1 Thessalonians 5
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now about the times and seasons, brothers, we do not need to write to you. | SWKCV 1 Basi, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira hatuna haja ya kuwaandikia, |
| BSB 2 For you are fully aware that the Day of the Lord will come like a thief in the night. | SWKCV 2 kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajapo usiku. |
| BSB 3 While people are saying, “Peace and security,” destruction will come upon them suddenly, like labor pains on a pregnant woman, and they will not escape. | SWKCV 3 Wakati watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka. |
| BSB 4 But you, brothers, are not in the darkness so that this day should overtake you like a thief. | SWKCV 4 Bali ninyi, ndugu, hampo gizani hata siku ile iwakute ghafula kama mwizi. |
| BSB 5 For you are all sons of the light and sons of the day; we do not belong to the night or to the darkness. | SWKCV 5 Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku. |
| BSB 6 So then, let us not sleep as the others do, but let us remain awake and sober. | SWKCV 6 Kwa hiyo basi, tusilale kama watu wengine walalavyo, bali tukeshe na kuwa na kiasi. |
| BSB 7 For those who sleep, sleep at night, and those who get drunk, get drunk at night. | SWKCV 7 Kwa kuwa wote walalao hulala usiku na wale walewao hulewa usiku. |
| BSB 8 But since we belong to the day, let us be sober, putting on the breastplate of faith and love, and the helmet of our hope of salvation. | SWKCV 8 Lakini kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukijivika imani na upendo kama dirii kifuani na tumaini letu la wokovu kama chapeo. |
| BSB 9 For God has not appointed us to suffer wrath, but to obtain salvation through our Lord Jesus Christ. | SWKCV 9 Kwa maana Mungu hakutuita ili tupate ghadhabu bali tupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. |
| BSB 10 He died for us so that, whether we are awake or asleep, we may live together with Him. | SWKCV 10 Yeye alikufa kwa ajili yetu ili hata kama tuko macho au tumelala, tupate kuishi pamoja naye. |
| BSB 11 Therefore encourage and build one another up, just as you are already doing. | SWKCV 11 Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa. |
| BSB 12 But we ask you, brothers, to acknowledge those who work diligently among you, who care for you in the Lord and who admonish you. | SWKCV 12 Sasa tunawaomba, ndugu, waheshimuni wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu, wale ambao wana mamlaka juu yenu katika Bwana na ambao wanawaonya. |
| BSB 13 In love, hold them in highest regard because of their work. Live in peace with one another. | SWKCV 13 Waheshimuni sana katika upendo kwa ajili ya kazi zao. Ishini kwa amani ninyi kwa ninyi. |
| BSB 14 And we urge you, brothers, to admonish the unruly, encourage the fainthearted, help the weak, and be patient with everyone. | SWKCV 14 Nasi twawasihi, ndugu, waonyeni walio wavivu, watieni moyo waoga, wasaidieni wanyonge na kuwavumilia watu wote. |
| BSB 15 Make sure that no one repays evil for evil. Always pursue what is good for one another and for all people. | SWKCV 15 Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote. |
| BSB 16 Rejoice at all times. | SWKCV 16 Furahini siku zote; |
| BSB 17 Pray without ceasing. | SWKCV 17 ombeni bila kukoma; |
| BSB 18 Give thanks in every circumstance, for this is God’s will for you in Christ Jesus. | SWKCV 18 shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu. |
| BSB 19 Do not extinguish the Spirit. | SWKCV 19 Msiuzime moto wa Roho Mtakatifu; |
| BSB 20 Do not treat prophecies with contempt, | SWKCV 20 msiyadharau maneno ya unabii. |
| BSB 21 but test all things. Hold fast to what is good. | SWKCV 21 Jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema. |
| BSB 22 Abstain from every form of evil. | SWKCV 22 Jiepusheni na uovu wa kila namna. |
| BSB 23 Now may the God of peace Himself sanctify you completely, and may your entire spirit, soul, and body be kept blameless at the coming of our Lord Jesus Christ. | SWKCV 23 Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo. |
| BSB 24 The One who calls you is faithful, and He will do it. | SWKCV 24 Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya hayo. |
| BSB 25 Brothers, pray for us as well. | SWKCV 25 Ndugu, tuombeeni. |
| BSB 26 Greet all the brothers with a holy kiss. | SWKCV 26 Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu. |
| BSB 27 I charge you before the Lord to have this letter read to all the brothers. | SWKCV 27 Nawaagizeni mbele za Bwana mhakikishe kuwa ndugu wote wanasomewa barua hii. |
| BSB 28 The grace of our Lord Jesus Christ be with you. | SWKCV 28 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi. Amen. |
Questions about 1 Thessalonians 5? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.