Revelation 9
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then the fifth angel sounded his trumpet, and I saw a star that had fallen from heaven to earth, and it was given the key to the pit of the Abyss. | SWKCV 1 Malaika wa tano akaipiga tarumbeta yake, nami nikaona nyota iliyokuwa imeanguka toka angani hadi ardhini. Nyota hiyo ilipewa ufunguo wa lile Shimo. |
| BSB 2 The star opened the pit of the Abyss, and smoke rose out of it like the smoke of a great furnace, and the sun and the air were darkened by the smoke from the pit. | SWKCV 2 Alipolifungua hilo Shimo, moshi ukapanda kutoka humo kama moshi wa tanuru kubwa sana. Jua na anga vikatiwa giza na ule moshi uliotoka katika hilo Shimo. |
| BSB 3 And out of the smoke, locusts descended on the earth, and they were given power like that of the scorpions of the earth. | SWKCV 3 Ndipo katika ule moshi wakatoka nzige wakaenda juu ya nchi, nao wakapewa nguvu kama zile za nge wa duniani. |
| BSB 4 They were told not to harm the grass of the earth or any plant or tree, but only those who did not have the seal of God on their foreheads. | SWKCV 4 Wakaambiwa wasidhuru nyasi ya nchi, wala mmea wala mti wowote, bali wawadhuru tu wale watu ambao hawana muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso zao. |
| BSB 5 The locusts were not given power to kill them, but only to torment them for five months, and their torment was like the stinging of a scorpion. | SWKCV 5 Wakaruhusiwa kuwatesa kwa muda wa miezi mitano, lakini wasiwaue. Uchungu wa kuuma kwao ulikuwa kama ule wa mtu aumwapo na nge. |
| BSB 6 In those days men will seek death and will not find it; they will long to die, but death will escape them. | SWKCV 6 Katika siku hizo watu watatafuta kifo lakini hawatakiona, watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia. |
| BSB 7 And the locusts looked like horses prepared for battle, with something like crowns of gold on their heads; and their faces were like the faces of men. | SWKCV 7 Wale nzige walikuwa na umbo kama la farasi waliotayarishwa kwa ajili ya vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji za dhahabu na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu. |
| BSB 8 They had hair like that of women, and teeth like those of lions. | SWKCV 8 Walikuwa na nywele kama za wanawake, na meno yao yalikuwa kama ya simba. |
| BSB 9 They also had breastplates like breastplates of iron, and the sound of their wings was like the roar of many horses and chariots rushing into battle. | SWKCV 9 Walikuwa na dirii kama za chuma, na sauti za mabawa yao zilikuwa kama ngurumo za farasi wengi na magari mengi yakikimbilia vitani. |
| BSB 10 They had tails with stingers like scorpions, which had the power to injure people for five months. | SWKCV 10 Walikuwa na mikia yenye miiba ya kuumia kama nge. Nguvu yao ya kutesa watu kwa huo muda wa miezi mitano ilikuwa katika hiyo mikia yao. |
| BSB 11 They were ruled by a king, the angel of the Abyss. His name in Hebrew is Abaddon, and in Greek it is Apollyon. | SWKCV 11 Walikuwa na mfalme wao, ambaye ni malaika wa lile Shimo, ambaye jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani ni Apolioni. |
| BSB 12 The first woe has passed. Behold, two woes are still to follow. | SWKCV 12 Ole ya kwanza imepita, bado nyingine mbili zinakuja. |
| BSB 13 Then the sixth angel sounded his trumpet, and I heard a voice from the four horns of the golden altar before God | SWKCV 13 Malaika wa sita akaipiga tarumbeta yake, nami nikasikia sauti ikitoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyoko mbele za Mungu. |
| BSB 14 saying to the sixth angel with the trumpet, “Release the four angels who are bound at the great river Euphrates.” | SWKCV 14 Ile sauti ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye ule mto mkubwa Frati.” |
| BSB 15 So the four angels who had been prepared for this hour and day and month and year were released to kill a third of mankind. | SWKCV 15 Basi wale malaika wanne, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ajili ya saa hiyo, na siku hiyo, na mwezi huo, na mwaka huo ili wawaue theluthi ya wanadamu wakafunguliwa. |
| BSB 16 And the number of mounted troops was two hundred million; I heard their number. | SWKCV 16 Idadi ya majeshi wapanda farasi ilikuwa 200,000,000. Nilisikia idadi yao. |
| BSB 17 Now the horses and riders in my vision looked like this: The riders had breastplates the colors of fire, sapphire, and sulfur. The heads of the horses were like the heads of lions, and out of their mouths proceeded fire, smoke, and sulfur. | SWKCV 17 Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika maono yangu: Wapanda farasi walivaa dirii vifuani zenye rangi nyekundu sana kama ya moto na yakuti samawi na kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vichwa vya simba, na moto, moshi na kiberiti vilitoka vinywani mwao. |
| BSB 18 A third of mankind was killed by the three plagues of fire, smoke, and sulfur that proceeded from their mouths. | SWKCV 18 Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo hayo matatu, yaani, huo moto, moshi na kiberiti, vilivyotoka kwenye vinywa vya hao farasi. |
| BSB 19 For the power of the horses was in their mouths and in their tails; indeed, their tails were like snakes, having heads with which to inflict harm. | SWKCV 19 Nguvu za hao farasi zilikuwa katika vinywa vyao na kwenye mikia yao, kwa sababu mikia yao ilikuwa kama nyoka, yenye vichwa ambayo waliitumia kudhuru. |
| BSB 20 Now the rest of mankind who were not killed by these plagues still did not repent of the works of their hands. They did not stop worshiping demons and idols of gold, silver, bronze, stone, and wood, which cannot see or hear or walk. | SWKCV 20 Wanadamu waliosalia, ambao hawakuuawa katika mapigo hayo, bado walikataa kutubia kazi za mikono yao na hawakuacha kuabudu mashetani na sanamu za dhahabu, za fedha, za shaba, za mawe na za miti, ambazo haziwezi kuona, kusikia wala kutembea. |
| BSB 21 Furthermore, they did not repent of their murder, sorcery, sexual immorality, and theft. | SWKCV 21 Wala hawakutubu na kuacha matendo yao ya uuaji, uchawi, uasherati wala wizi wao. |
Questions about Revelation 9? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.