Colossians 4
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Masters, supply your slaves with what is right and fair, since you know that you also have a Master in heaven. | SWKCV 1 Ninyi mabwana, watendeeni watumwa wenu yaliyo haki na yanayostahili, mkitambua ya kwamba ninyi pia mnaye Bwana mbinguni. |
| BSB 2 Devote yourselves to prayer, being watchful and thankful, | SWKCV 2 Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru. |
| BSB 3 as you pray also for us, that God may open to us a door for the word, so that we may proclaim the mystery of Christ, for which I am in chains. | SWKCV 3 Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa. |
| BSB 4 Pray that I may declare it clearly, as I should. | SWKCV 4 Ombeni ili nipate kuitangaza Injili kwa udhahiri kama ipasavyo kunena. |
| BSB 5 Act wisely toward outsiders, redeeming the time. | SWKCV 5 Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. |
| BSB 6 Let your speech always be gracious, seasoned with salt, so that you may know how to answer everyone. | SWKCV 6 Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo na inavyofaa kumjibu kila mtu. |
| BSB 7 Tychicus will tell you all the news about me. He is a beloved brother, a faithful minister, and a fellow servant in the Lord. | SWKCV 7 Tikiko atawaambia habari zangu zote. Yeye ni ndugu mpendwa, mtendakazi mwaminifu na mtumishi mwenzangu katika Bwana. |
| BSB 8 I have sent him to you for this very purpose, that you may know about us, and that he may encourage your hearts. | SWKCV 8 Nimemtuma kwenu kwa madhumuni haya ili mpate kufahamu hali yetu, na pia awatie moyo. |
| BSB 9 With him I am sending Onesimus, our faithful and beloved brother, who is one of you. They will tell you about everything here. | SWKCV 9 Anakuja pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpendwa na mwaminifu, ambaye ni mmoja wenu. Watawaambia mambo yote yanayotendeka hapa kwetu. |
| BSB 10 My fellow prisoner Aristarchus sends you greetings, as does Mark the cousin of Barnabas. You have already received instructions about him: If he comes to you, welcome him. | SWKCV 10 Aristarko aliye mfungwa pamoja nami anawasalimu, vivyo hivyo Marko, binamu yake Barnaba. (Mmeshapata maagizo yanayomhusu; akija kwenu, mpokeeni.) |
| BSB 11 Jesus, who is called Justus, also sends greetings. These are the only Jews among my fellow workers for the kingdom of God, and they have been a comfort to me. | SWKCV 11 Yesu, yeye aitwaye Yusto, pia anawasalimu. Hawa peke yao ndio Wayahudi miongoni mwa watendakazi wenzangu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, nao wamekuwa faraja kwangu. |
| BSB 12 Epaphras, who is one of you and a servant of Christ Jesus, sends you greetings. He is always wrestling in prayer for you, so that you may stand mature and fully assured in the full will of God. | SWKCV 12 Epafra, ambaye ni mmoja wenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimu. Yeye siku zote anawaombea kwa bidii kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mungu, mkiwa wakamilifu na thabiti. |
| BSB 13 For I testify about him that he goes to great pains for you and for those at Laodicea and Hierapolis. | SWKCV 13 Ninashuhudia kumhusu kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, na kwa ajili ya ndugu wa Laodikia na wale wa Hierapoli. |
| BSB 14 Luke, the beloved physician, and Demas send you greetings. | SWKCV 14 Rafiki yetu mpenzi Luka yule tabibu, pamoja na Dema, wanawasalimu. |
| BSB 15 Greet the brothers in Laodicea, as well as Nympha and the church that meets at her house. | SWKCV 15 Wasalimuni ndugu wote wa Laodikia, na pia Nimfa, pamoja na kanisa linalokutana katika nyumba yake. |
| BSB 16 After this letter has been read among you, make sure that it is also read in the church of the Laodiceans, and that you in turn read the letter from Laodicea. | SWKCV 16 Baada ya barua hii kusomwa kwenu, hakikisheni kwamba inasomwa pia katika kanisa la Walaodikia. Nanyi pia msome barua inayotoka Laodikia. |
| BSB 17 Tell Archippus: “See to it that you complete the ministry you have received in the Lord.” | SWKCV 17 Mwambieni Arkipo hivi: “Hakikisha kuwa unakamilisha ile huduma uliyopokea katika Bwana.” |
| BSB 18 This greeting is in my own hand—Paul. Remember my chains. Grace be with you. | SWKCV 18 Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni minyororo yangu. Neema iwe nanyi. Amen. |
Questions about Colossians 4? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.