Job 10
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “I loathe my own life; I will express my complaint and speak in the bitterness of my soul. | SWKCV 1 “Nayachukia sana haya maisha yangu; kwa hiyo nitatoa malalamiko yangu kwa wazi bila kujizuia, nami nitanena kutokana na uchungu wa moyo wangu. |
| BSB 2 I will say to God: Do not condemn me! Let me know why You prosecute me. | SWKCV 2 Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu. |
| BSB 3 Does it please You to oppress me, to reject the work of Your hands and favor the schemes of the wicked? | SWKCV 3 Je, inakupendeza wewe kunionea, kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu? |
| BSB 4 Do You have eyes of flesh? Do You see as man sees? | SWKCV 4 Je, wewe una macho ya kimwili? Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo? |
| BSB 5 Are Your days like those of a mortal, or Your years like those of a man, | SWKCV 5 Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu, au miaka yako ni kama ile ya mtu, |
| BSB 6 that You should seek my iniquity and search out my sin— | SWKCV 6 ili kwamba utafute makosa yangu na kuichunguza dhambi yangu; |
| BSB 7 though You know that I am not guilty, and there is no deliverance from Your hand? | SWKCV 7 ingawa wajua kuwa mimi sina hatia, na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako? |
| BSB 8 Your hands shaped me and altogether formed me. Would You now turn and destroy me? | SWKCV 8 “Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya. Je, sasa utageuka na kuniangamiza? |
| BSB 9 Please remember that You molded me like clay. Would You now return me to dust? | SWKCV 9 Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi. Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena? |
| BSB 10 Did You not pour me out like milk, and curdle me like cheese? | SWKCV 10 Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa, na kunigandisha kama jibini, |
| BSB 11 You clothed me with skin and flesh, and knit me together with bones and sinews. | SWKCV 11 ukanivika ngozi na nyama, na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa? |
| BSB 12 You have granted me life and loving devotion, and Your care has preserved my spirit. | SWKCV 12 Umenipa uhai na kunitendea wema, katika uangalizi wako umeilinda roho yangu. |
| BSB 13 Yet You concealed these things in Your heart, and I know that this was in Your mind: | SWKCV 13 “Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako, nami ninajua kuwa hili lilikuwa katika nia yako: |
| BSB 14 If I sinned, You would take note, and would not acquit me of my iniquity. | SWKCV 14 Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona, wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa. |
| BSB 15 If I am guilty, woe to me! And even if I am righteous, I cannot lift my head. I am full of shame and aware of my affliction. | SWKCV 15 Kama nina hatia, ole wangu! Hata kama ningekuwa sina hatia, siwezi kukiinua kichwa changu, kwa kuwa nimejawa na aibu, na kuzama katika mateso yangu. |
| BSB 16 Should I hold my head high, You would hunt me like a lion, and again display Your power against me. | SWKCV 16 Kama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba, na kuonyesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu. |
| BSB 17 You produce new witnesses against me and multiply Your anger toward me. Hardships assault me in wave after wave. | SWKCV 17 Wewe waleta mashahidi wapya dhidi yangu na kuzidisha hasira yako juu yangu; nazo nguvu zako zinanijia wimbi moja baada ya jingine. |
| BSB 18 Why then did You bring me from the womb? Oh, that I had died, and no eye had seen me! | SWKCV 18 “Kwa nini basi ulinitoa tumboni? Ninatamani ningekufa kabla jicho lolote halijaniona. |
| BSB 19 If only I had never come to be, but had been carried from the womb to the grave. | SWKCV 19 Laiti nisingekuwako kamwe, au ningekuwa nimechukuliwa moja kwa moja kutoka tumboni kwenda kaburini! |
| BSB 20 Are my days not few? Withdraw from me, that I may have a little comfort, | SWKCV 20 Je, siku zangu chache si zimekaribia kuisha? Niachie ili niweze kupata muda mfupi wa kufurahi |
| BSB 21 before I go—never to return—to a land of darkness and gloom, | SWKCV 21 kabla sijaenda mahali ambapo hakuna kurudi tena, katika nchi ya giza na uvuli wa mauti, |
| BSB 22 to a land of utter darkness, of deep shadow and disorder, where even the light is like darkness.” | SWKCV 22 nchi ya giza kuu sana, yenye uvuli wa giza na machafuko, mahali ambapo hata nuru ni giza.” |
Questions about Job 10? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.