Galatians 3
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 O foolish Galatians! Who has bewitched you? Before your very eyes Jesus Christ was clearly portrayed as crucified. | SWKCV 1 Ninyi Wagalatia wajinga! Ni nani aliyewaroga? Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele yenu kwamba amesulubiwa. |
| BSB 2 I would like to learn just one thing from you: Did you receive the Spirit by works of the law, or by hearing with faith? | SWKCV 2 Nataka nijifunze neno moja kutoka kwenu: Je, mlipokea Roho wa Mungu kwa kushika sheria, au kwa kuyaamini yale mliyosikia? |
| BSB 3 Are you so foolish? After starting in the Spirit, are you now finishing in the flesh? | SWKCV 3 Je, ninyi ni wajinga kiasi hicho? Baada ya kuanza kwa Roho, je, sasa mwataka kumalizia katika mwili? |
| BSB 4 Have you suffered so much for nothing, if it really was for nothing? | SWKCV 4 Je, mlipata mateso kiasi hicho bure? Ni kama kweli yalikuwa bure! |
| BSB 5 Does God lavish His Spirit on you and work miracles among you because you practice the law, or because you hear and believe? | SWKCV 5 Je, Mungu huwapa Roho wake na kufanya miujiza katikati yenu kwa sababu mnatii sheria, au kwa sababu mnaamini kile mlichosikia? |
| BSB 6 So also, “Abraham believed God, and it was credited to him as righteousness.” | SWKCV 6 Kama vile “Abrahamu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki.” |
| BSB 7 Understand, then, that those who have faith are sons of Abraham. | SWKCV 7 Fahamuni basi kwamba wale walio na imani, hao ndio watoto wa Abrahamu. |
| BSB 8 The Scripture foresaw that God would justify the Gentiles by faith, and foretold the gospel to Abraham: “All nations will be blessed through you.” | SWKCV 8 Maandiko yakitabiri kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa Mataifa kwa imani, alitangulia kumtangazia Abrahamu Injili akisema kwamba, “Kwa kupitia kwako mataifa yote yatabarikiwa.” |
| BSB 9 So those who have faith are blessed along with Abraham, the man of faith. | SWKCV 9 Kwa sababu hii, wale wote wanaoamini wanabarikiwa pamoja na Abrahamu, mtu wa imani. |
| BSB 10 All who rely on works of the law are under a curse. For it is written: “Cursed is everyone who does not continue to do everything written in the Book of the Law.” | SWKCV 10 Kwa maana wote wanaotumainia matendo ya sheria wako chini ya laana, kwa kuwa imeandikwa, “Alaaniwe kila mtu asiyeshikilia kutii mambo yote yaliyoandikwa katika Kitabu cha Sheria.” |
| BSB 11 Now it is clear that no one is justified before God by the law, because, “The righteous will live by faith.” | SWKCV 11 Basi ni dhahiri kwamba hakuna mtu anayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa kushikilia sheria, kwa maana, “Mwenye haki ataishi kwa imani.” |
| BSB 12 The law, however, is not based on faith; on the contrary, “The man who does these things will live by them.” | SWKCV 12 Lakini sheria haitegemei imani. Kinyume chake, “Mtu atendaye matendo hayo ataishi kwa hayo.” |
| BSB 13 Christ redeemed us from the curse of the law by becoming a curse for us. For it is written: “Cursed is everyone who is hung on a tree.” | SWKCV 13 Kristo alitukomboa kutoka laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.” |
| BSB 14 He redeemed us in order that the blessing promised to Abraham would come to the Gentiles in Christ Jesus, so that by faith we might receive the promise of the Spirit. | SWKCV 14 Alitukomboa ili kwamba baraka aliyopewa Abrahamu ipate kuwafikia watu wa Mataifa kwa njia ya Kristo Yesu, ili kwa imani tupate kupokea ile ahadi ya Roho. |
| BSB 15 Brothers, let me put this in human terms. Even a human covenant, once it is ratified, cannot be canceled or amended. | SWKCV 15 Ndugu zangu, nataka nitoe mfano kutoka maisha ya kila siku. Kama vile hakuna mtu awezaye kutangua au kuongeza kitu katika agano la mtu ambalo limekwisha kuthibitishwa, vivyo hivyo kwa hali kama hii. |
