2 Timothy 2
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 You therefore, my child, be strong in the grace that is in Christ Jesus. | SWKCV 1 Basi, wewe mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo ndani ya Kristo Yesu. |
| BSB 2 And the things that you have heard me say among many witnesses, entrust these to faithful men who will be qualified to teach others as well. | SWKCV 2 Nayo mambo yale uliyonisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu watakaoweza kuwafundisha watu wengine vilevile. |
| BSB 3 Join me in suffering, like a good soldier of Christ Jesus. | SWKCV 3 Vumilia taabu pamoja nasi kama askari mwema wa Kristo Yesu. |
| BSB 4 A soldier refrains from entangling himself in civilian affairs, in order to please the one who enlisted him. | SWKCV 4 Hakuna askari yeyote ambaye akiwa vitani hujishughulisha na mambo ya kawaida ya maisha haya kwa sababu nia yake ni kumpendeza yule aliyemwandika awe askari. |
| BSB 5 Likewise, a competitor does not receive the crown unless he competes according to the rules. | SWKCV 5 Vivyo hivyo, yeye ashindanaye katika michezo hawezi kupewa tuzo ya ushindi asiposhindana kulingana na kanuni za mashindano. |
| BSB 6 The hardworking farmer should be the first to partake of the crops. | SWKCV 6 Mkulima mwenye bidii ya kazi ndiye anayestahili kuwa wa kwanza kupata fungu la mavuno. |
| BSB 7 Consider what I am saying, for the Lord will give you insight into all things. | SWKCV 7 Fikiri sana kuhusu haya nisemayo, kwa maana Bwana atakupa ufahamu katika mambo hayo yote. |
| BSB 8 Remember Jesus Christ, raised from the dead, descended from David, as proclaimed by my gospel, | SWKCV 8 Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, yeye aliye wa uzao wa Daudi. Hii ndiyo Injili yangu, |
| BSB 9 for which I suffer to the extent of being chained like a criminal. But the word of God cannot be chained! | SWKCV 9 ambayo kwayo ninateseka hata kufikia hatua ya kufungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu halifungwi. |
| BSB 10 For this reason I endure all things for the sake of the elect, so that they too may obtain the salvation that is in Christ Jesus, with eternal glory. | SWKCV 10 Kwa hiyo ninavumilia mambo yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, kusudi wao nao wapate wokovu ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele. |
| BSB 11 This is a trustworthy saying: If we died with Him, we will also live with Him; | SWKCV 11 Hili ni neno la kuaminiwa: Kwa maana kama tumekufa pamoja naye, tutaishi pia pamoja naye. |
| BSB 12 if we endure, we will also reign with Him; if we deny Him, He will also deny us; | SWKCV 12 Kama tukistahimili, pia tutatawala pamoja naye. Kama tukimkana yeye, naye atatukana sisi. |
| BSB 13 if we are faithless, He remains faithful, for He cannot deny Himself. | SWKCV 13 Kama tusipoamini, yeye hudumu kuwa mwaminifu, kwa maana hawezi kujikana mwenyewe. |
| BSB 14 Remind the believers of these things, charging them before God to avoid quarreling over words, which succeeds only in leading the listeners to ruin. | SWKCV 14 Endelea kuwakumbusha mambo haya ukiwaonya mbele za Bwana waache kushindana kwa maneno ambayo hayana faida yoyote bali huwaangamiza tu wale wanaoyasikia. |
| BSB 15 Make every effort to present yourself approved to God, an unashamed workman who accurately handles the word of truth. | SWKCV 15 Jitahidi kujionyesha kwa Mungu kuwa umekubaliwa naye, mtendakazi asiye na sababu ya kuona aibu, ukilitumia kwa usahihi neno la kweli. |
| BSB 16 But avoid irreverent, empty chatter, which will only lead to more ungodliness, | SWKCV 16 Jiepushe na maneno mabaya, yasiyo na maana, yasiyo ya utauwa, kwa maana hayo huzidi kuwatosa watu katika kukosa heshima kwa Mungu. |
| BSB 17 and the talk of such men will spread like gangrene. Among them are Hymenaeus and Philetus, | SWKCV 17 Mafundisho yao yataenea kama kidonda kisichopona. Miongoni mwao wamo Himenayo na Fileto |
| BSB 18 who have deviated from the truth. They say that the resurrection has already occurred, and they undermine the faith of some. | SWKCV 18 ambao wameiacha kweli, wakisema kwamba ufufuo wa wafu umekwisha kuwako, nao huharibu imani ya baadhi ya watu. |
| BSB 19 Nevertheless, God’s firm foundation stands, bearing this seal: “The Lord knows those who are His,” and, “Everyone who calls on the name of the Lord must turn away from iniquity.” | SWKCV 19 Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, ukiwa na muhuri wenye maandishi haya: “Bwana anawajua walio wake”; tena, “Kila alitajaye jina la Bwana, na auache uovu.” |
| BSB 20 A large house contains not only vessels of gold and silver, but also of wood and clay. Some indeed are for honorable use, but others are for common use. | SWKCV 20 Katika nyumba kubwa si kwamba kuna vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali pia vimo vyombo vya miti na vya udongo; vingine kwa matumizi maalum, na vingine kwa matumizi ya kawaida. |
| BSB 21 So if anyone cleanses himself of what is unfit, he will be a vessel for honor: sanctified, useful to the Master, and prepared for every good work. | SWKCV 21 Basi ikiwa mtu amejitakasa na kujitenga na hayo niliyoyataja, atakuwa chombo maalum, kilichotengwa na ambacho kinamfaa mwenye nyumba, kimeandaliwa tayari kwa kila kazi njema. |
| BSB 22 Flee from youthful passions and pursue righteousness, faith, love, and peace, together with those who call on the Lord out of a pure heart. | SWKCV 22 Zikimbie tamaa mbaya za ujana, ufuate haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. |
| BSB 23 But reject foolish and ignorant speculation, for you know that it breeds quarreling. | SWKCV 23 Jiepushe na mabishano ya kipumbavu na yasiyo na maana, kwa kuwa wajua ya kwamba hayo huzaa magomvi. |
| BSB 24 And a servant of the Lord must not be quarrelsome, but must be kind to everyone, able to teach, and forbearing. | SWKCV 24 Tena haimpasi mtumishi wa Bwana kuwa mgomvi, bali inampasa awe mwema kwa kila mtu, awezaye kufundisha, tena mvumilivu. |
| BSB 25 He must gently reprove those who oppose him, in the hope that God may grant them repentance leading to a knowledge of the truth. | SWKCV 25 Inampasa kuwaonya kwa upole wale wanaopingana naye, kwa matumaini kwamba Mungu atawajalia kutubu na kuijua kweli, |
| BSB 26 Then they will come to their senses and escape the snare of the devil, who has taken them captive to his will. | SWKCV 26 ili fahamu zao ziwarudie tena, nao waponyoke katika mtego wa ibilisi ambaye amewateka wapate kufanya mapenzi yake. |
Questions about 2 Timothy 2? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.