John 10
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “Truly, truly, I tell you, whoever does not enter the sheepfold by the gate, but climbs in some other way, is a thief and a robber. | SWKCV 1 “Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, ni mwizi na mnyangʼanyi. |
| BSB 2 But the one who enters by the gate is the shepherd of the sheep. | SWKCV 2 Yeye anayeingia kwa kupitia kwenye lango ndiye mchungaji wa kondoo. |
| BSB 3 The gatekeeper opens the gate for him, and the sheep listen for his voice. He calls his own sheep by name and leads them out. | SWKCV 3 Mlinzi humfungulia lango na kondoo huisikia sauti yake. Huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa nje ya zizi. |
| BSB 4 When he has brought out all his own, he goes on ahead of them, and his sheep follow him because they know his voice. | SWKCV 4 Akiisha kuwatoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaijua sauti yake. |
| BSB 5 But they will never follow a stranger; in fact, they will flee from him because they do not recognize his voice.” | SWKCV 5 Lakini kondoo hawatamfuata mgeni bali watamkimbia, kwa sababu hawaijui sauti ya mgeni.” |
| BSB 6 Jesus spoke to them using this illustration, but they did not understand what He was telling them. | SWKCV 6 Yesu alitumia mfano huu, lakini wao hawakuelewa hayo aliyokuwa akiwaambia. |
| BSB 7 So He said to them again, “Truly, truly, I tell you, I am the gate for the sheep. | SWKCV 7 Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Amin, amin nawaambia, mimi ndimi lango la kondoo. |
| BSB 8 All who came before Me were thieves and robbers, but the sheep did not listen to them. | SWKCV 8 Wote walionitangulia ni wevi na wanyangʼanyi, lakini kondoo hawakuwasikia. |
| BSB 9 I am the gate. If anyone enters through Me, he will be saved. He will come in and go out and find pasture. | SWKCV 9 Mimi ndimi lango, yeyote anayeingia zizini kwa kupitia kwangu ataokoka, ataingia na kutoka, naye atapata malisho. |
| BSB 10 The thief comes only to steal and kill and destroy. I have come that they may have life, and have it in all its fullness. | SWKCV 10 Mwizi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. Mimi nimekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele. |
| BSB 11 I am the good shepherd. The good shepherd lays down His life for the sheep. | SWKCV 11 “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. |
| BSB 12 The hired hand is not the shepherd, and the sheep are not his own. When he sees the wolf coming, he abandons the sheep and runs away. Then the wolf pounces on them and scatters the flock. | SWKCV 12 Mtu wa kuajiriwa sio mchungaji mwenye kondoo. Amwonapo mbwa mwitu akija, yeye hukimbia na kuwaacha kondoo. Naye mbwa mwitu hulishambulia kundi na kulitawanya. |
| BSB 13 The man runs away because he is a hired servant and is unconcerned for the sheep. | SWKCV 13 Yeye hukimbia kwa sababu ameajiriwa wala hawajali kondoo. |
| BSB 14 I am the good shepherd. I know My sheep and My sheep know Me, | SWKCV 14 “Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu nao kondoo wangu wananijua. |
| BSB 15 just as the Father knows Me and I know the Father. And I lay down My life for the sheep. | SWKCV 15 Kama vile Baba anavyonijua mimi, nami ninavyomjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. |
| BSB 16 I have other sheep that are not of this fold. I must bring them in as well, and they will listen to My voice. Then there will be one flock and one shepherd. | SWKCV 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili, inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu, hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja. |
| BSB 17 The reason the Father loves Me is that I lay down My life in order to take it up again. | SWKCV 17 Baba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena. |
| BSB 18 No one takes it from Me, but I lay it down of My own accord. I have authority to lay it down and authority to take it up again. This charge I have received from My Father.” | SWKCV 18 Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.” |
| BSB 19 Again there was division among the Jews because of Jesus’ message. | SWKCV 19 Kwa maneno haya Wayahudi waligawanyika. |
| BSB 20 Many of them said, “He is demon-possessed and insane. Why would you listen to Him?” | SWKCV 20 Wengi wao wakasema, “Huyu amepagawa na pepo mchafu, naye amechanganyikiwa.” |
| BSB 21 But others replied, “These are not the words of a man possessed by a demon. Can a demon open the eyes of the blind?” | SWKCV 21 Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mtu aliyepagawa na pepo mchafu. Je, pepo mchafu aweza kufungua macho ya kipofu?” |
