Colossians 3
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Therefore, since you have been raised with Christ, strive for the things above, where Christ is seated at the right hand of God. | SWKCV 1 Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo alikoketi mkono wa kuume wa Mungu. |
| BSB 2 Set your minds on things above, not on earthly things. | SWKCV 2 Yafikirini mambo yaliyo juu, wala si ya duniani. |
| BSB 3 For you died, and your life is now hidden with Christ in God. | SWKCV 3 Kwa maana ninyi mlikufa, nao uhai wenu sasa umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. |
| BSB 4 When Christ, who is your life, appears, then you also will appear with Him in glory. | SWKCV 4 Wakati Kristo, aliye uzima wenu, atakapotokea, ndipo nanyi mtakapotokea pamoja naye katika utukufu. |
| BSB 5 Put to death, therefore, the components of your earthly nature: sexual immorality, impurity, lust, evil desires, and greed, which is idolatry. | SWKCV 5 Kwa hiyo, ueni kabisa chochote kilicho ndani yenu cha asili ya kidunia: yaani uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya na ulafi, ambayo ndiyo ibada ya sanamu. |
| BSB 6 Because of these, the wrath of God is coming on the sons of disobedience. | SWKCV 6 Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu ya Mungu inakuja. |
| BSB 7 When you lived among them, you also used to walk in these ways. | SWKCV 7 Ninyi pia zamani mlienenda katika mambo haya mlipoishi maisha hayo. |
| BSB 8 But now you must put aside all such things as these: anger, rage, malice, slander, and filthy language from your lips. | SWKCV 8 Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote: yaani hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu. |
| BSB 9 Do not lie to one another, since you have taken off the old self with its practices, | SWKCV 9 Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake, |
| BSB 10 and have put on the new self, which is being renewed in knowledge in the image of its Creator. | SWKCV 10 nanyi mmevaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu sawasawa na mfano wa Muumba wake. |
| BSB 11 Here there is no Greek or Jew, circumcised or uncircumcised, barbarian, Scythian, slave, or free, but Christ is all and is in all. | SWKCV 11 Hapa hakuna Myunani wala Myahudi, aliyetahiriwa wala asiyetahiriwa, asiyestaarabika wala aliyestaarabika, mtumwa wala mtu huru, bali Kristo ni yote, na ndani ya wote. |
| BSB 12 Therefore, as the elect of God, holy and beloved, clothe yourselves with hearts of compassion, kindness, humility, gentleness, and patience. | SWKCV 12 Kwa hiyo, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. |
| BSB 13 Bear with one another and forgive any complaint you may have against someone else. Forgive as the Lord forgave you. | SWKCV 13 Vumilianeni na kusameheana mtu akiwa na lalamiko lolote dhidi ya mwenzake. Sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi. |
| BSB 14 And over all these virtues put on love, which is the bond of perfect unity. | SWKCV 14 Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika umoja mkamilifu. |
| BSB 15 Let the peace of Christ rule in your hearts, for to this you were called as members of one body. And be thankful. | SWKCV 15 Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani. |
| BSB 16 Let the word of Christ richly dwell within you as you teach and admonish one another with all wisdom, and as you sing psalms, hymns, and spiritual songs with gratitude in your hearts to God. | SWKCV 16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu. |
| BSB 17 And whatever you do, in word or deed, do it all in the name of the Lord Jesus, giving thanks to God the Father through Him. | SWKCV 17 Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye. |
| BSB 18 Wives, submit to your husbands, as is fitting in the Lord. | SWKCV 18 Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana. |
| BSB 19 Husbands, love your wives and do not be harsh with them. | SWKCV 19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe na uchungu dhidi yao. |
| BSB 20 Children, obey your parents in everything, for this is pleasing to the Lord. | SWKCV 20 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hivi ndivyo inavyompendeza Bwana. |
| BSB 21 Fathers, do not provoke your children, so they will not become discouraged. | SWKCV 21 Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa. |
| BSB 22 Slaves, obey your earthly masters in everything, not only to please them while they are watching, but with sincerity of heart and fear of the Lord. | SWKCV 22 Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, wala si kwa kutafuta upendeleo wao, bali kwa moyo mnyofu na kumcha Bwana. |
| BSB 23 Whatever you do, work at it with your whole being, as for the Lord and not for men, | SWKCV 23 Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu, |
| BSB 24 because you know that you will receive an inheritance from the Lord as your reward. It is the Lord Christ you are serving. | SWKCV 24 kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Yesu Kristo mnayemtumikia. |
| BSB 25 Whoever does wrong will be repaid for his wrong, and there is no favoritism. | SWKCV 25 Yeyote atendaye mabaya atalipwa kwa ajili ya mabaya yake, wala hakuna upendeleo. |
Questions about Colossians 3? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.