Ephesians 3
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 For this reason I, Paul, the prisoner of Christ Jesus for the sake of you Gentiles... | SWKCV 1 Kwa sababu hii, mimi Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi watu wa Mataifa: |
| BSB 2 Surely you have heard about the stewardship of God’s grace that was given to me for you, | SWKCV 2 Kwa hakika mmekwisha kusikia kuhusu ile huduma ya neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu, |
| BSB 3 that is, the mystery made known to me by revelation, as I have already written briefly. | SWKCV 3 yaani, ile siri iliodhihirishwa kwangu kwa njia ya ufunuo, kama nilivyotangulia kuandika kwa kifupi. |
| BSB 4 In reading this, then, you will be able to understand my insight into the mystery of Christ, | SWKCV 4 Kwa kusoma haya, basi mtaweza kuelewa ufahamu wangu katika siri ya Kristo. |
| BSB 5 which was not made known to men in other generations as it has now been revealed by the Spirit to God’s holy apostles and prophets. | SWKCV 5 Siri hii haikudhihirishwa kwa wanadamu katika vizazi vingine kama vile sasa ilivyodhihirishwa na Roho kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu. |
| BSB 6 This mystery is that through the gospel the Gentiles are fellow heirs, fellow members of the body, and fellow partakers of the promise in Christ Jesus. | SWKCV 6 Siri hii ni kwamba, kwa njia ya Injili, watu wa Mataifa ni warithi pamoja na Israeli, viungo vya mwili mmoja na washiriki pamoja wa ahadi katika Kristo Yesu. |
| BSB 7 I became a servant of this gospel by the gift of God’s grace, given me through the working of His power. | SWKCV 7 Nimekuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa nguvu yake itendayo kazi. |
| BSB 8 Though I am less than the least of all the saints, this grace was given me: to preach to the Gentiles the unsearchable riches of Christ, | SWKCV 8 Ingawa mimi ni mdogo kuliko aliye mdogo kabisa miongoni mwa watakatifu wote, nilipewa neema hii: ili niwahubirie watu wa Mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo, |
| BSB 9 and to illuminate for everyone the stewardship of this mystery, which for ages past was kept hidden in God, who created all things. | SWKCV 9 na kuweka wazi kwa kila mtu siri hii iliyokuwa imefichwa tangu zamani katika Mungu, aliyeumba vitu vyote. |
| BSB 10 His purpose was that now, through the church, the manifold wisdom of God should be made known to the rulers and authorities in the heavenly realms, | SWKCV 10 Ili sasa kwa njia ya Kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kujulikana kwa watawala na wenye mamlaka katika ulimwengu wa roho, |
| BSB 11 according to the eternal purpose that He accomplished in Christ Jesus our Lord. | SWKCV 11 sawasawa na kusudi lake la milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. |
| BSB 12 In Him and through faith in Him we may enter God’s presence with boldness and confidence. | SWKCV 12 Ndani yake na kwa njia ya imani katika yeye twaweza kumkaribia Mungu kwa uhuru na kwa ujasiri. |
| BSB 13 So I ask you not to be discouraged because of my sufferings for you, which are your glory. | SWKCV 13 Kwa hiyo, nawaomba msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, hayo ni utukufu wenu. |
| BSB 14 ... for this reason I bow my knees before the Father, | SWKCV 14 Kwa sababu hii nampigia Baba magoti, |
| BSB 15 from whom every family in heaven and on earth derives its name. | SWKCV 15 ambaye ubaba wote wa kila jamaa za mbinguni na za duniani unatokana naye. |
| BSB 16 I ask that out of the riches of His glory He may strengthen you with power through His Spirit in your inner being, | SWKCV 16 Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, |
| BSB 17 so that Christ may dwell in your hearts through faith. Then you, being rooted and grounded in love, | SWKCV 17 ili kwamba, Kristo apate kukaa mioyoni mwenu kwa njia ya imani. Nami ninaomba kwamba ninyi mkiwa wenye mizizi tena imara katika msingi wa upendo, |
| BSB 18 will have power, together with all the saints, to comprehend the length and width and height and depth | SWKCV 18 mwe na uwezo wa kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, urefu, kimo na kina upendo wa Kristo, |
| BSB 19 of the love of Christ, and to know this love that surpasses knowledge, that you may be filled with all the fullness of God. | SWKCV 19 na kujua upendo huu unaopita fahamu, ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wote wa Mungu. |
| BSB 20 Now to Him who is able to do immeasurably more than all we ask or imagine, according to His power that is at work within us, | SWKCV 20 Basi kwa yeye awezaye kutenda mambo ya ajabu yasiyopimika kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya uweza wake ule utendao kazi ndani yetu, |
| BSB 21 to Him be the glory in the church and in Christ Jesus throughout all generations, forever and ever. Amen. | SWKCV 21 yeye atukuzwe katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amen. |
Questions about Ephesians 3? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.