| BSB 16 The promises were spoken to Abraham and to his seed. The Scripture does not say, “and to seeds,” meaning many, but “and to your seed,” meaning One, who is Christ. | SWKCV 16 Ahadi zilinenwa kwa Abrahamu na kwa mzao wake. Maandiko hayasemi “kwa wazao,” likimaanisha watu wengi, bali “kwa mzao wako,” yaani mtu mmoja, ndiye Kristo. |
| BSB 17 What I mean is this: The law that came 430 years later does not revoke the covenant previously established by God, so as to nullify the promise. | SWKCV 17 Ninachotaka kusema ni kwamba, sheria, ambayo ilitolewa miaka 430 baadaye, haitangui Agano lililothibitishwa na Mungu ili kuibatilisha ahadi ile. |
| BSB 18 For if the inheritance depends on the law, then it no longer depends on a promise; but God freely granted it to Abraham through a promise. | SWKCV 18 Kwa maana kama urithi hupatikana kwa sheria, basi hautegemei tena ahadi, lakini Mungu kwa neema yake alimpa Abrahamu urithi kwa njia ya ahadi. |
| BSB 19 Why then was the law given? It was added because of transgressions, until the arrival of the seed to whom the promise referred. It was administered through angels by a mediator. | SWKCV 19 Kwa nini basi iwepo sheria? Sheria iliwekwa kwa sababu ya makosa mpaka atakapokuja yule Mzao wa Abrahamu, ambaye alitajwa katika ile ahadi. Sheria iliamriwa na malaika kwa mkono wa mpatanishi. |
| BSB 20 A mediator is unnecessary, however, for only one party; but God is one. | SWKCV 20 Basi mpatanishi huhusisha zaidi ya upande mmoja, lakini Mungu ni mmoja. |
| BSB 21 Is the law, then, opposed to the promises of God? Certainly not! For if a law had been given that could impart life, then righteousness would certainly have come from the law. | SWKCV 21 Je basi, sheria inapingana na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa maana kama sheria iliyotolewa ingeweza kuwapa watu uzima, basi haki ingepatikana kwa njia ya sheria. |
| BSB 22 But the Scripture pronounces all things confined by sin, so that by faith in Jesus Christ the promise might be given to those who believe. | SWKCV 22 Lakini Maandiko yamefanya vitu vyote vifungwe chini ya nguvu ya dhambi, ili yale yaliyoahidiwa kwa njia ya imani katika Yesu Kristo yapate kupewa wale wanaoamini. |
| BSB 23 Before this faith came, we were held in custody under the law, locked up until faith should be revealed. | SWKCV 23 Kabla imani hii haijaja tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ile imani ifunuliwe. |
| BSB 24 So the law became our guardian to lead us to Christ, that we might be justified by faith. | SWKCV 24 Hivyo, sheria ilikuwa kiongozi kutufikisha kwa Kristo, ili tupate kuhesabiwa haki kwa imani. |
| BSB 25 Now that faith has come, we are no longer under a guardian. | SWKCV 25 Lakini sasa kwa kuwa ile imani imekuja, hatusimamiwi tena na sheria. |
| BSB 26 You are all sons of God through faith in Christ Jesus. | SWKCV 26 Kwa maana ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika Kristo Yesu kwa njia ya imani. |
| BSB 27 For all of you who were baptized into Christ have clothed yourselves with Christ. | SWKCV 27 Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Kristo, mmemvaa Kristo. |
| BSB 28 There is neither Jew nor Greek, slave nor free, male nor female, for you are all one in Christ Jesus. | SWKCV 28 Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu. |
| BSB 29 And if you belong to Christ, then you are Abraham’s seed and heirs according to the promise. | SWKCV 29 Nanyi mkiwa ni mali ya Kristo, basi ninyi ni wa uzao wa Abrahamu na warithi sawasawa na ile ahadi. |
Questions about Galatians 3? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.