John 4
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 When Jesus realized that the Pharisees were aware He was gaining and baptizing more disciples than John | SWKCV 1 Mafarisayo wakasikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kubatiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana, |
| BSB 2 (although it was not Jesus who baptized, but His disciples), | SWKCV 2 ingawa kwa kweli si Yesu mwenyewe aliyekuwa akibatiza, ila ni wanafunzi wake. |
| BSB 3 He left Judea and returned to Galilee. | SWKCV 3 Bwana alipojua mambo haya, aliondoka Uyahudi akarudi tena Galilaya. |
| BSB 4 Now He had to pass through Samaria. | SWKCV 4 Wakati huo ilimlazimu apitie Samaria. |
| BSB 5 So He came to a town of Samaria called Sychar, near the plot of ground that Jacob had given to his son Joseph. | SWKCV 5 Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yosefu. |
| BSB 6 Since Jacob’s well was there, Jesus, weary from His journey, sat down by the well. It was about the sixth hour. | SWKCV 6 Huko ndiko kulikokuwa na kile kisima cha Yakobo. Naye Yesu alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana. |
| BSB 7 When a Samaritan woman came to draw water, Jesus said to her, “Give Me a drink.” | SWKCV 7 Mwanamke mmoja Msamaria akaja kuteka maji, Yesu akamwambia, “Naomba maji ninywe.” |
| BSB 8 (His disciples had gone into the town to buy food.) | SWKCV 8 (Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.) |
| BSB 9 “You are a Jew,” said the woman. “How can You ask for a drink from me, a Samaritan woman?” (For Jews do not associate with Samaritans.) | SWKCV 9 Yule mwanamke Msamaria akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” (Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.) |
| BSB 10 Jesus answered, “If you knew the gift of God and who is asking you for a drink, you would have asked Him, and He would have given you living water.” | SWKCV 10 Yesu akajibu akamwambia, “Kama ungelijua karama ya Mungu, naye ni nani anayekuambia, Nipe maji ninywe, wewe ungelimwomba yeye, naye angelikupa maji yaliyo hai.” |
| BSB 11 “Sir,” the woman replied, “You have nothing to draw with and the well is deep. Where then will You get this living water? | SWKCV 11 Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji ya uzima utayapata wapi? |
| BSB 12 Are You greater than our father Jacob, who gave us this well and drank from it himself, as did his sons and his livestock?” | SWKCV 12 Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?” |
| BSB 13 Jesus said to her, “Everyone who drinks this water will be thirsty again. | SWKCV 13 Yesu akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena. |
| BSB 14 But whoever drinks the water I give him will never thirst. Indeed, the water I give him will become in him a fount of water springing up to eternal life.” | SWKCV 14 Lakini yeyote anywaye maji nitakayompa hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika uzima wa milele.” |
| BSB 15 The woman said to Him, “Sir, give me this water so that I will not get thirsty and have to keep coming here to draw water.” | SWKCV 15 Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena na wala nisije tena hapa kuteka maji!” |
| BSB 16 Jesus told her, “Go, call your husband and come back.” | SWKCV 16 Yesu akamjibu, “Nenda ukamwite mumeo, uje naye hapa.” |
| BSB 17 “I have no husband,” the woman replied. Jesus said to her, “You are correct to say that you have no husband. | SWKCV 17 Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.” Yesu akamwambia, “Umesema kweli kuwa huna mume. |
| BSB 18 In fact, you have had five husbands, and the man you now have is not your husband. You have spoken truthfully.” | SWKCV 18 Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanaume unayeishi naye sasa si mume wako! Umesema ukweli.” |
| BSB 19 “Sir,” the woman said, “I see that You are a prophet. | SWKCV 19 Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. |
| BSB 20 Our fathers worshiped on this mountain, but you Jews say that the place where one must worship is in Jerusalem.” | SWKCV 20 Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.” |
| BSB 21 “Believe Me, woman,” Jesus replied, “a time is coming when you will worship the Father neither on this mountain nor in Jerusalem. | SWKCV 21 Yesu akamjibu, “Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. |
| BSB 22 You worship what you do not know; we worship what we do know, for salvation is from the Jews. | SWKCV 22 Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi. |
| BSB 23 But a time is coming and has now come when the true worshipers will worship the Father in spirit and in truth, for the Father is seeking such as these to worship Him. | SWKCV 23 Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. |
| BSB 24 God is Spirit, and His worshipers must worship Him in spirit and in truth.” | SWKCV 24 Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” |
| BSB 25 The woman said, “I know that Messiah” (called Christ) “is coming. When He comes, He will explain everything to us.” | SWKCV 25 Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masiya (aitwaye Kristo) anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.” |
| BSB 26 Jesus answered, “I who speak to you am He.” | SWKCV 26 Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye.” |
| BSB 27 Just then His disciples returned and were surprised that He was speaking with a woman. But no one asked Him, “What do You want from her?” or “Why are You talking with her?” | SWKCV 27 Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?” |
| BSB 28 Then the woman left her water jar, went back into the town, and said to the people, | SWKCV 28 Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaambia watu, |
