Psalms 135
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Hallelujah! Praise the name of the LORD. Give praise, O servants of the LORD, | SWKCV 1 Msifuni Bwana. Lisifuni jina la Bwana, msifuni, enyi watumishi wa Bwana, |
| BSB 2 who stand in the house of the LORD, in the courts of the house of our God. | SWKCV 2 ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu. |
| BSB 3 Hallelujah, for the LORD is good; sing praises to His name, for it is lovely. | SWKCV 3 Msifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema, liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza. |
| BSB 4 For the LORD has chosen Jacob as His own, Israel as His treasured possession. | SWKCV 4 Kwa maana Bwana amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe, Israeli kuwa mali yake ya thamani. |
| BSB 5 For I know that the LORD is great; our Lord is above all gods. | SWKCV 5 Ninajua ya kuwa Bwana ni mkuu, kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote. |
| BSB 6 The LORD does all that pleases Him in the heavens and on the earth, in the seas and in all their depths. | SWKCV 6 Bwana hufanya lolote apendalo, mbinguni na duniani, katika bahari na vilindi vyake vyote. |
| BSB 7 He causes the clouds to rise from the ends of the earth. He generates the lightning with the rain and brings forth the wind from His storehouses. | SWKCV 7 Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia; hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua na huleta upepo kutoka ghala zake. |
| BSB 8 He struck down the firstborn of Egypt, of both man and beast. | SWKCV 8 Alimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama. |
| BSB 9 He sent signs and wonders into your midst, O Egypt, against Pharaoh and all his servants. | SWKCV 9 Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri, dhidi ya Farao na watumishi wake wote. |
| BSB 10 He struck down many nations and slaughtered mighty kings: | SWKCV 10 Aliyapiga mataifa mengi, na akaua wafalme wenye nguvu: |
| BSB 11 Sihon king of the Amorites, Og king of Bashan, and all the kings of Canaan. | SWKCV 11 Mfalme Sihoni na Waamori, Ogu mfalme wa Bashani na wafalme wote wa Kanaani: |
| BSB 12 He gave their land as an inheritance, as a heritage to His people Israel. | SWKCV 12 akatoa nchi yao kuwa urithi, urithi kwa watu wake Israeli. |
| BSB 13 Your name, O LORD, endures forever, Your renown, O LORD, through all generations. | SWKCV 13 Ee Bwana, jina lako ladumu milele, kumbukumbu za fahari zako, Ee Bwana, kwa vizazi vyote. |
| BSB 14 For the LORD will vindicate His people and will have compassion on His servants. | SWKCV 14 Maana Bwana atawathibitisha watu wake, na kuwahurumia watumishi wake. |
| BSB 15 The idols of the nations are silver and gold, made by the hands of men. | SWKCV 15 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. |
| BSB 16 They have mouths, but cannot speak; they have eyes, but cannot see; | SWKCV 16 Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona; |
| BSB 17 they have ears, but cannot hear; nor is there breath in their mouths. | SWKCV 17 zina masikio, lakini haziwezi kusikia, wala hakuna pumzi katika vinywa vyao. |
| BSB 18 Those who make them become like them, as do all who trust in them. | SWKCV 18 Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia. |
| BSB 19 O house of Israel, bless the LORD; O house of Aaron, bless the LORD; | SWKCV 19 Ee nyumba ya Israeli, msifuni Bwana; ee nyumba ya Aroni, msifuni Bwana; |
| BSB 20 O house of Levi, bless the LORD; you who fear the LORD, bless the LORD! | SWKCV 20 ee nyumba ya Lawi, msifuni Bwana; ninyi mnaomcha, msifuni Bwana. |
| BSB 21 Blessed be the LORD from Zion—He who dwells in Jerusalem. Hallelujah! | SWKCV 21 Msifuni Bwana kutoka Sayuni, msifuni yeye aishiye Yerusalemu. Msifuni Bwana. |
Questions about Psalms 135? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.