5 Njooni, mle chakula changu na mnywe divai niliyoichanganya. |
| BSB 6 Leave your folly behind, and you will live; walk in the way of understanding.” | SWKCV 6 Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu. |
| BSB 7 He who corrects a mocker brings shame on himself; he who rebukes a wicked man taints himself. | SWKCV 7 “Yeyote anayemkosoa mwenye mzaha hukaribisha matukano; yeyote anayekemea mtu mwovu hupatwa na matusi. |
| BSB 8 Do not rebuke a mocker, or he will hate you; rebuke a wise man, and he will love you. | SWKCV 8 Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia; mkemee mwenye hekima naye atakupenda. |
| BSB 9 Instruct a wise man, and he will be wiser still; teach a righteous man, and he will increase his learning. | SWKCV 9 Mfundishe mtu mwenye hekima naye atakuwa na hekima zaidi; mfundishe mtu mwadilifu naye atazidi kufundishika. |
| BSB 10 The fear of the LORD is the beginning of wisdom, and knowledge of the Holy One is understanding. | SWKCV 10 “Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu. |
| BSB 11 For through wisdom your days will be multiplied, and years will be added to your life. | SWKCV 11 Kwa maana kwa msaada wangu siku zako zitakuwa nyingi, na miaka itaongezwa katika maisha yako. |
| BSB 12 If you are wise, you are wise to your own advantage; but if you scoff, you alone will bear the consequences. | SWKCV 12 Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo; kama wewe ni mtu wa mzaha, wewe mwenyewe ndiwe utateseka.” |
| BSB 13 The woman named Folly is loud; she is naive and knows nothing. | SWKCV 13 Mwanamke aitwaye Mpumbavu ana kelele; hana adabu na hana maarifa. |
| BSB 14 She sits at the door of her house, on a seat in the heights of the city, | SWKCV 14 Huketi kwenye mlango wa nyumba yake, juu ya kiti katika mahali pa juu sana pa mji, |
| BSB 15 calling out to those who pass by, who make their paths straight. | SWKCV 15 akiita wale wapitao karibu, waendao moja kwa moja kwenye njia yao. |
| BSB 16 “Whoever is simple, let him turn in here!” she says to him who lacks judgment. | SWKCV 16 Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa ndani!” |
| BSB 17 “Stolen water is sweet, and bread eaten in secret is tasty!” | SWKCV 17 “Maji yaliyoibiwa ni matamu; chakula kinacholiwa sirini ni kitamu!” |
| BSB 18 But they do not know that the dead are there, that her guests are in the depths of Sheol. | SWKCV 18 Lakini hawajui hata kidogo kuwa wafu wako humo, kwamba wageni wake huyo mwanamke wako katika vilindi vya kuzimu. |
Questions about Proverbs 9? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.