| BSB 29 “Come, see a man who told me everything I ever did. Could this be the Christ?” | SWKCV 29 “Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Kristo?” |
| BSB 30 So they left the town and made their way toward Jesus. | SWKCV 30 Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu. |
| BSB 31 Meanwhile the disciples urged Him, “Rabbi, eat something.” | SWKCV 31 Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Rabi, kula angalau chochote.” |
| BSB 32 But He told them, “I have food to eat that you know nothing about.” | SWKCV 32 Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.” |
| BSB 33 So the disciples asked one another, “Could someone have brought Him food?” | SWKCV 33 Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?” |
| BSB 34 Jesus explained, “My food is to do the will of Him who sent Me and to finish His work. | SWKCV 34 Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake. |
| BSB 35 Do you not say, ‘There are still four months until the harvest’? I tell you, lift up your eyes and look at the fields, for they are ripe for harvest. | SWKCV 35 Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune?’ Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa! |
| BSB 36 Already the reaper draws his wages and gathers a crop for eternal life, so that the sower and the reaper may rejoice together. | SWKCV 36 Mvunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele. Ili yeye apandaye na yeye avunaye wafurahi pamoja. |
| BSB 37 For in this case the saying ‘One sows and another reaps’ is true. | SWKCV 37 Hivyo kule kusema, ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa. |
| BSB 38 I sent you to reap what you have not worked for; others have done the hard work, and now you have taken up their labor.” | SWKCV 38 Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.” |
| BSB 39 Many of the Samaritans from that town believed in Jesus because of the woman’s testimony, “He told me everything I ever did.” | SWKCV 39 Wasamaria wengi katika mji ule wakamwamini Yesu kwa sababu ya ushuhuda wa yule mwanamke alipowaambia kwamba, “Ameniambia kila kitu nilichotenda.” |
| BSB 40 So when the Samaritans came to Him, they asked Him to stay with them, and He stayed two days. | SWKCV 40 Hivyo wale Wasamaria walipomjia, wakamsihi akae kwao. Naye akakaa huko siku mbili. |
| BSB 41 And many more believed because of His message. | SWKCV 41 Kwa sababu ya neno lake, watu wengi wakaamini. |
| BSB 42 They said to the woman, “We now believe not only because of your words; we have heard for ourselves, and we know that this man truly is the Savior of the world.” | SWKCV 42 Wakamwambia yule mwanamke, “Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu, bali kwa kuwa tumemsikia sisi wenyewe. Tumejua hakika kweli ya kwamba huyu ndiye Kristo, Mwokozi wa ulimwengu.” |
| BSB 43 After two days, Jesus left for Galilee. | SWKCV 43 Baada ya zile siku mbili, Yesu aliondoka kwenda Galilaya. |
| BSB 44 Now He Himself had testified that a prophet has no honor in his own hometown. | SWKCV 44 (Basi Yesu mwenyewe alikuwa amesema kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe.) |
| BSB 45 Yet when He arrived, the Galileans welcomed Him. They had seen all the great things He had done in Jerusalem at the feast, for they had gone there as well. | SWKCV 45 Alipofika Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha, kwani walikuwa wameona yale aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Pasaka. Kwa maana wao pia walikuwa wamehudhuria hiyo Sikukuu. |
| BSB 46 So once again He came to Cana in Galilee, where He had turned the water into wine. And there was a royal official whose son lay sick at Capernaum. | SWKCV 46 Hivyo Yesu akaja tena mpaka Kana ya Galilaya, kule alikokuwa amebadili maji kuwa divai. Huko kulikuwepo na afisa mmoja wa mfalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu. |
| BSB 47 When he heard that Jesus had come from Judea to Galilee, he went and begged Him to come down and heal his son, who was about to die. | SWKCV 47 Huyo mtu aliposikia kwamba Yesu alikuwa amewasili Galilaya kutoka Uyahudi, alimwendea na kumwomba ili aje kumponya mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa. |
| BSB 48 Jesus said to him, “Unless you people see signs and wonders, you will never believe.” | SWKCV 48 Yesu akamwambia, “Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.” |
| BSB 49 “Sir,” the official said, “come down before my child dies.” | SWKCV 49 Yule afisa wa mfalme akamwambia, “Bwana, tafadhali shuka kabla mwanangu hajafa.” |
| BSB 50 “Go,” said Jesus. “Your son will live.” The man took Jesus at His word and departed. | SWKCV 50 Yesu akamjibu, “Enenda zako, mwanao yu hai.” Yule afisa akaamini yale maneno Yesu aliyomwambia, akaondoka akaenda zake. |
| BSB 51 And while he was still on the way, his servants met him with the news that his boy was alive. | SWKCV 51 Alipokuwa bado yuko njiani, akakutana na watumishi wake wakamwambia kwamba mwanawe yu mzima. |
| BSB 52 So he inquired as to the hour when his son had recovered, and they told him, “The fever left him yesterday at the seventh hour.” | SWKCV 52 Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.” |
| BSB 53 Then the father realized that this was the very hour in which Jesus had told him, “Your son will live.” And he and all his household believed. | SWKCV 53 Ndipo baba wa huyo mtoto akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Yesu alikuwa amemwambia, “Mwanao yu hai.” Kwa hiyo yeye pamoja na wote wa nyumbani mwake wakamwamini Yesu. |
| BSB 54 This was now the second sign that Jesus performed after coming from Judea into Galilee. | SWKCV 54 Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Yesu alifanya aliporudi Galilaya kutoka Uyahudi. |
Questions about John 4? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.