Deuteronomy 23
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 No man with crushed or severed genitals may enter the assembly of the LORD. | SWKCV 1 Asiingie mtu yeyote aliyehasiwa kwa kupondwa makende au kwa kukatwa uume wake katika kusanyiko la Bwana. |
| BSB 2 No one of illegitimate birth may enter the assembly of the LORD, nor may any of his descendants, even to the tenth generation. | SWKCV 2 Mtu yeyote ambaye amezaliwa kwenye ndoa isiyo halali au wazao wake wasiingie kwenye kusanyiko la Bwana, hata mpaka kizazi cha kumi. |
| BSB 3 No Ammonite or Moabite or any of their descendants may enter the assembly of the LORD, even to the tenth generation. | SWKCV 3 Hapatakuwa na Mwamoni au Mmoabu au yeyote wa wazao wao atakayeruhusiwa kuingia katika kusanyiko la Bwana, hata mpaka kizazi cha kumi. |
| BSB 4 For they did not meet you with food and water on your way out of Egypt, and they hired Balaam son of Beor from Pethor in Aram-naharaim to curse you. | SWKCV 4 Kwa kuwa hawakuja kuwalaki wakiwa na mkate na maji mlipokuwa njiani mlipotoka Misri, tena walimwajiri Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyoko Aramu-Naharaimu ili kuwalaani ninyi. |
| BSB 5 Yet the LORD your God would not listen to Balaam, and the LORD your God turned the curse into a blessing for you, because the LORD your God loves you. | SWKCV 5 Hata hivyo, Bwana Mungu wenu hakumsikiliza Balaamu bali aligeuza laana kuwa baraka kwenu kwa sababu Bwana Mungu wenu anawapenda. |
| BSB 6 You are not to seek peace or prosperity from them as long as you live. | SWKCV 6 Msitafute mapatano ya urafiki nao maisha yenu yote. |
| BSB 7 Do not despise an Edomite, for he is your brother. Do not despise an Egyptian, because you lived as a foreigner in his land. | SWKCV 7 Usimchukie Mwedomu, kwa kuwa yeye ni ndugu yako. Usimchukie Mmisri, kwa sababu uliishi kama mgeni katika nchi yake. |
| BSB 8 The third generation of children born to them may enter the assembly of the LORD. | SWKCV 8 Kizazi cha tatu cha watoto watakaozaliwa nao wanaweza kuingia katika kusanyiko la Bwana. |
| BSB 9 When you are encamped against your enemies, then you shall keep yourself from every wicked thing. | SWKCV 9 Unapokuwa umepiga kambi dhidi ya adui zako, jitenge na kitu chochote kisicho safi. |
| BSB 10 If any man among you becomes unclean because of a nocturnal emission, he must leave the camp and stay outside. | SWKCV 10 Ikiwa mtu amechafuka kwa sababu ya kutokwa na shahawa usiku, inampasa atoke nje ya kambi na kukaa huko. |
| BSB 11 When evening approaches, he must wash with water, and when the sun sets he may return to the camp. | SWKCV 11 Lakini jioni ikikaribia ataoga, na baada ya jua kuzama ataingia tena kambini. |
| BSB 12 You must have a place outside the camp to go and relieve yourself. | SWKCV 12 Tengeni mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda kujisaidia. |
| BSB 13 And you must have a digging tool in your equipment so that when you relieve yourself you can dig a hole and cover up your excrement. | SWKCV 13 Kama sehemu ya vifaa vyenu kuweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho. |
| BSB 14 For the LORD your God walks throughout your camp to protect you and deliver your enemies to you. Your camp must be holy, lest He see anything unclean among you and turn away from you. | SWKCV 14 Kwa kuwa Bwana Mungu wenu hutembea katika kambi yenu ili kuwalinda na kuwaweka adui zenu mikononi mwenu. Kambi yenu ni lazima iwe takatifu, ili asione kitu chochote miongoni mwenu kilicho kichafu akageuka na kuwaacha. |
| BSB 15 Do not return a slave to his master if he has taken refuge with you. | SWKCV 15 Ikiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake. |
| BSB 16 Let him live among you wherever he chooses, in the town of his pleasing. Do not oppress him. | SWKCV 16 Mwache aishi miongoni mwenu mahali popote anapopapenda na katika mji wowote anaochagua. Usimwonee. |
| BSB 17 No daughter or son of Israel is to be a shrine prostitute. | SWKCV 17 Asiwepo Mwisraeli mwanamke kahaba au mwanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu. |
| BSB 18 You must not bring the wages of a prostitute, whether female or male, into the house of the LORD your God to fulfill any vow, because both are detestable to the LORD your God. | SWKCV 18 Kamwe usilete mapato ya ukahaba ikiwa ni ya mwanamke au ni ya mwanaume katika nyumba ya Bwana Mungu wako kwa ajili ya nadhiri yoyote, kwa sababu Bwana Mungu wako anachukizwa na yote mawili. |
| BSB 19 Do not charge your brother interest on money, food, or any other type of loan. | SWKCV 19 Usimtoze ndugu yako riba, iwe ni fedha ama chakula ama kitu kingine chochote ambacho waweza kupata riba juu yake. |
| BSB 20 You may charge a foreigner interest, but not your brother, so that the LORD your God may bless you in everything to which you put your hand in the land that you are entering to possess. | SWKCV 20 Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili kwamba Bwana Mungu wako akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoingia kuimiliki. |
| BSB 21 If you make a vow to the LORD your God, do not be slow to keep it, because He will surely require it of you, and you will be guilty of sin. | SWKCV 21 Ukiweka nadhiri kwa Bwana Mungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi. |
| BSB 22 But if you refrain from making a vow, you will not be guilty of sin. | SWKCV 22 Lakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia. |
| BSB 23 Be careful to follow through on what comes from your lips, because you have freely vowed to the LORD your God with your own mouth. | SWKCV 23 Chochote kitakachotamkwa kwa midomo yako ni lazima uhakikishe umekifanya, kwa sababu uliweka nadhiri yako kwa hiari mbele za Bwana Mungu wako kwa kinywa chako mwenyewe. |
| BSB 24 When you enter your neighbor’s vineyard, you may eat your fill of grapes, but you must not put any in your basket. | SWKCV 24 Kama ukiingia katika shamba la mizabibu la jirani yako, unaweza kula zabibu kadiri utakavyo, lakini usiweke chochote kwenye kikapu chako. |
| BSB 25 When you enter your neighbor’s grainfield, you may pluck the heads of grain with your hand, but you must not put a sickle to your neighbor’s grain. | SWKCV 25 Kama ukiingia katika shamba la nafaka la jirani yako, unaweza kukwanyua kwa mikono yako, lakini usikate kwa mundu nafaka iliyosimama. |
Questions about Deuteronomy 23? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.