1 Corinthians 16
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now about the collection for the saints, you are to do as I directed the churches of Galatia: | SWKCV 1 Basi kuhusu changizo kwa ajili ya watakatifu: Kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia, fanyeni vivyo hivyo. |
| BSB 2 On the first day of every week, each of you should set aside a portion of his income, saving it up, so that when I come no collections will be needed. | SWKCV 2 Siku ya kwanza ya kila juma, kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha, kulingana na mapato yake na fedha hizo aziweke akiba, ili nitakapokuja pasiwe na lazima ya kufanya mchango. |
| BSB 3 Then, on my arrival, I will send letters with those you recommend to carry your gift to Jerusalem. | SWKCV 3 Kwa hiyo nitakapowasili, nitawapa wale mtakaowachagua barua za kuwatambulisha, ili kuwatuma wapeleke zawadi zenu huko Yerusalemu. |
| BSB 4 And if it is advisable for me to go also, they can travel with me. | SWKCV 4 Kama ikionekana ni vyema na mimi niende, basi hao watu watafuatana nami. |
| BSB 5 After I go through Macedonia, however, I will come to you; for I will be going through Macedonia. | SWKCV 5 Baada ya kupitia Makedonia nitakuja kwenu, maana ninakusudia kupitia Makedonia. |
| BSB 6 Perhaps I will stay with you awhile, or even spend the winter, so that you can help me on my journey, wherever I go. | SWKCV 6 Huenda nitakaa nanyi kwa muda, au hata kukaa nanyi kipindi chote cha baridi, ili mweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendapo. |
| BSB 7 For I do not want to see you now only in passing; I hope to spend some time with you, if the Lord permits. | SWKCV 7 Kwa maana sitaki niwaone sasa na kupita tu; natarajia kuwa nanyi kwa muda wa kutosha, kama Bwana akipenda. |
| BSB 8 But I will stay in Ephesus until Pentecost, | SWKCV 8 Lakini nitakaa Efeso mpaka wakati wa Pentekoste, |
| BSB 9 because a great door for effective work has opened to me, even though many oppose me. | SWKCV 9 kwa maana mlango mkubwa umefunguliwa kwangu kufanya kazi yenye matunda, nako huko kuna adui wengi wanaonipinga. |
| BSB 10 If Timothy comes, see to it that he has nothing to fear while he is with you, for he is doing the work of the Lord, just as I am. | SWKCV 10 Ikiwa Timotheo atakuja kwenu, hakikisheni kwamba hana hofu yoyote akiwa nanyi, kwa sababu anafanya kazi ya Bwana, kama mimi nifanyavyo. |
| BSB 11 No one, then, should treat him with contempt. Send him on his way in peace so that he can return to me, for I am expecting him along with the brothers. | SWKCV 11 Basi asiwepo mtu atakayekataa kumpokea. Msafirisheni kwa amani ili aweze kunijia tena. Namtarajia pamoja na ndugu. |
| BSB 12 Now about our brother Apollos: I strongly urged him to go to you with the brothers. He was not at all inclined to go now, but he will go when he has the opportunity. | SWKCV 12 Basi kwa habari za ndugu yetu Apolo, nimemsihi kwa bidii aje kwenu pamoja na hao ndugu. Ingawa alikuwa hapendi kabisa kuja sasa, lakini atakuja apatapo nafasi. |
| BSB 13 Be on the alert. Stand firm in the faith. Be men of courage. Be strong. | SWKCV 13 Kesheni, simameni imara katika imani, fanyeni kiume, kuweni mashujaa kuweni hodari. |
| BSB 14 Do everything in love. | SWKCV 14 Fanyeni kila kitu katika upendo. |
| BSB 15 You know that Stephanas and his household were the first converts in Achaia, and they have devoted themselves to the service of the saints. Now I urge you, brothers, | SWKCV 15 Ninyi mnajua kwamba watu wa nyumbani mwa Stefana ndio waliokuwa wa kwanza kuamini katika Akaya, nao wamejitoa kwa ajili ya kuwahudumia watakatifu. Ndugu nawasihi, |
| BSB 16 to submit to such as these, and to every fellow worker and laborer. | SWKCV 16 mjitie katika kuwahudumia watu kama hawa na kila mmoja aingiaye kwenye kazi na kuifanya kwa bidii. |
| BSB 17 I am glad that Stephanas, Fortunatus, and Achaicus have arrived, because they have supplied what was lacking from you. | SWKCV 17 Nilifurahi wakati Stefana, Fortunato na Akaiko walipofika, kwa sababu wamenipatia yale niliyopungukiwa kutoka kwenu. |
| BSB 18 For they refreshed my spirit and yours as well. Show your appreciation, therefore, to such men. | SWKCV 18 Kwa kuwa waliiburudisha roho yangu na zenu pia. Watu kama hawa wanastahili kutambuliwa. |
| BSB 19 The churches in the province of Asia send you greetings. Aquila and Prisca greet you warmly in the Lord, and so does the church that meets at their house. | SWKCV 19 Makanisa ya Asia yanawasalimu. Akila na Prisila, pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao wanawasalimu sana katika Bwana. |
| BSB 20 All the brothers here send you greetings. Greet one another with a holy kiss. | SWKCV 20 Ndugu wote walioko hapa wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu. |
| BSB 21 This greeting is in my own hand—Paul. | SWKCV 21 Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. |
| BSB 22 If anyone does not love the Lord, let him be under a curse. Come, O Lord! | SWKCV 22 Kama mtu yeyote hampendi Bwana Yesu Kristo, na alaaniwe. Bwana wetu, njoo. |
| BSB 23 The grace of the Lord Jesus be with you. | SWKCV 23 Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi. |
| BSB 24 My love be with all of you in Christ Jesus. Amen. | SWKCV 24 Upendo wangu uwe nanyi nyote katika Kristo Yesu. Amen. |
Questions about 1 Corinthians 16? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.