| BSB 22 At that time the Feast of Dedication took place in Jerusalem. It was winter, | SWKCV 22 Wakati huo ilikuwa Sikukuu ya Kuwekwa wakfu kwa Hekalu huko Yerusalemu, nao ulikuwa wakati wa majira ya baridi. |
| BSB 23 and Jesus was walking in the temple courts in Solomon’s Colonnade. | SWKCV 23 Naye Yesu alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika ukumbi wa Solomoni. |
| BSB 24 So the Jews gathered around Him and demanded, “How long will You keep us in suspense? If You are the Christ, tell us plainly.” | SWKCV 24 Wayahudi wakamkusanyikia wakamuuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo tuambie waziwazi.” |
| BSB 25 “I already told you,” Jesus replied, “but you did not believe. The works I do in My Father’s name testify on My behalf. | SWKCV 25 Yesu akawajibu, “Nimewaambia, lakini hamwamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yananishuhudia. |
| BSB 26 But because you are not My sheep, you refuse to believe. | SWKCV 26 Lakini hamwamini, kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. |
| BSB 27 My sheep listen to My voice; I know them, and they follow Me. | SWKCV 27 Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata, |
| BSB 28 I give them eternal life, and they will never perish. No one can snatch them out of My hand. | SWKCV 28 nami ninawapa uzima wa milele, hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu. |
| BSB 29 My Father who has given them to Me is greater than all. No one can snatch them out of My Father’s hand. | SWKCV 29 Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwapokonya kutoka mikononi mwake. |
| BSB 30 I and the Father are one.” | SWKCV 30 Mimi na Baba yangu tu umoja.” |
| BSB 31 At this, the Jews again picked up stones to stone Him. | SWKCV 31 Kwa mara nyingine Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo, |
| BSB 32 But Jesus responded, “I have shown you many good works from the Father. For which of these do you stone Me?” | SWKCV 32 lakini Yesu akawaambia, “Nimewaonyesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni ipi katika hiyo mnataka kunipiga mawe?” |
| BSB 33 “We are not stoning You for any good work,” said the Jews, “but for blasphemy, because You, who are a man, make Yourself out to be God.” | SWKCV 33 Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa sababu ya mambo mema uliyotenda, bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ingawa ni mwanadamu unajifanya kuwa Mungu.” |
| BSB 34 Jesus replied, “Is it not written in your Law: ‘I have said you are gods’? | SWKCV 34 Yesu akawajibu, “Je, haikuandikwa katika Sheria ya kwamba, ‘Nimesema kuwa, ninyi ni miungu?’ |
| BSB 35 If he called them gods to whom the word of God came—and the Scripture cannot be broken— | SWKCV 35 Kama aliwaita ‘miungu,’ wale ambao neno la Mungu liliwafikia, nayo Maandiko hayawezi kutanguka, |
| BSB 36 then what about the One whom the Father sanctified and sent into the world? How then can you accuse Me of blasphemy for stating that I am the Son of God? | SWKCV 36 je, mwawezaje kusema kwamba yule ambaye Baba amemweka wakfu na kumtuma ulimwenguni anakufuru, kwa sababu nilisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu?’ |
| BSB 37 If I am not doing the works of My Father, then do not believe Me. | SWKCV 37 Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msiniamini, |
| BSB 38 But if I am doing them, even though you do not believe Me, believe the works themselves, so that you may know and understand that the Father is in Me, and I am in the Father.” | SWKCV 38 lakini ikiwa nazifanya kazi za Mungu, hata kama hamniamini mimi ziaminini hizo kazi, ili mpate kujua na kuelewa kwamba Baba yu ndani yangu, nami ndani yake.” |
| BSB 39 At this, they tried again to seize Him, but He escaped their grasp. | SWKCV 39 Ndipo wakajaribu kumkamata kwa mara nyingine, lakini akaponyoka kutoka mikononi mwao. |
| BSB 40 Then Jesus went back across the Jordan to the place where John had first been baptizing, and He stayed there. | SWKCV 40 Akaenda tena ngʼambo ya Mto Yordani mpaka mahali pale ambapo Yohana alikuwa akibatiza hapo awali, naye akakaa huko. |
| BSB 41 Many came to Him and said, “Although John never performed a sign, everything he said about this man was true.” | SWKCV 41 Watu wengi wakamjia, nao wakawa wakisema, “Yohana hakufanya muujiza wowote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.” |
| BSB 42 And many in that place believed in Jesus. | SWKCV 42 Nao wengi wakamwamini Yesu huko. |
Questions about John 10? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.