Psalms 36
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 For the choirmaster. A Psalm of David, the servant of the LORD. An oracle is in my heart regarding the transgression of the wicked man: There is no fear of God before his eyes. | SWKCV 1 Kuna neno moyoni mwangu kuhusu hali ya dhambi ya mwovu. Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake. |
| BSB 2 For his eyes are too full of conceit to detect or hate his own sin. | SWKCV 2 Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake. |
| BSB 3 The words of his mouth are wicked and deceitful; he has ceased to be wise and well-doing. | SWKCV 3 Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu, ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema. |
| BSB 4 Even on his bed he plots wickedness; he sets himself on a path that is not good; he fails to reject evil. | SWKCV 4 Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya, hujitia katika njia ya dhambi na hakatai lililo baya. |
| BSB 5 Your loving devotion, O LORD, reaches to the heavens, Your faithfulness to the clouds. | SWKCV 5 Upendo wako, Ee Bwana, unafika hadi mbinguni, uaminifu wako hadi kwenye anga. |
| BSB 6 Your righteousness is like the highest mountains; Your judgments are like the deepest sea. O LORD, You preserve man and beast. | SWKCV 6 Haki yako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama kilindi kikuu. Ee Bwana, wewe huwahifadhi mwanadamu na mnyama. |
| BSB 7 How precious is Your loving devotion, O God, that the children of men take refuge in the shadow of Your wings! | SWKCV 7 Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mbawa zako. |
| BSB 8 They feast on the abundance of Your house, and You give them drink from Your river of delights. | SWKCV 8 Wanajifurahisha katika wingi nyumbani mwako, nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako. |
| BSB 9 For with You is the fountain of life; in Your light we see light. | SWKCV 9 Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, katika nuru yako twaona nuru. |
| BSB 10 Extend Your loving devotion to those who know You, and Your righteousness to the upright in heart. | SWKCV 10 Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe, haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo. |
| BSB 11 Let not the foot of the proud come against me, nor the hand of the wicked drive me away. | SWKCV 11 Mguu wa mwenye kiburi usije dhidi yangu, wala mkono wa mwovu usinifukuze. |
| BSB 12 There the evildoers lie fallen, thrown down and unable to rise. | SWKCV 12 Angalia jinsi watenda mabaya walivyoanguka: wametupwa chini, hawawezi kuinuka! |
Questions about Psalms 36? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.