2 Thessalonians 3
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Finally, brothers, pray for us, that the word of the Lord may spread quickly and be held in honor, just as it was with you. | SWKCV 1 Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili Neno la Bwana lipate kuenea kwa haraka na kuheshimiwa kila mahali, kama vile ilivyokuwa kwenu. |
| BSB 2 And pray that we may be delivered from wicked and evil men; for not everyone holds to the faith. | SWKCV 2 Ombeni pia ili tupate kuokolewa kutokana na watu waovu na wabaya, kwa maana si wote wanaoamini. |
| BSB 3 But the Lord is faithful, and He will strengthen you and guard you from the evil one. | SWKCV 3 Lakini Bwana ni mwaminifu, naye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutokana na yule mwovu. |
| BSB 4 And we have confidence in the Lord that you are doing and will continue to do what we command. | SWKCV 4 Nasi tuna tumaini katika Bwana ya kuwa mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaagiza. |
| BSB 5 May the Lord direct your hearts into God’s love and Christ’s perseverance. | SWKCV 5 Bwana aiongoze mioyo yenu katika upendo wa Mungu na katika saburi ya Kristo. |
| BSB 6 Now we command you, brothers, in the name of our Lord Jesus Christ, to keep away from any brother who leads an undisciplined life that is not in keeping with the tradition you received from us. | SWKCV 6 Ndugu, tunawaagiza katika Jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapa. |
| BSB 7 For you yourselves know how you ought to imitate us, because we were not undisciplined among you, | SWKCV 7 Maana ninyi wenyewe mnajua jinsi iwapasavyo kufuata mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa pamoja nanyi, |
| BSB 8 nor did we eat anyone’s food without paying for it. Instead, in labor and toil, we worked night and day so that we would not be a burden to any of you. | SWKCV 8 wala hatukula chakula cha mtu yeyote pasipo kukilipia. Badala yake tulifanya kazi kwa bidii usiku na mchana, ili tusimlemee mtu yeyote miongoni mwenu. |
| BSB 9 Not that we lack this right, but we wanted to offer ourselves as an example for you to imitate. | SWKCV 9 Tulifanya hivi, si kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada kama huo, bali ndio sisi wenyewe tuwe kielelezo. |
| BSB 10 For even while we were with you, we gave you this command: “If anyone is unwilling to work, he shall not eat.” | SWKCV 10 Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri kwamba: “Mtu yeyote asiyetaka kufanya kazi, hata kula asile.” |
| BSB 11 For we hear that some of you are leading undisciplined lives, accomplishing nothing, but being busybodies. | SWKCV 11 Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi bali hujishughulisha na mambo ya wengine. |
| BSB 12 We command and urge such people by our Lord Jesus Christ to begin working quietly to earn their own living. | SWKCV 12 Basi watu kama hao tunawaagiza na kuwahimiza katika Bwana Yesu Kristo, kwamba wafanye kazi kwa utulivu kwa ajili ya chakula chao wenyewe. |
| BSB 13 But as for you, brothers, do not grow weary in well-doing. | SWKCV 13 Kwa upande wenu, ndugu, ninyi kamwe msichoke katika kutenda mema. |
| BSB 14 Take note of anyone who does not obey the instructions we have given in this letter. Do not associate with him, so that he may be ashamed. | SWKCV 14 Ikiwa mtu yeyote hayatii maagizo yetu yaliyoko katika barua hii, mwangalieni sana mtu huyo. Msishirikiane naye, ili apate kuona aibu. |
| BSB 15 Yet do not regard him as an enemy, but admonish him as a brother. | SWKCV 15 Lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu. |
| BSB 16 Now may the Lord of peace Himself give you peace at all times and in every way. The Lord be with all of you. | SWKCV 16 Basi, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa kila njia. Bwana awe nanyi nyote. |
| BSB 17 This greeting is in my own hand—Paul. This is my mark in every letter; it is the way I write. | SWKCV 17 Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Hivi ndivyo niandikavyo. |
| BSB 18 The grace of our Lord Jesus Christ be with all of you. | SWKCV 18 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote. Amen. |
Questions about 2 Thessalonians 3? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.